HISTORIA FUPI YA CHUO CHA UALIMU MARANGU T. T. C

HISTORIA FUPI YA CHUO CHA UALIMU MARANGU T. T. C

Chuo Hiki Ni Taasisi Ya Elimu Iliyo Chini Ya Wizara Ya Elimu na Mafunzo Ya Ufundi Inayotoa Mafunzo Ya Ualimu Mpaka Ngazi Ya Diploma. Kwa Mazingira na Majengo Ni Chuo Chenye Hadhi Ya Juu Sana.

Chuo Hiki Kilianza Kama Seminari Ya Kwanza Kilimanjaro Mwaka 1902 Chini Ya Wamisionari wa Kanisa La Kilutheri, Katika Eneo La Kidia, Old Moshi Sio Kwa Lengo La Kutoa Mafunzo Ya Theolojia Bali Kutoa Mafunzo Ya Ualimu na Uinjilisti.

Seminari Ya Kidia Ilianza Kutoa Wachungaji Wasomi Bora Sana Wa Kilutheri Ambao Walipata Umaarufu Mkubwa Kama Wachungaji Wenye Elimu na Uwezo Mkubwa Katika Bara Zima La Afrika.

Mwaka 1912 Seminari Hii Ilitakiwa Kutanuka Zaidi na Eneo La Kidia Ilipokuwepo Lilionekana Kuwa Dogo Hivyo Ilihamishwa Kutoka Kidia, Old Moshi Kuhamishiwa Eneo La Marangu, Arisi Ilipo Mpaka Leo.

Seminari Hii Ya Marangu Iliendelea Kukua na Kutanuka Ikipata Umaarufu Mkubwa Ndani na Nje Ya Kilimanjaro Ikiendelea Kutoa Mafunzo Bora Sana Kwa Walimu, Wainjilisti na Wachungaji.

Miaka Ya 1970 Wakati Serikali Ya Tanzania Chini Ya Sera Ya Ujamaa Inafanya Utaifishaji wa Taasisi Zisizo za Kiserikali Ilitaifisha Chuo Hiki na Kukifanya Cha Serikali na Mpaka Leo Kimeendelea Kuwa Hivyo Kikitoa Mafunzo Ya Ualimu Kwa Ngazi Mbalimbali Mpaka Ngazi Ya Diploma.

Karibu kwa Maoni, Je Unadhani Chuo Cha Marangu Kinafaa Kupandishwa Hadhi Kuwa Chuo Kikuu?

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *