MOSHI – MJI MKONGWE ZAIDI KASKAZINI YA TANZANIA.

MOSHI – MJI MKONGWE ZAIDI KASKAZINI YA TANZANIA.

– Moshi Sio Tu Kwamba Ndio Mji Mkongwe Zaidi na Mji Mama Kaskazini Ya Tanzania, Bali Pia Ndio Ulikuwa Mji wa Utawala Kaskazini Ya Tanzania Kuanzia Mwishoni mwa Karne Ya 19 na Mwanzoni Mwa Karne Ya 20.

– Kilimanjaro Ikiwa Ndio Eneo Maarufu Zaidi Tanganyika Kutokea Pwani, Huku Mangi Rindi Mandara na Sultan wa Zanzibar Wakiwa Watawala Mashuhuri Zaidi Ulaya Karne Ya 19, Taasisi Nyingi za Mwanzoni za Kiserikali na Kidini Kaskazini Ya Tanganyika Zilianzia Moshi – Kilimanjaro.

– Mji wa Moshi Wenyewe Ambao Ulianzia Old Moshi na Baadaye Karne Ya 20 Kuteremka Moshi Mjini Ulikuwa Ndio Mji Mama Kaskazini Ya Tanganyika Ambapo Ndio Ulikuwa Ofisi za Utawala kwa Eneo Lililoitwa Wakati Huo “Wider Kilimanjaro” Lililokuwa Linaanzia Usambara Mpaka Arusha Ambapo Arusha Yenyewe Inataliwa Kutokea Moshi.

– Hata Mwaka 1899 Wachagga Walipoungana Pamoja na Kwenda Kuvamia Wamasai Arusha Kuwakomboa Baadhi Ya Ndugu Zao Waliokuwa Wamechukuliwa Mateka Umasaini, Sambamba na Kupora Mali Nyingi za Wamasai, Mji wa Arusha Ulikuwa Bado Haujaanza, Wakati Mji wa Moshi Ulishaanza Wakati Huo Ukiwa Old Moshi na Arusha Ilikuwa Ikitawaliwa Kutokea Moshi.

– Hata Taasisi za Dini Ya Kikristo Zilianzishwa Kilimanjaro Kwanza kabla Ya Kwenda Maeneo Mengine, Kwa Mfano Misheni Ya Kilutheri Ilianza Kufungua Vituo Sita vya Misheni Ya Kilutheri Kilimanjaro vya Nkwarungo, Machame, Ashira, Kidia, Siha, Masama na Mwika Kabla Ya Kwenda Kufungua Misheni Arusha. Ni Zaidi Ya Miaka 15 Baadaye Ndipo Misheni za Ilboru na Nkoaranga Zilianzishwa Arusha Zikiwa Kama Matawi Ya Misheni Ya Kilutheri Kilimanjaro. Hata Misheni Ya Kanisa Katoliki Baada Ya Zanzibar na Bagamoyo Moja kwa Moja Walienda Kijiimarisha Kilimanjaro Haraka Kabla Hawajazidiwa na Waprotestanti Kabla Hawajafikiria Maeneo Mengine.

– Hivyo Mji wa Moshi Ulianza Kukua Mapema na Taasisi Nyingi Zilianza Kuimarika Kilimanjaro na Kuzidi Kuuongezea Umuhimu Mji wa Moshi.

SWALI NI JE, NINI KIMESABABISHA MJI WA MOSHI KURUDI NYUMA NA KUPOTEZA UMUHIMU NA UMASHUHURI WAKE KASKAZINI YA TANGANYIKA NA TANZANIA KWA UJUMLA?

– Mpaka Kufikia Miaka Ya 1960’s, Pengine Mpaka Mwanzoni mwa 1970’s Moshi Ilikuwa Bado Ni Mji Mkubwa Sawa au Zaidi Ya Arusha na Ukiwa na Taasisi Nyingi za Kitaaluma Ambapo Kilimanjaro Ilikuwa na Shule Nyingi Sana za Sekondari na Msingi Kuliko Sehemu Yoyote Tanzania, na Huku Ikiwa na Chuo cha Kwanza cha Elimu Ya Juu Tanzania Kilichojengwa na Wachagga Wenyewe, Chuo cha Ushirika Moshi. Vyote Hivi Vikiichangamsha na Kuipa Umuhimu Mkubwa Kilimanjaro na Mji wa Moshi kwa Ujumla.

– Kuna Nadharia Kwamba Moshi Imerudi Nyuma na Kuzidiwa na Arusha Ambayo Iliitangulia Mwanzoni kwa Sababu Wachagga ni Wagumu Kuuza Ardhi Sababu Ya Mila Zao Juu Ya Suala La Ardhi Ndio Maana Mji Hautanuki, Lakini Hoja Hii Nafikiri Haina Uhalisia Sana kwa Maeneo Ya Tambarare Uliopo Mji wa Moshi Ambapo Ndipo Unatanukia Zaidi.

– Hoja Nyingine ni Watu Kusema Hali Ya Hewa Ya Moshi Mjini Haivutii Kama Arusha Ambayo Iko Karibu Zaidi na Mlima Meru Kuliko Jinsi Moshi Mjini Ilivyo Karibu na Mlima Kilimanjaro, Hivyo Asili Ya Eneo Ya Hali Ya Hewa Kimazingira Imechangia.- Hoja Nyingine ni Wenyeji Wenyewe Wachagga Kutokuwa na Utayari wa Kuendeleza Mji Wao na Kwenda Kuendeleza Miji Mengine, Japo Hoja Hii Iko Kinyume Kidogo na Kanuni za Kiuchumi.

– Hoja Nyingine Ni Kwamba Kudumazwa kwa Kilimanjaro Baada Ya Uhuru kwa Sera Kwamba Kilimanjaro Imeshaendelea Inatakiwa Kusubiri Mikoa Mingine Iendelee Ili Kuleta Usawa. Kwa Mujibu wa Abisai Temba, Hii Ilikuwa ni Sera Ya Awamu Ya Kwanza Ya Nyerere Ambapo Miradi Ya Maendeleo Ilipelekwa Zaidi Mikoa Mingine Kwa Kigezo kwamba Kilimanjaro Inatakiwa Kusubiri kwa Sababu Imeshaendelea, Hata Kama Inalipa Kodi, Sera Ya Serikali Ambayo Iliidhoofisha Kilimanjaro na Kuchangia Kudumaza Mji wa Moshi.

– Hoja Nyingine ni Kuuawa kwa Chama cha Ushirika cha KNCU kwa Sera za Serikali Ya Awamu Ya Kwanza. Kwa Mujibu wa Reginald Mengi Chama cha Ushirika cha KNCU Kiliuawa kwa Sera za Serikali Ya Awamu Ya Kwanza Chini Ya Nyerere Ili Kutekeleza Sera za Ujamaa au Ni Nyerere Mwenyewe Kuogopa Nguvu za Kisiasa za Ushirika Hivyo Kuamua Kuviua Kwa Maslahi Yake Kisiasa.

– Kwa Mujibu wa Abisai Temba, Uchumi wa Kilimanjaro Kupitia KNCU Ulikuwa Mkubwa Sana na Ulikuwa Unaendelea Kukua Kwa Kasi Sana Kiasi Kwamba Serikali Ya Tanganyika Chini Ya Waingereza Ilikuwa Inategemea Kiasi Kikubwa cha Mapato Kutoka Kilimanjaro Kwa Ajili Ya Kuendesha Serikali, na Hata Kilimanjaro Yenyewe Ilikuwa Ikitajirika Sana, Hivyo Kuuawa kwa Vyama vya Ushirika Kumepeleka Umaskini Kilimanjaro na Kuidhoofisha na Hata Kuudumaza Mji wa Moshi Huku Kukiwa Hakuna Mbadala Mwingine wa Haraka Kiuchumi.

– Kuna Sababu Nyingine Zaidi Zinazosemwa Ambazo Zimechanganya Ukweli na Nadharia.

Kwa Wenye Uzoefu na Wenye Umri Mkubwa Kidogo Tusaidiane Unafikiri ni Nini Kimesababisha Mji wa Moshi Kurudi Nyuma Kiasi cha Kuzidiwa Maendeleo na Arusha Ambayo Moshi ni Mzazi Wake, Wakati Katika Hali Ya Kawaida Moshi Ilitakiwa Kuwa Mbele Zaidi?

Karibu kwa Maoni.

MJI WA MOSHI KARNE YA 21
MJI WA MOSHI KARNE YA 21
MJI WA ARUSHA MWAKA 2020
JIJI LA ARUSHA MWAKA 2020

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

6 Comments

 1. Kama Serikali za Awamu zote wanadhani Kilimanjaro Imeendelea Kwa Vigezo vyao Sisi Wana Kilimanjaro tunaona Maendeleo yetu ni bado Sana kutokana na Historia yetu.
  Inabidi Sisi wenyewe tufanye jitihada zetu wenyewe kuufanya Mikoa wetu uingie kwenye Ramani kwenye nchi yetu Tanzania pamoja na nje ya nje.
  Ni vigumu Kuzuia Maendeleo ya Watu Kwa Vigezo dhaifu,.
  Kwa hiyo ni kuwa pamoja kuona Jambo la kufanya tuweze kujiletea Maendeleo yetu kutokana Tamaduni zetu ambazo zilitufikisha hapa tulipo.

  1. Ni kweli kabisa. Inabidi tuamke, tuchangamke.

 2. Hoja kuwa awamu ya Kwanza ya utawala ilifanya Moshi kubaki nyuma ni ya kweli
  Nyerere alituma Sera ya ujamaa kuchota utajiri wa Moshi kwenda kuendeleza maeneo mengine ya nchi
  Simlaumu ndie amejenga Taifa moja na watu wa Moshi tunaona faida ya umoja wa kitaifa

  1. Nyuma yake kulikuwa na hila nyingi. Suala la kujenga Taifa moja sio hoja ya msingi sana kwani mataifa yote ya Afrika ni matokeo ya kazi iliyofanywa na wazungu kutoka Ulaya kugawa makoloni na nchi zote ambazo yalikuwa makoloni yote yamekuwa taifa moja. Ni jambo ambalo limefanyika Afrika nzima baada ya wazungu kuondoka hivyo sio jambo la ajabu au la tofuati sana. Hakuna koloni ambalo halijawa taifa.

 3. Ni muhumu sana kwa Jamii ya Wachagga kuamka. Na elimu itolewa kwa Vijana na Watoto wakichaga. Wafahamu historia yao nzuri. Na wafahamishwa Siasa zilizopo sasa thidi ya wachagga. Na namna yakupambana nazo. Muhimu pia waamasishwe kupapenda nyumbani.hata kama wamezaliwa mikoani. Lakini watambue wapo safarini na Kilimanjaro ndo Nyumbani.

  1. Sahihi kabisa Mr. Kimaro.

   Karibu sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *