KIJIJI CHA KOMAKUNDI, MAMBA
– KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI
USHARIKA WA KOMAKUNDI.
– SHULE YA MSINGI KOMAKUNDI.
– KOMAKUNDI SHOPPING CENTRE AND BAR.
NOTE: Kitu Kilichonifurahisha Hapa KOMAKUNDI ni Uwepo wa Wale Wahunzi/Wafuavyuma wa Mamba wa Ukoo wa Ngowi, Makundi, Kimei, Nyella, Temu, Moshi, Koka n.k.,.
Kwa Kipindi cha Karibu Miaka 400 Mamba Imekuwa Ikisifika Kwa Uhodari wa Kutengeneza Vifaa vya Chuma Hasa Silaha Kali za Kivita Kwa Sehemu Kubwa Ya Historia Ya Wachagga na Walikuwa Wauzaji wa Silaha na Vifaa Vingine Kwa Watu Mbalimbali Wakiwemo Wamasai.
Tangu Miaka Ya 1700 Mpaka Leo 2020 Bado Wanaendelea na Kazi Hiyo na Nimekutana Nao na Kuzungumza Nao. Kinachosikitisha Tu Ni Kwamba Hawajaiendeleza Sana Teknolojia Hiyo Wala Kujenga Viwanda Vikubwa vya Kisasa Vya Kuwawezesha Kuzalisha Kwa Wingi na Kwa Viwango vya Juu ili Kujiletea Utajiri Mkubwa Licha Ya Kuifanya Kazi kwa Karibu Miaka 400.
Kwa Ujumla Wamenivutia Sana.
Urithi Wetu Wachagga
urithiwetuwachagga@gmail.com