BUSTANI HALISI YA EDENI – KILIMANJARO.
Kilimanjaro Imekuwa Ni Sehemu Inayovutia Sana Duniani, Pengine Inaongoza Au Ni Moja Ya Maeneo Ya Asili Yenye Kuvutia Sana Duniani.
Mwishoni Mwa Karne Ya 19 Wakati Serikali Ya Ujerumani Ilipoamua Kuja Kuitawala Kilimanjaro Na Kutuma Vijana Wa Kijerumani Kuja Kujitolea Katika Jeshi na Katika Serikali Mpya Ya Kikoloni Vijana Hawa wa Kijerumani Waliita Kilimanjaro “BUSTANI HALISI YA EDEN”. Kilimanjaro Ilipata Umaarufu Huko Ujerumani Kama Bustani Ya Edeni.
Wajerumani Waliamua Kwamba Wataifanya Kilimanjaro Kuwa Makazi Yao Ya Kudumu Na Kuiita “New Germany” au “Ujerumani Mpya”, na Eneo Lote La Kaskazini Ya Tanganyika Liliitwa Kilimanjaro, na Makao Makuu Yake Yakiwa Moshi, Wakati Huo Mji wa Moshi Ukiwa Old Moshi. Wajerumani Walijitahidi Kuijenga Kilimanjaro Kwa Kasi Lakini Baada Ya Kushindwa Vita Ya Kwanza Ya Dunia na Kunyang’anywa Maeneo Yao Kilimanjaro Ilianza Kutawaliwa na Uingereza.
Waingereza Hawakuweka Nguvu Kubwa Sana Kuijenga Kilimanjaro Badala Yake Waliwaachia Wachagga Wenyewe Waindeleze Kilimanjaro Wao Wakibaki Kuwa Kama Wasimamizi Zaidi na Wachagga Kwa Kweli Walijitahidi Sana Kabla Ya Uhuru wa Tanganyika Walikuwa Wamefanikisha Mengi.
Baada Ya Hapo Wachagga Hawakuweza Tena Kuweka Focus Kuijenga Zaidi Kilimanjaro Kutokana na Mabadiliko Ya Serikali na Sera za Serikali Mpya Iliyokuja na Mfumo Uliopeleka Focus Kwenye Serikali Kuu na Utekelezaji wa Sera za Serikali Kuu na Kutoruhusu Mfumo wa Serikali za Majimbo.
Bustani Halisi Ya Eden Ambayo Bado Ina Mazingira Bora Sana Ya Asili Ambayo Sio Rahisi Kuyapata Eneo Lolote Duniani Imerudi Nyuma, Hata Hotel Zenye Hadhi Ya Nyota Tano Kwa Ajili Ya Watalii wa Kupanda Mlima Kilimanjaro Wenye Umaarufu Mkubwa Sana Duniani Ni Nadra Kuzipata.
Ni Jukumu Letu Wachagga Kwanza Tuwashukuru Babu Zetu wa Miaka Ya 1600 Kuweza Kusafiri Safari Nzito na Ndefu Sana Kuweza Kufika Eneo Lililobarikiwa Kiasi Hiki, Pia Tumshukuru Mungu Wetu Ruwa/Iruwa Kwa Kuwaongeza Vyema Babu Zetu Kufikia Eneo Hili Ambalo Amelitoa Kama Zawadi Kwetu Wachagga. Muhimu Zaidi Tuna Jukumu Zito La Kuifufua na Kuitimiza Ndoto Iliyokufa Mwaka 1961 Ya Kuifanya Bustani Hii Halisi Ya Edeni Kuwa Sehemu Bora Sana Ya Kuishi Kama Ilivyokuwa Inaazimiwa Tangu Karne Ya 19.
Urithi Wetu Wachagga
urithiwetuwachagga@gmail.com