KIJIJI KILICHOTIMIZA VIGEZO VINGI ZAIDI VYA KUWA NA MVUTO ZAIDI KILIMANJARO.

KIJIJI KILICHOTIMIZA VIGEZO VINGI ZAIDI VYA KUWA NA MVUTO ZAIDI KILIMANJARO.

KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.

– Imetuchukua Muda Mrefu Kufikia Hitimisho Hili Kwamba Katika Vijiji Vyote Tulivyotembelea Uchaggani, Kilimanjaro Ni Kijiji Gani Tunaweza Kukitaja Kwamba Kimeweza Kuwa na Uwiano Mzuri Zaidi wa Kufikia Vigezo Tulivyoweka.

– Kama Mnavyojua na Mlivyoweza Kujionea Hapa Pia Vijiji vya Uchaggani, Kilimanjaro Vimekamilika Sana Kila Idara Kuanzia Mvuto wa Asili, Maendeleo Ya Watu, Maendeleo Ya Vitu, Ustaarabu wa Watu, Miundombinu n.k.,

Tumeweza Kuwa na Vijiji Zaidi Ya 20 Ambavyo Karibu Vyote Vinaonekana Kulingana Kwenye Namba Moja, Huku Vikiziadana Vitu Vidogo Vidogo Sana. Lakini Mwisho wa Siku Hata Ukienda Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani Utakutana na Mwanafunzi Anayefanya Vizuri Zaidi Kwa Ujumla Licha Ya Kwamba Wote Waliodahiliwa Wana Uwezo Mkubwa Sana.

– Vigezo Vilikuwa ni

1. Mazingira Bora Ya Asili.

2. Miundombinu Bora.

3. Taasisi Zilizopo.

4. Hadhi Ya Makazi kwa Ujumla.

5. Ustaarabu wa Watu.

6. Ubora wa Huduma za Kijamii.

7. Hali Ya Kijiografia.

Vijiji Vingi Vinafikia Vigezo Hivi, Kama Mlivyoweza Kujionea Wenyewe Kwenye Ziara Tuliyofanya, Lakini Tumefikia Hitimisho Kwamba “Arisi”, Ndio Imekuwa “The Most Impressive”, Japo Kwa Shida sana na Pengine Mtu Mwingine Anaweza Kuja na Pendekezo Tofauti Kwa Vigezo Hivyo Hivyo.

Hata Hivyo Naweza Kusema Kwa “Arisi” na Vijiji Jirani, Vinafaidika Zaidi na Mazingira Ya Asili Ambapo Ni Maeneo Yenye Maji Mengi Sana na Ardhi Yenye Rutuba Sana. Pia Kuna Baadhi Ya Vigezo “Arisi” Imezidiwa na Vijiji Vingine Kama Vile “Arisi” Kuwa na Mwinuko Mkali Wakati Vijiji Kama Foo, Lyamrakana, Mweka, Nronga Viko Tambarare Zaidi.

Nachoweza Kusema Wachagga Japo Kwenye Suala La Kujali Mazingira Tunajitahidi Lakini Bado Tunahitaji Kuongeza Bidii Zaidi Eneo Hili, Hasa Watu wa Ukanda wa Chini.

Bado Tuna Nafasi Ya Kuboresha Zaidi Mazingira na Kuifanya Kilimanjaro Kuwa Ya Kijani Zaidi Hasa Ukanda Ambapo Maeneo Hayo Yanahitaji Kupanda Miti Zaidi na Kuitunza Mpaka Ikomae Kabisa, Hiyo Itapelekea Napo Patakuwa Bora Zaidi Kimakazi Kuliko Hata Ukanda wa Juu Ambao Ni Kijani Zaidi.

Karibuni Kwa Maoni au Mapendekezo Mbadala.

KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.
KIJIJI CHA ARISI, MARANGU.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *