WACHAGGA WAHAFIDHINA vs WACHAGGA MALIBERALI.

Linapokuja suala la kutunza tamaduni siku zote watu hugawanyika katika pande kuu mbili japo wachache hubaki katikati. Kuna wale wa mrengo wa kulia ambao ndio huitwa wahafidhina(conservatives) na wale wa mrengo wa kushoto ambao huitwa *maliberali(liberals)*(huru).Hata miongoni mwetu Wachagga wapo wahafidhina ambao ndio huitwa wa mrengo wa kulia na wapo maliberali ambao huitwa wa mrengo wa kushoto.

Wachagga wahafidhina ni Wachagga ambao wanapigania au kuunga mkono kulindwa, kutunzwa, kuhifadhiwa na kuenziwa kwa tamaduni, hadhi, utukufu na mambo yote yaliyowapa Wachagga umashuhuri na ufahari ambao wamekuwa wanajivunia kwa miaka mingi, wakati Wachagga maliberali wanaona mambo ya kuhifadhi au kuenzi tamaduni hayana haja ya kupewa uzito na hawaoni umuhimu wa kutunza au kujivunia chochote bali maisha yaende popote yanapokwenda ili mradi mtu anaishi kwa uhuru na amani na anaweza kubadilika mwenyewe na kuchagua aina yoyote ya maisha itakayompendeza bila kujihangaisha kuenzi tamaduni za asili.

Mfano wa makundi mengine unaoweza kufanana na huu, ni kwenye biblia katika dini ya Wayahudi kati Mafarisayo na Masadukayo. Wakati mafarisayo wakipigania kuenzi na kubaki na tamaduni za kiyahudi katika dini bila kuchanganyika na watu wa mataifa(gentiles), Masadukayo wao walikuwa wanaunga mkono kuchanganya Uyahudi na baadhi ya tamaduni za Wayunani(Ancient Greece) ambao walikuwa ndio wasomi zaidi wa kale na waliokuwa na ushawishi mkubwa kwa dunia ya kale ikiwa ni pamoja na himaya ya Rumi ya kale(Ancient Rome) iliyokuja kuwa na nguvu sana kwa dunia ya kale na kuendelea kuwa msingi wa tamaduni za kimagharibi mpaka leo hii. Lakini hata hivyo japo Masadukayo walionekano kama ndio wasomi wanaokwenda na wakati kwa nyakati zile za utukufu na umashuhuri wa Wayunani na baadaye Warumi, lakini ni Mafarisayo ambao ndio kama wahafidhina wa kiyahudi ambao walisaidia zaidi tamaduni za kiyahudi kutunzwa na kuendelea kuwepo mpaka sasa.

Hata ma-Rabbi wa dini ya kiyahudi wa leo hii wanakiri kwamba sehemu kubwa ya mafundisho yao imetokana zaidi na mafundisho ya Mafarisayo kuliko mafundisho ya kundi lingine lolote ndani ya dini ya kiyahudi zamani na wanaona kwamba Mafarisayo walifanya kazi muhimu zaidi katika kuhifadhi dini na tamaduni za kiyahudi zilizochangia kuendelea kuwepo kwa dini ya kiyahudi mpaka leo hii ambayo pia ndio msingi wa ukristo. Kwa upande wetu Wachagga wahafidhina wanataka ushirikiano zaidi baina ya Wachagga, mwingiliano zaidi baina yetu, kutunza na kuelimishana kuhusu historia, tamaduni zote, maadili ya kichagga na kila kizuri kuhifadhiwa, kutunzwa na kuenziwa.

Wachagga wahafidhina wanataka kuona mila na desturi za wachagga zikiendelea kuwepo na kudumu kwa maelfu ya vizazi vitakavyoendelea kufanya mambo makubwa na kurithisha tamaduni hizi na historia kubwa iliyojaa utukufu ndani yake kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine na kutotamani kuona mila, desturi, tamaduni na historia yetu vikipotea na kusahaulika kabisa baada ya vizazi vichache kupita.

Kwa upande wa Wachagga maliberali wao hawaoni kama yote haya yana umuhimu wowote, wao kikubwa kuwe na haki, utulivu, amani na maendeleo haya mengine hayana maana, maliberali hawaoni kama kuna haja ya maadili na wanaunga mkono mabadiliko yote ya kijamii kama mienendo ya vijana kutothamini sana maadili na tamaduni zilizopita na kuiga tamaduni zozote zinazoonekana kwenda na wakati, hawajali kuhusu mavazi, vyakula, nyimbo, ngoma, ardhi ya urithi, lugha ya asili ya kichagga, wala urithi wowote ulioachwa kutokea vizazi vilivyopita, badala yake wanaunga mkono kuishi vyovyote unavyofurahia wewe haijalishi sana kama unaendana na maadili ya jamii yako au hauendani nayo.

Karibu kwa maoni, ushauri na Mchango zaidi.

Wewe ni Mchagga Mhafidhina au Mliberali?

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

11 Comments

  1. Shedrack Makundi says:

    Mie napenda watu waelewe kuwa kutunza na kuhifadhi desturi na mila za kabila fulani sio kosa, kuna mengi ya kijifunza na mengi mazuri ya kudumisha

  2. Good

  3. Uko sahihi kabisa Mr. Makundi watu wamepotoshwa sana mambo mengi, Lakini sisi hatuna haja ya kibishana wala kushindana na mtu sisi tufanye kazi ya kuandika na kuelimisha taratibu jambo hili litaonekana ni la kawaida na jamii nyingine wenye kutamani kufanya hivi wataiga.

    Sisi Urithi Wetu Wachagga tutaendelea kuandika na kuja na ubunifu mpya bila kuacha na watu wataendelea kuelewa.

    Siku zote kitu kipya hakieleweki lakini kuna mahali itafika itakuwa ndio habari ya mjini.

  4. Everlyn Nicodemus says:

    Aika .

    Ninasoma Habari za Wachagga .

    Aika.

    Dr EVERLYN NICODEMUS PhD.

    Artist /writer/ Art historian.

    Aika.

    Ruwa Lutarame.

    EVERLYN .
    Urithi wa Wachagga

  5. Innocent William Mushi says:

    Asante sana kwa andiko hili, ni vyema historia yetu tuka itunza na kuihifadhi kisasa hivi.
    Mimi binafsi ni muhanga wa Wachaga Maliberali. Naona aibu kua siwezi kuongea kichaga fluent kwakua wazazi hawakuona fahari sie watoto kujua lugha yetu ya asili.
    Mimi nimeamua kubadilika na kufuata tamaduni na nimeanza kwa kumpa binti yangu jina la kichaga. Anaitwa Aika. Na kwasasa sina mpango wa kuwapa wanangu majina ya kizungu. Ninaona fahari kuwa mchagga na najivunia historia yetu na tamaduni zetu.

    1. Hongera sana Mr. Innocent Mushi.

      Tunaianza safari hiyo na hatutarudi nyuma kamwe.

  6. Hongera sana Mr. Innocent Mushi.

    Uko sahihi kabisa na unafanya vizuri sana

  7. Sisti Marishay says:

    Hongera sana Kwa Malala nzuri

  8. Mimi nina watoto wanner, na nimewapa majina ya kichagga.
    Simbaufoo, kundaeli, Aikaeli, na arafumin

    1. Safii sana, naamini hayo ndio majina yao rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *