UMUHIMU WA KUFAHAMU HISTORIA.

B. H. Liddell Hart, Aliyekuwa Mwanajeshi Katika Jeshi La Uingereza Aliyeshiriki Katika Vita Ya Kwanza Ya Dunia 1914 – 1918 na Vita Ya Pili Ya Dunia 1939 – 1945 Ameandika Kitabu Kilichopata Umaarufu Kama (Why Don’t We Learn From History?), Akimaanisha, (Kwa Nini Hatujifunzi Kutoka Kwenye Historia?)

Liddell Hart Anasema Tofauti na Wengi Wanavyochukulia Kufahamu Historia Ni Muhimu Sana, na Jamii Ya Watu Wanaofahamu Historia Wana “Advantage” Kubwa Ukilinganisha na Jamii Isiyofahamu Historia.

– Historia Kwanza Huwa Inasisimua Akili na Kuburudisha, Japo Mara Nyingine Huwa na Ukweli Ambao Unaumiza Lakini Huwaweka Watu Huru Zaidi.

– Pili Manufaa Ya Kufahamu Historia Ni Ya Muda Mrefu na Yanaweza Kuleta Hamasa Ya Mabadiliko Ambayo Hayakutegemewa.

– Historia Inatusaidia Kujiepusha na Kurudia Makosa Ambayo Yalishafanyika Huko Nyuma. Hata Mambo Mengi Ya Hovyo Yanayofanyika Kwenye Siasa Ni Kwa Sababu Watu Hawataki Kujifunza Historia. Makosa Mengi Yanayofanyika Ni Marudio Ya Makosa Ambayo Tayari Yalishafanyika Huko Miaka Ya Nyuma.

– Historia Inasaidia Watu Kuwa na Hekima Zaidi. – Historia Ina Manufaa Kwa Mtu Mmoja Kwa Sababu Inasaidia Sana Katika Kujijengea Falsafa Binafsi, Kwa Jamii na Kwa Taifa Kwa Ujumla.

– Kupitia Historia Tunaweza Kuwa na Maisha Bora.

– Historia Inasaidia Sana Kuleta Matumaini Wakati Tunapita Kwenye Changamoto Ngumu Kwa Kujaribu Kulinganisha Tunachopitia na Kile Ambacho Historia Inatuambia.

– Kupitia Historia Tunajifunza Kutoka Kwenye Uzoefu wa Watu Wengine na Hivyo Kujua Ni Kipi Cha Kuepuka na Kwa Wakati Gani.

– Historia Ni Kwa Ajili Ya Kila Mtu na Sio Tu Kwa Ajili Ya Taasisi na Serikali.

Tunapaswa Kuendelea Kujifunza na Kujikumbusha Historia, Hatutabaki Kama Tulivyo.

Urithi Wetu Wachagga

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *