KITIMBIRIHU HOLISTIC CENTRE!

KITIMBIRIHU HOLISTIC CENTRE!

  • Ni Mtaa Katika Kijiji Cha Mdawi Ya Juu, Old Moshi.
  • Ni Sehemu Ya Kwanza Ambapo Injili Ya Yesu Kristo Ilianza Kuhuburiwa, Sio Tu Ndani Ya Uchaggani Na Kanda Ya Kaskazini Bali Ni Sehemu Ya Kwanza Kufanyika Ibada Ya Kikristo Katika Tanganyika Nzima Ukiondoa Bagamoyo.
  • KKKT, Dayosisi Ya Kaskazini Walitangaza Rasmi Eneo Hili Kuwa Eneo Takatifu La Kanisa Na Mradi Huo Unaendelea. -Mwaka 1871 Mmisionari Wa Kiingereza Charles New Alifika Old Moshi Na Mangi Rindi Mandara Kumpa Eneo Hili Ili Kuanzisha Shule Rasmi. Hata Hivyo Miaka Michache Baadaye Charles New Alifariki Dunia Akiwa Anaelekea Pwani Kutokea Kilimanjaro.
  • Mwaka 1878 Mangi Rindi Mandara Aliwaandikia Barua Wamisionari wa CMS Society Kutoka London Uingereza Kuja Kuanzisha Shule Rasmi, Kilimanjaro Na Mwaka 1885 Walifika Na Kuanzisha Kituo Cha Misheni Cha Kitimbirihu Na Kufanya Ibada Ya Kwanza Ya Kikristo Tanganyika Ukiondoa Bagamoyo Tarehe 01/Julai/1885. Hata Hivyo Mangi Rindi Mandara Aliwazuia Kutangaza Injili Kilimanjaro Badala Yake Alitaka Waanzishe Shule Na Kufundisha Wananchi Taaluma Mbalimbali.
  • Mwaka 1883 Mpelelezi Na Mwanasayansi wa Kiingereza Sir Harry Hamilton Johnston Alifika Old Moshi, Kilimanjaro Akiwa Na Barua Ya Utambulisho Kutoka Kwa Balozi wa Uingereza Zanzibar Kuja Kwa Mangi Rindi Mandara Na Mangi Rindi Kumtambua Na Kumpa Eneo Hili La Kitimbirihu Aweke Makazi Yake.
  • Mwaka 1892 Baada Ya Mangi Rindi Mandara Kuwa Amefariki Na Old Moshi Ikitawaliwa Na Mtoto Wake Mangi Meli Mandara Wakristo Wa Kwanza Tanganyika Ukiondoa Bagamoyo Walibatizwa Katika Eneo Hili La Kitimbirihu.
  • Hata Hivyo Eneo Hili Halikuendelezwa Sana Na Wamisionari Baada Ya 1892 Kwa Sababu Kanisa Hili Pamoja Na Misheni Yake Vilihamia Katika Kijiji Cha Kidia, Old Moshi.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *