CHAGGA SPIRIT, “ARI YA WACHAGGA”

CHAGGA SPIRIT

Nyakati Zimekuwa Zikibadilika Uchaggani Tangu Karne Nyingi Zilizopita na Wachagga Wamekuwa na Tabia Tofauti Kutokana Kwa Nyakati Tofauti Kutokana na Matukio Fulani Yaliyotokea na Kubadilisha Hali Ya Kisiasa Kilimanjaro na Kuhama Kwa Nguvu za Kisiasa Kutoka Eneo Moja Kwenda Jingine na Hata Ushawishi wa Kisiasa Kutoka Himaya Moja Kwenda Nyingine.

Jinsi Hali Ya Mambo Ilivyokuwa Kilimanjaro Miaka Ya 1700, Ni Tofauti na Ilivyokuwa Miaka Ya 1800, Ambayo Pia Ni Tofauti na Miaka Ya 1900 na Hata Sasa Miaka Ya 2000. Yote Hiyo Ikitegemea na Sababu Mbalimbali.

Tabia Zimekuwa Zikibadilika na Hata Umaarufu wa Maeneo Pia Umekuwa Ukibadilika, Lakini Kwa Ni Tabia Ambazo Zinaweza Kwa Uchache Kabisa Kuchukua Nusu Karne Zinaenda Mpaka Karne Nzima Au Zaidi Mara Nyingi Haziwezi Kuonekana Kwa Mtazamo Rahisi Ni Mpaka Mtu Awe Mfuatiliaji Sana Wa Historia Ndio Anaweza Kuelewa Kwa Sababu Pia Zinakuwa Zimechangiwa na Matukio Fulani Ya Kihistoria Ambayo Yanakuwa Yamebadilisha Mwenendo wa Mambo.

Kuna Huyu Dada Muingereza Aliyeitwa Eva Stuart Watt Ambaye Aliishi Kilimanjaro Katika Eneo La Marangu Akitumikia Kama Mmisionari Katika Misheni Ya Ashira Karibu Miaka 100 Iliyopita Sasa.

Alikuwa na Haya Ya Kusema Juu Ya Makundi Mbalimbali Ya Wachagga Kwa Miaka Aliyoishi Kilimanjaro, Kwa Namna Walivyokuwa.

ALISEMA:

“Wachagga wa Marangu Wamechangamka na Wenye Ari Kubwa Sana.”

“Wachagga wa Old Moshi, Ndio Wenye Uthubutu Mkubwa Zaidi.”

“Wachagga wa Kibosho ni Kama Wana Majivuno Zaidi Pengine Kwa Sababu Ya Mafanikio Waliowahi Kuwa Nayo Miaka Ya Nyuma.”

Lakini Wale wa Mashariki Waliowahi Kupitia Manyanyaso Akimaanisha Wachagga wa Rombo ni Wanyenyekevu, Wakimya na Wasio na Imani na Watu Wengine na Pengine Ndani Ya Mioyo Yao Iliyoumizwa Wamehifadhi Kinyongo na Wanajiandaa Kuja Kulipa Kisasi Miaka Ijayo.

Japo Kwa Bahati Mbaya au Makusudi Kuna Maeneo Mengine Muhimu Aliyasahau Kama Machame, Uru, Siha na Baadhi Ya Maeneo Ya Vunjo Pengine Kwa Sababu Ya Umaarufu Wa Maeneo Hayo Kupungua Sana Mwishoni mwa Karne Ya 19 na Mwanzoni mwa Karne Ya 20.

Lakini Aliweza Kuongea Aliyoyaona Au Akachanganya na Kuhadithiwa Pia.

Hizi Sifa Zimekuwa Zikichukua Muda Mrefu Kubadilika Lakini Siku Zote Kumekuwepo na Sababu Japo Inaweza Isionekane Bila Kufuatilia Kwa Undani na Kwa Kina.

Hata Hivyo kwa Sababu Ya Mahusiano Mengi Ya Kindugu, Asili na Kuishi Kwa Karne Nyingi Kwenye Mifumo Ya Aina Moja Ya Tawala Zinazoingiliana Tabia Nyingi za Msingi Kwa Wachagga Zimekuwa Ni Zile Zile Kama Ilivyo Mila Desturi na Tamaduni.

Karibu Utoe Maoni Juu Ya Mtazamo wa Mwandishi, “Eva Stuart Watt”.

CHAGGA SPIRIT
ARI YA WACHAGGA

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *