KIJIJI CHA WAZALENDO.
KIJIJI CHA KOMAKUNDI, MAMBA
– Katika Ziara Yote Tuliyofanya Kilimanjaro Hakuna Kijiji Ambacho Tumekuta Watu ni Wazalendo na Wanaojivunia Kijiji Chao Kama Watu wa Kijiji cha Komakundi, Mamba. Baadhi Ya Vijiji vya Rombo Pia Watu Wanajivunia Vijiji Vyao Lakini Sio Kama Komakundi.
– Kwanza Ndicho Kijiji Pekee Kilimanjaro Nzima Ambacho Kabla Hujaingia Unaanza Kukutana na Kibao cha Kukukaribisha Kimeandika “KARIBU KOMAKUNDI VILLAGE”, Ambayo Ni Ishara Kwamba Hiki Kijiji Kina Watu Wanaofikiri Kwa Utofauti.
– Watu Wengi wa Komakundi Tuliokutana Nao Wanazungumzia Kijiji Chao Kwa Mazuri na Kwa Namna Ya Kuonyesha Kwamba Wanajivunia Sana Komakundi. Hata Ukifuatilia Hapa Kwenye Ukurasa wa Facebook, Katika Vijiji Vyote Tulivyo-post Hakuna Post Ya Kijiji Iliyopata “Likes” na “Comments” Nyingi Kama Kijiji cha Komakundi.
– Mwanzoni Tulifikiri Labda Kijiji Kinachoongoza Kwa Watu Kuwa na Uzalendo Zaidi Kwa Kijiji Chao ni Kijiji Cha Nronga, Machame Lakini Tukaja Kugundua Nronga Bado Wapo Nyuma Sana Kwenye Suala Hili, Hakuna Hata Kijiji Kinachokaribia Komakundi kwa Uzalendo.
– Kijiji Cha Komakundi Pia Ni Kijiji Kilichoendelea Sana na Ndio Kijiji Maarufu kwa Kufua Vyuma Kilimanjaro.
– Zamani Wafua Vyuma Ambao Pia Ndio Walikuwa Watengenezaji Wakubwa wa Silaha za Kivita Walikuwa ni Watu Walioheshimika Sana Kilimanjaro Hata Nje Ya Kilimanjaro Kwani Wamasai Pia Walitegemea Kununua Silaha Zilizotengenezwa Uchaggani. Ambapo Kati Ya Watu Walioheshimika Kwa Kutengeneza Silaha ni Pamoja na Watu wa Ukoo wa Makundi wa Kijiji cha Komakundi, Mamba, Watu wa Ukoo wa Malisa wa Kijiji cha Kidia, Old Moshi, Watu wa Ukoo wa Chuwa wa Kijiji Cha Singa, Kibosho n.k.,
– Lakini Licha Ya Koo Hizi Zote Kupata Umashuhuri Mkubwa wa Utengenezaji Silaha za Kivita, Ambapo Watu wa Ukoo wa Makundi wa Komakundi, Mamba na Watu wa Ukoo wa Malisa wa Kidia, Old Moshi Walisifika Zaidi na Waliuza Sana Silaha Ndani na Nje Ya Kilimanjaro, ni Kijiji Hiki cha Komakundi Pekee Ndicho Kimeendeleza Utamaduni Huu Mpaka Sasa na Wanajivunia Sana Pia na Ukifika Lazima Wakupeleke Kwenye Kiwanda Ukakutane na Wataalamu Wao.
– Licha ya Kwamba Ukoo Mkubwa Zaidi Hapa Komakundi ni Ukoo wa Makundi Ambao Pia Ndio Umebeba Jina La Kijiji Lakini Pia Kuna Koo Nyingine Kubwa Kama Ngowi, Temu, Kimei, Mbuya, Chao, Nyella, Koka n.k.,
– Hongereni Komakundi, Wachagga Tunapaswa Kuiga Mfano wa Komakundi Linapokuja Suala La Uzalendo Nyumbani.
Nakaribisha Maoni.
Urithi Wetu Wachagga
urithiwetuwachagga@gmail.com