ELIMU YA ASILI YA WACHAGGA.

– Kwanza kabla ya kuingia kwenye mada yetu ya elimu ya asili tujiulize elimu ni nini na chimbuko lake. – Elimu ni ule mchakato wa kupokea mkusanyiko wa taarifa na maarifa yaliyotokana na uzoefu wa watu katika maeneo mbalimbali yakakusanywa kwa kipindi kirefu na kuendelea kurithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Maarifa haya pia yanaweza …

MAADILI YA JUU ZAIDI KWA WACHAGGA (THE HIGHEST VIRTUE) ILIKUWA NI UJASIRI(BRAVERY).

– Kila jamii au kila nchi duniani kuna thamani inayowekwa kwenye matendo ambayo yamepewa ukuu na utakatifu zaidi kuliko mengine na yanahesabika kuwa ndio matendo mema zaidi(virtues) na kinyume chake ni matendo maovu na ya hovyo(vices). – Hivyo watu wengi wa jamii husika hupenda kuhusishwa na matendo hayo ili kujenga ushawishi zaidi na hivyo matendo …

BARABARA YA KILEMA.

– Moja kati ya jukumu kubwa sana na muhimu kabisa tulilonalo ni kufundisha historia kwa kizazi kinachokua kisha iendelee kurithishwa kwa vizazi vinavyofuata ili waweze kujua umuhimu wa vitu na watu mbalimbali kadiri ya michango yao kwenye jamii husika. Lakini kwa bahati mbaya sana kwa upande wa wachagga historia ilififia zamani sana ukilinganisha na hapo …

TAASISI YA UMANGI.

KAZI ZAKE, UMUHIMU WAKE NA MABADILIKO YAKE. – Kila kitu duniani kinachohusiana na watu au kuathiri maisha ya watu wa jamii kwa namna moja au nyingine huwa kinatoka kwenye asili ya binadamu. Mifumo ya kijamii kwa ujumla wake hutoka kwenye asili ya binadamu ikilenga kutatua changamoto fulani au kuboresha maisha ya watu wa jamii hiyo …

TEKNOLOJIA YA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI KATIKA NCHI YA WACHAGGA.

– Jamii Yoyote Ili Iweze Kupiga Hatua Kubwa Kimaendeleo Katika Nyanja Zake Zote Inapaswa Kuwekeza Sana Kwenye Maendeleo Ya Kiteknolojia. Na Jamii Yoyote Inayoweka Juhudi Kubwa Kwenye Kuhimiza Kuchochea na Kukuza Teknolojia Zake Katika Nyanja Mbalimbali Huweza Kukua Haraka Kwani Inarahisisha Sana Mifumo Yake Ya Kiuchumi Katika Utengenezaji wa Thamani Ambao Kimsingi Ndio Utajiri wa …