MWANAZUONI WA HISTORIA, TAMADUNI NA MILA ZA KICHAGGA DR. BRUNO GUTTMAN

  • Huyu Aliitwa Dr. Bruno Gutmann, Mmisionari wa Kilutheri na Mwanazuoni wa Mila, Desturi, Tamaduni na Falsafa Mbalimbali za Jamii Ya Wachagga. -Dr. Bruno Gutmann Alizaliwa Tarehe 4/Julai/1876 Katika Mji wa Dresden Huko Nchini Ujerumani.
  • Dr. Bruno Gutmann Aliishi Kilimanjaro Kwa Zaidi Ya Miaka 36 Kuanzia Mwaka 1902 Mpaka Mwaka 1938 Akijifunza Mambo Mbalimbali Kuhusu Jamii Ya Wachagga na Kuandika Vitabu na Makala Nyingi Sana Zinazosemekana Kuwa Ni Zaidi Ya Vitabu na Makala 480.
  • Dr. Bruno Gutmann Alihudumu Machame Magharibi Huko Masama, Mamba Huko Mashariki Ya Marangu na Old Moshi Alikoishi Kwa Miaka Mingi Zaidi na Kuandika Mambo Mengi Zaidi.
  • Dr. Bruno Gutmann Ndiye Mwandishi Aliyeandika Mambo Mengi Kuhusu Wachagga Kuliko Mwandishi Mwingine Yeyote Ambapo Ameandika Vitabu Vingi Vyenye Kurasa Zaidi Ya 700 na Hata Vingine Vyenye Kurasa Zaidi Ya 2,000. Changamoto Pekee Ni Kwamba Maandiko Yake Mengi Bado Yako Kwa Lugha Ya Kijerumani na Machache Yametafsiriwa Kwa Kiingereza.
  • Chuo Kikuu Cha Wurzburg Cha Nchini Ujerumani Kilimtunuku Dr. Bruno Gutmann PhD Ya Heshima Kwa Kitabu Chake Maarufu Sana Cha (Das Recht der Tchagga) au Kwa Kiingereza (Chagga Law) Ambacho Kinasemekana Ndio Kazi Bora Zaidi Ya Uandishi Katika Tasnia Hiyo Afrika Nzima Mpaka Wakati Wake.
  • Dr. Bruno Gutmann Alikuwa na Uzalendo wa Kipekee Kwa Jamii Ya Wachagga na Alikuwa Anapigania Taasisi na Mifumo Ya Kijamii Ya Asili Ya Wachagga Kutovurugwa Bali Kuboreshwa na Kuendelea Kutumika Kama Ilivyo Kwani Alikiri llikuwa ni Mifumo Bora Sana Kuliko Hata Ya Kwao Ujerumani na Inaweza Kuwa na Mafanikio Makubwa Zaidi Ikitumika Kama Ilivyo Bila Kuvurugwa au Kulazimishiwa Mifumo Mingine Isiyo Ya Asili Kwa Wachagga.
  • Dr. Bruno Gutmann Alijifunza Lugha Ya Kichagga na Alikuwa Akiongea Kwa Ufasaha Inasemekana Kuliko Hata Wachagga Wenyewe, na Watoto Wake Wote Aliwapa Majina Ya Kichagga.
  • Kazi Chache za Dr. Bruno Gutmann Zimetafsiriwa Kwa Kiingereza na Nyingi Leo Hii Zinatumika Kufundishia Vyuo Vikuu Mbalimbali Duniani Hasa Vyuo Vya Magharibi Vya Ulaya na Marekani Katika Tasnia Husika.
  • Baada Ya Kurudi Ulaya Mwaka 1938 Kutokana na Misuguano Ya Kisiasa Iliyokuwepo Kati Ya Ujerumani na Uingereza Iliyopeleka Vita Ya Pili Ya Dunia na Hakuweza Tena Kurudi Kilimanjaro Baada Ya Hapo, Dr. Bruno Guttman Aliendelea Kuandika na Kufuatilia Mambo Ya Wachagga na Aliwakaribisha Kwake na Hata Kuishi na Wachagga Waliokwenda Ulaya Miaka Ya 1940s Mpaka 1960s.
  • Dr. Bruno Gutmann Alifariki Tarehe 17/Desemba/1966 Akiwa na Umri wa Miaka 90 Huko Ehingen am Hesselberg Nchini Ujerumani.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *