ZIWA CHALLA, Katika Kijiji Cha Kidondoni, Kata Ya Challa, MAMSERA CHINI, ROMBO.
– Tafiti Zinaonyesha Kwamba Ziwa Hili Limekuwepo Kwa Takriban Miaka 250,000 Iliyopita Mpaka Sasa.
– Hili Ni Ziwa Ambalo Limetumbukia Kidogo Ndani Ya Ardhi na Lina Kina Cha Mita 170 Kutoka Usawa wa Ardhi na Ukubwa wa Eneo La Kilomita za Mraba 4.2
– Ziwa Hili Ambalo Liko Mashariki Ya Mlima Kilimanjaro Linapata Maji Yake Kutoka Ardhini, Katika Chemchem za Ardhi Ya Mlima Kilimanjaro.
– Ni Ziwa Lenye Samaki Aina Ya Tilapia na Lina Mamba Pia.
– Ni Eneo Zuri Sana Kutembelea Kwa Ajili Ya Kustarehe na Kula Bata Huku Ukitazama Muonekano wa Ziwa Hili, Ni Eneo Lenye Utulivu Mkubwa Linalotembelewa Sana na Watalii.