Watu Wengi Wamekuwa Wakishangaa Kwamba Kuna Maeneo Mengi Ya Uchaggani, Kilimanjaro Yanafaanana Majina na Kushindwa Kuelewa Mara Moja Sababu Yake Nini. Japo Kweli Sababu Yake Haiko Wazi Kabisa Lakini Inajulikana Kwamba Zamani Wachagga, Kilimanjaro Walikuwa Ni Watu wa Kuhama Sehemu Moja Ya Kilimanjaro Kwenda Sehemu Nyingine Kwa Sababu Mbalimbali.Lakini Kuna Nyakati Uchaggani Kabla Ya Karne Ya 20, Ilikuwa Ni Sera za Koo Nyingi za Uchagga Kutoa Matawi Ambayo Yalisambaa Maeneo Mbalimbali Ndani Ya Kilimanjaro Ili Kuhakikisha Kwamba Wanakuwa na Matawi Maeneo Mengi Kwa Tahadhari Pale Inapotokea Changamoto Kwenye Eneo Moja Basi Eneo Jingine Ndio Linatoa “Backup” Kama Ugonjwa Vita Njaa N.k.,
Japo Waliendelea Kutembeleana na Kufanya Sherehe Zote na Mila Zote Kwa Pamoja, Pamoja na Kusadiana. Suala Hili Ameliandika Charles Dundas Kwenye “Kilimanjaro and It’s People”. Sasa Nadharia Ya Hili Ni Kwamba Watu Walipohamia Eneo Fulani Hasa Kijiji au Mtaa Kwa Wingi Ndio Unakuta Wanahama na Jina La Eneo Walilotoka.Kwa Utafiti Tuliofanya na Kutembelea Tumegundua Kwamba Kuna Maeneo Mengi Sana Ya Kilimanjaro Yanayofanana Majina Hasa Vitongoji Na Maeneo Mengine Ya Kilimanjaro Kiasi Kwamba Ni Vigumu Kuwa Imetokea Kwa Bahati Mbaya, Japo Wachagga wa Leo Wengi Hawajui Kama Kuna Eneo Jingine Lina Jina Kama La Eneo Lao.Orodha Ya Maeneo Yanayofanana Majina Uchaggani, Kilimanjaro na Mahali Yanapopatikana na Hadhi Ya Eneo Husika Hii Hapa:-
1. MACHAME.
– Machame ni Tarafa katika Jimbo la Hai.
– Machame ni kijiji katika kata ya Aleni, Keni Aleni Rombo.
– Machame ni Kitongoji katika kijiji cha Maringa, Mwika Kaskazini.
– Machame Kinyasini ni Kitongoji katika kijiji cha Ushiri, kata ya Ushiri/Ikuini, Mkuu Rombo.
– Machame ni Kitongoji katika kijiji cha Sangasa, Usseri, Rombo.
2. MARANGU.
– Marangu ni Tarafa katika Jimbo la Vunjo.
– Marangu ni kijiji katika kata ya Olele, Rombo.
– Marangu ni Kitongoji katika kijiji cha Mrere, Mashati, Rombo.
3. USSERI.
– Usseri ni Tarafa katika Jimbo la Rombo.
– Usseri ni Kitongoji katika kijiji cha Uduru, Machame Kaskazini.
4. TELLA.
– Tella ni kijiji, Old Moshi.
– Tella ni Kitongoji katika KIJIJI cha SAMANGA, Marangu.
– Tella ni Kitongoji katika KIJIJI cha Koresa, Kirua Vunjo.
– Tella ni Kitongoji katika KIJIJI cha IWA, Kirua Vunjo.
– Tella ni KIJIJI katika Kata ya Narumu, Machame.
5. MENGENI.
– Mengeni ni Kitongoji katika Kijiji cha Kisaseni, Old Moshi.
– Mengeni ni Kitongoji katika Kijiji cha Kondeni, Mwika.
– Mengeni ni Kitongoji katika Kijiji cha Kitowo, Marangu.
– Mengeni ni Kitongoji katika Kijiji cha Ruwa Kilema.
– Mengeni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Kilema chini, Kilema.
– Mengeni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Mrumeni, Kirua Vunjo.
– Mengeni ni Shule katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.
– Mengeni ni Shule katika KIJIJI cha Marangu, Olele Rombo.
– Mengeni ni Kata katika Tarafa ya Keni, Rombo.
6. SANGO.
– Sango ni Kijiji, Old Moshi.
– Sango ni Kitongoji, katika Kijiji cha Makami Juu, Kilema.
– Sango ni Kitongoji Katika Kijiji cha Makami Chini, Kilema.
– Sango ni Usharika katika kijiji cha Samaki Maini, Siha.
– Sango ni Kitongoji katika Kijiji cha Samanga, Usseri, Rombo.
7. KILEMA.
– Kilema ni Tarafa katika Jimbo la Vunjo.
– Kilema ni kijiji katika kata ya Olele, Rombo.
– Kilema ni Kitongoji katika kijiji cha Mengwe chini, kata ya Mengwe, Rombo.
8. TSUDUNYI.
– Tsudunyi ni KIJIJI, Old Moshi.
– Tsuduni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Mwasi Kaskazini, Uru mashariki.
9. SAMANGA.
– Samanga ni kijiji, Marangu.
– Samanga ni Kitongoji katika kijiji cha Kisale, Mashati Rombo.
– Samanga ni kijiji katika Tarafa ya Usseri, Rombo.
– Samanga ni Kitongoji katika kijiji cha Saawe, Masama.
10. MAMBA.
– Mamba ni Tarafa katika Jimbo la Vunjo.
– Mamba ni kijiji sambamba na Uswaa, katika kata ya Machame Uroki, Machame.
– Mamba ni Kitongoji katika kijiji cha Sangasa, Usseri, Rombo.
11. MWIKA.
– Mwika ni Kitongoji katika kijiji cha Tema, Kata ya Mbokomu, Old Moshi.
– Mwika ni Tarafa katika Jimbo la Vunjo.
12. KIRUWENI.
– Kiruweni ni kijiji, Mwika.
– Kiruweni ni Kitongoji katika kijiji cha Shimbi Kati, Shimbi Mkuu, Rombo.
– Kiruweni ni Kitongoji katika kijiji cha Kooti, Kata ya Olele, Rombo.
13. KOMAKUNDI.
– Komakundi ni kijiji, Mamba Kaskazini katika Jimbo la Vunjo.
– Komakundi ni Kitongoji katika kijiji cha Lole Marera, Mwika Kaskazini.
14. KIRUA.
– Kirua ni Tarafa katika Jimbo la Vunjo.
– Kirua ni Kijiji katika katika kata ya Kirwakeni, Mashati, Rombo.
– Kirua ni Kitongoji katika kijiji cha Matala, Mwika Kusini.
15. NGASINYI.
– Ngasinyi ni Kitongoji katika kijiji cha Kisaseni, Old Moshi.
– Ngasinyi ni Kitongoji katika Kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi. – Ngasinyi, Kijiji Kahe.
– Ngasinyi ni Kitongoji katika Kijiji cha Kirisha, Siha/Sanya Juu.
– Ngasinyi ni Kitongoji katika Kijiji cha Mdawi, Old Moshi.
16. OLELE.
– Olele ni Kitongoji katika kijiji cha Mweka, Kibosho mashariki.
– Olele ni kata iliyopo kati ya Mashati na Usseri, Rombo.
17. MORI.
– Mori ni Kitongoji katika KIJIJI cha Tella, Old Moshi.
– More ni Kitongoji katika KIJIJI cha KIMANGARO, Mwika.
– Moori ni Kitongoji katika KIJIJI cha Lyamrakana, Marangu.
– Mori ni Kitongoji katika KIJIJI cha Arisi, Marangu.
18. KITANDU.
– Kitandu ni KIJIJI katika kata ya Uru Kusini.
– Kitandu ni kijiji katika KATA ya Kibosho Okaoni.
19. KITOWO.
– Kitowo ni Kitongoji katika kijiji cha Materuni, Uru Mashariki.
– Kitowo ni kijiji, Marangu.
– Kitowo ni kijiji katika kata ya Olele, Rombo.
– Kitowo ni Kitongoji katika kijiji cha Kimbogho, Mamba Kusini.
20. KITONGORIA.
– Kitongoria ni Kitongoji katika KIJIJI cha Ushiri, Rombo.
– Kitongoria ni Kitongoji katika KIJIJI cha Kitowo kata ya Olele, Rombo.
– Kitongoro ni Kitongoji katika Kijiji cha Shinga, Uru.
21. NGANYENI.
– Nganyeni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Kishumundu, Uru Mashariki.
– Nganyeni ni kijiji Msae, Mwika. – Nganyeni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Mengwe Juu, Rombo.
22. MSESEWENI.
– Mseseweni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Mwasi Kaskazini, Uru mashariki.
– Maseseweni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Uri, Kibosho.
– Mseseweni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Msae Kinyamvuo, Mwika.
23. SERAMFO.
– Seramfo ni Kitongoji katika KIJIJI cha Kishumundu, Uru.
– Seramfo ni Kitongoji katika KIJIJI cha Mwasi Kaskazini Uru.
24. KIFUMBU.
– Kifumbu ni Kitongoji katika KIJIJI cha Kishumundu, Uru Mashariki.
– Kifumbu ni Kitongoji katika KIJIJI cha Kitandu, Uru Kusini.
25. KIFUNI.
– Kifuni ni Kitongoji katika KIJIJI cha Kishumundu, Uru mashariki.
– Kifuni ni kijiji katika kata ya Kibosho Okaoni.
26. MAMBOLEO.
– Mamboleo ni Kitongoji katika kijiji cha Mwasi Kusini, Uru mashariki.
– Mamboleo ni Kitongoji katika KIJIJI cha MSANGAI, Tarakea, Rombo.
27. NGARUMA
– Ngaruma ni Kitongoji katika kijiji cha Shimbwe Juu, Uru.
– Ngaruma ni shule na Usharika katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.
28. TEMA.
– Tema ni Kijiji, Katika Kata ya Mbokomu, Old Moshi.
– Tema ni Kitongoji katika kijiji cha Mboreny, Masama Mashariki.
– Tema ni Kitongoji katika kijiji cha Sonu, Masama mashariki.
29. NGIRINY
– Ngiriny ni Kitongoji katika Kijiji cha Kirima Kati, Kibosho.
– Ngiriny ni mtaa katika kijiji cha Lukani, Masama.
– Ngiriny ni Kijiji katika kata ya Ngiriny, Siha/Sanya juu.
30. NGANGU.
– Ngangu ni Kitongoji katika kijiji cha Kindi, kata ya Kindi, Kibosho.
– Ngangu ni Kijiji, Kilema.
31. KIMARORONI.
– Kimaroroni ni Kitongoji katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.
– Kimaroroni ni Kijiji, Kilema.
32. KYUU.
– Kyuu ni Kitongoji katika kijiji cha Ngangu, Kilema.
– Kyuu ni Kijiji, Masama Magharibi.
33. MKUU.
– Mkuu ni Kitongoji katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.
– Mkuu ni Tarafa katika Jimbo la Rombo. – Nkuu ni kijiji, Machame.
34. FUMVUNI.
– Fumvuni ni Kitongoji katika kijiji cha Leghomulo, Kilema.
– Fumvuni ni Kitongoji katika kijiji cha Kwamare, Kirua Vunjo.
35. USAGARA.
– Usagara ni Kitongoji katika kijiji cha Kilema chini, Kilema.
– Usagara ni Shule katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.
36. OMARINI.
– Omarini ni kijiji katika kata ya Kibosho Okaoni.
– Umarini ni Kitongoji katika kijiji cha Kirongo chini, Usseri, Rombo.
– Umarini ni Kitongoji katika kijiji cha Kisale, Mashati, Rombo.
37. KOLILA.
– Kolila ni Kitongoji katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.
– Kolila ni Shule/Eneo katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.
38. SISA.
– Sisa ni Kitongoji katika kijiji cha Sisamaro, Kibosho.
– Sisa ni Kitongoji katika kijiji cha Mkomilo, Kibosho.
39. SAWE.
– Sawe ni Kitongoji katika kijiji cha Mkomilo, Kibosho.
– Saawe Ni Kijiji katika KATA ya Masama Mashariki.
40. SAA.
– Saa ni Kitongoji katika kijiji cha Uchau Kaskazini, Kibosho Kati.
– Saa ni Kitongoji katika kijiji cha Lyamungo Sinde, Machame.
41. MAUA.
– Maua ni Kijiji katika kata ya Kibosho kati, Kibosho.
– Maua ni Shule na eneo katika kijiji cha Kyou, Kilema.
42. SINGA.
– Singa ni Kijiji, Kibosho mashariki.
– Singa ni Kitongoji katika kijiji cha Kwalakamu, Usseri, Rombo.
43. MBORENI.
– Mboreni ni Kitongoji katika kijiji cha Sungu, Kibosho mashariki.
– Mboreny ni kijiji katika kata ya Masama mashariki.
44. MRITI.
– Mriti ni Kitongoji katika kijiji cha Matala, Mwika Kusini.
– Mriti ni shule katika kata ya Mahida, Mamsera Rombo.
45. KISHINGONY.
– Kishingony ni Kitongoji katika kijiji cha Uuwo, Mwika.
– Kishingony ni Kitongoji katika kijiji cha Mamsera kati, Mamsera, Rombo.
46. CHONA.
– Chona ni Kitongoji katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika Kaskazini.
– Nchona ni Kitongoji katika kijiji cha Uchau Kusini, Kibosho kati.
47. RAUYA.
– Rauya ni kijiji, Marangu mashariki.
– Rauya ni Kitongoji katika kijiji cha Kiria, Mamba Kusini.
48. MASIA.
– Masia Mamba ni Kitongoji katika kijiji cha Kokirie, Mamba Kaskazini.
– Masia ni Kitongoji katika kijiji cha Yamu, Kirua Vunjo Kusini.
49. MAUWO.
– Mauwo ni Kitongoji katika kijiji cha Samanga Marangu.
– Mauwo ni Kitongoji katika kijiji cha Ashira, Marangu.
50. MSHIRI.
– Mshiri ni Kijiji, Marangu.
– Mshiri ni Kitongoji katika kijiji cha Ashira, Marangu.
– Ushiri ni Kijiji na ni Kata pia, Katika Tarafa ya Mkuu, Rombo.
51. KIRARACHA.
– Kiraracha ni kijiji, Marangu.
– Kiraracha ni Kitongoji katika kijiji Yamu, Kirua Vunjo Kusini.
52. MRIA.
– Mria ni Kitongoji katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.
– Mria ni Kitongoji katika kijiji cha Mwasi Kaskazini, Uru mashariki.
53. LOLE.
– Lole ni kijiji, Mwika Kaskazini.
– Lole ni Kitongoji katika cha Manu, Kirua Vunjo Magharibi.
54. KIRIMA.
– Kirima ni Kijiji na kata, Kibosho.
– Kirima ni Kitongoji katika kijiji cha Longoi kata ya Weruweru.
55. MSARANGA.
– Msaranga ni kijiji na ni kata katika Tarafa ya Mashati, Rombo.
– Msaranga ni kijiji na ni kata Upande wa Kusini wa Old Moshi.
56. MBWEERA.
– Mbweera ni kijiji katika kata ya Masama mashariki.
– Mbweera ni Kitongoji katika kijiji cha Uswaa, Machame.
57. URAA.
– Uraa ni kijiji katika kata ya Masama Kusini.
– Uraa ni Kitongoji katika kijiji cha Wari Sinde, Machame Kaskazini.
58. KYALIA.
– Kyalia ni Kitongoji katika kijiji cha Foo, Machame.
– Kyalia ni Kitongoji katika kijiji cha Wari Ndoo, Machame.
59. NDUWENI.
– Nduweni ni Kijiji, Marangu Magharibi.
– Nduweni ni Kitongoji katika kijiji cha Mbomai, Tarakea, Rombo.
60. MIASENI.
– Miaseni ni Kitongoji katika kijiji cha Ngira, Masama mashariki.
– Miaseni ni Kitongoji katika kijiji cha Nronga, Machame Magharibi.
61. NGARONY.
– Ngarony ni kijiji katika kata ya Livishi, Siha/Sanya Juu.
– Ngarony ni Shule katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.
62. MLAMBAI.
– Mlambai ni Kitongoji katika kijiji cha Ngoyoni, Mengwe, Rombo.
– Mlambai ni Kitongoji katika kijiji cha Shimbi Mashami, Shimbi, Mkuu, Rombo.
63. MRAO.
– Mrao ni kijiji katika kata ya Mraokeryo, Mashati, Rombo.
– Mrao ni Kitongoji katika kijiji cha Mengeni chini, kata ya Mengeni, Keni Rombo.
64. KITIRIMA.
– Kitirima ni kata katika Tarafa ya Usseri, Rombo.
– Kitirima ni Kitongoji katika kijiji cha Shimbi Masho, Shimbi, Mkuu, Rombo.
65. KENI.
– Keni ni Tarafa katika Jimbo la Rombo.
– Keni ni Kijiji katika kata ya Kirwakeni, Mashati, Rombo.
66. MLEMBEA.
– Mlembea ni Kitongoji katika kijiji cha Kooti katika kata ya Olele, Rombo.
– Mlembea ni Kitongoji katika kijiji cha Kirongo juu, Usseri, Rombo.
67. MAWELA.
– Mawela ni Kitongoji katika kijiji cha Kooti katika kata ya Olele, Rombo.
– Mawela ni mtaa katika kijiji cha Kimanganuni, Uru Kusini.
68. MRUWIA.
– Mruvia ni Kitongoji katika kijiji cha Kirongo chini, Usseri, Rombo.
– Mruwia ni kijiji katika kata ya Uru Mashariki.
Whatsapp +255 754 584 270.
Email: urithiwetuwachagga@gmail.com