KWA NINI NI MUHIMU KURUDISHA UTUKUFU ULIOPOTEA?

Katika Uhalisia Unapokuwa Unaishi Kwenye Jamii Yoyote Aidha Kwa Kujua Au Kutokujua Lazima Kuna Falsafa Fulani Unaiishi. Inaweza Kuwa ni Falsafa Moja au Mseto Fulani Ambayo Ndio Imebebea Maadili Yanayokubalika na Jamii Husika. Maadili Hayo Yanayokubalika Huwa na Nguvu Kubwa Sana Kwa Mtu Yeyote Anayeishi Kwenye Jamii Hiyo Ambapo Sio Rahisi Kwenda Kinyume Nayo Kwani Kwa Kufanya Hivyo Atakuwa ni Sawa na Anatenda Dhambi. Lakini Hata Kama Ataenda Kinyume Nayo Aidha Atafanya Kwa Kificho au Angalau Hawezi Kujivunia Alichofanya.

Kwa Mfano Kama Umekulia Kwenye Jamii Ambayo Inaamini Kufanya Biashara ni Kitu Kibaya na Hakiendani na Maadili Ya Jamii Husika Basi Sio Rahisi Kuwa na Ujasiri wa Kuwaambia Watu Kwamba Unafanya Biashara. Au Umekulia Kwenye Jamii Ambayo Inaamini Kwamba Kuoa Mke Mmoja ni Udhaifu na Dalili za Umaskini na Kuoa Wake Wengi ni Ushujaa Mkubwa na Ishara Kwamba Wewe ni Tajiri, Basi Utaona Aibu Kuwaambia Watu Kwamba Una Mke Mmoja. Lakini Kinyume Chake Kama Umekulia Kwenye Jamii Ya Wakristo Inayoamini Kwamba Kuoa Mke Mmoja Ndio Maadili Basi Huwezi Kuthubutu Kujitangaza Kwamba Una Wake Wawili. Hiyo Ndio Mifano Ya Maadili Ya Jamii, na Hili Linakwenda Kwenye Kila Kitu Katika Maisha.

Hata Hivyo Mwanafalsafa Mashuhuri Sana wa Karne Ya 19, Mjerumani Friedrich Nietzsche(1844 – 1900), Akiwa ni Moja Kati Ya Wanafalsafa Waliokuja Kukubali Sana Duniani Baaadaye Alikuwa Mkosoaji Mkubwa Sana wa Suala Zima La Maadili Ya Jamii(Social Morality). Friedrich Nietzsche Anasema Maadili Ya Jamii Mambo Yaliyotengenezwa na Kuaminishwa Kwa Watu wa Jamii Hiyo Tangu Mtu Anapozaliwa Anayakuta Lakini Mara Nyingi Haya Faida Kwa Mtu Mmoja Mmoja Wala Kwa Jamii Nzima Bali Yanaweza Kuwa Yalikuwa na Lengo Fulani Lenye Maslahi Kwa Mtu au Kikundi Cha Watu Fulani Ambao Walitumia Nafasi Yao Kijamii Kuyafanya Kuwa Ndio Maadili Ya Jamii Hiyo.

Au Wakati Mwingine Maadili Ya Jamii Yanaweza Kuwa Yametokana na Maoni Ya Watu Wengi wa Jamii Hiyo Ambayo Yalitumiwa na Watu Waliotaka Kujenga Ushawishi na Kupata Nguvu Kwenye Jamii Husika Ili Kufanikisha Malengo Hayo. Kwa Mfano Labda Watu Wengi wa Jamii Husika ni Watu Maskini Hivyo Hawawezi Kumudu Gharama za Kujenga Nyumba, Anaweza Kutokea Mtu Akaja na Sera Kwamba Kujenga Nyumba Sio Jambo La Kimaadili Bali ni Ubinafsi na Uchoyo na Kwamba Maadili ni Watu Kukaa Kwenye Nyumba za Pamoja za Kupanga Ili Kushirikiana na Kusaidiana. Sera Hizo Zinaweza Kuungwa Mkono na Watu Wengi Waliokata Tamaa Ya Kujenga Nyumba na Kisha Kukubalika Kuwa Ndio Maadili Ya Jamii Hiyo. Hivyo Watu Wachache Waliojenga Nyumba Wataanza Kujisikia Aibu Kwamba Wanaishi Kwenye Nyumba Zao na Hilo Litawakatisha Watu Wengi Tamaa Kujenga Nyumba Zao na Badala Yake Kujivunia Kwamba Wamepangisha Nyumba.

Na Hii Ndio Maana Friedrich Nietzsche Anakosoa Sana Maadili Ya Jamii. Friedrich Nietzsche Anaamini Kwamba Maadili Ya Jamii Yamekuwa Kikwazo Kwa Watu Wengi Kufikia Malengo Yao Au Kufanya Makubwa Kwenye Maisha. Kwa Mfano Mtu Anaweza Kuwa Anauonea Aibu Utajiri na Kujivunia Umaskini Kwa Sababu Tu Maadili Ya Jamii Kwa Sehemu Kubwa Yanawachukulia Matajiri Kama Watu Wabaya, Licha Ya Kwamba Umasikini ni Mateso Lakini bado Mtu Anaweza Kujivunia Kwa Sababu Tu Unakubalika na Maadili Ya Jamii Husika. Sisi Sote ni Mashahidi Jinsi Baadhi Ya Wanasiasa Hujivunia Wao ni Maskini, Japo Mara Nyingi ni Wanafki Lakini Inawasaidia Kupata Wafuasi Kwa Sababu Umaskini Uliwahi Kutengenezewa Utakatifu Ndani Ya Jamii Hiyo, Pamoja na Sifa na Falsafa Mbalimbali za Kuutukuza. Friedrich Nietzsche Anaamini Kwamba Mtu Anatakiwa Kujitoa Kwenye Kufungwa na Maadili Ya Jamii Aliyopo na Kuwa Huru Kuishi Kwa Namna Yake na Kufanikisha Mambo Makubwa Kwenye Maisha Yake, Hii ni Kwa Sababu Kuna Maadili Ya Jamii Yake Yanaweza Kuwa Kikwazo Kwake Kupiga Hatua Lakini Hayana Maana Yoyote Hivyo Anapaswa Kuyapuuza.

Mpaka Hapo Tunaweza Kuona Kwamba Maadili Ya Jamii Sio Kitu Muhimu Sana Au Cha Kuzingatia Sana Ikiwa Hujayachunguza Undani Wake Kujiridhisha Lengo na Umuhimu Wake. Kuna Sehemu Kubwa Ya Maadili Yanapotosha na Kuiumiza Jamii Husika Bila Watu Wenyewe Kujua. Lakini Bado Hiyo Haipunguzi Nguvu Ya Matendo Ya Maadili Hayo Kwa Watu wa Jamii Husika. Watu Wengi Bado Wataogopa Sana na Kujiona Wanatenda Dhambi Kwa Kwenda Kinyume na Maadili Ya Jamii Yao Japo Kiuhalisia Wanafanya Jambo Sahihi Sana Kwa Maendeleo Yao.

SASA TURUDI KWENYE MADA, JE KURUDISHA UTUKUFU ULIOPOTEA NI JAMBO MUHIMU NA LA MAANA?

Kwanza Tuangalie Faida za Huo Utukufu;

Utukufu Binafsi Sambamba na Utukufu wa Kundi La Kijamii Unalotokea Huwa Unaleta Hali Ya Kujikubali na Kuongeza Kujiamini Binafsi Maarufu Kama (Self Esteem). Hii “Self Esteem” Imekuwa ni Sifa Muhimu Ya Watu Kufanikiwa Kwani Inamletea Mtu Ari na Shauku Ya Kufanikisha Mambo na Kupiga Hatua Kubwa Kimaendeleo. Hii Ndio Sababu Pia Huwa Inachukua Muda Mrefu au Vizazi Kahdaa Kwa Familia Tajiri Kurudi Nyuma Mpaka Kurudi Kwenye Umaskini Kabisa na Inachukua Muda Mrefu Mtu Kutoka Kwenye Umaskini Kabisa Kupanda Mpaka Kufikia Utajiri Mkubwa. Hivyo Hali Ya Kwamba Wewe au Jamii Uliyotoka ni Ya Watu Wakuu na Watu Wengine Kuwaona Kwamba Nyie ni Watu Wakuu Huongeza Sana Hamasa na Nguvu Ya Kuweka Bidii Katika Kufanikisha Mambo Makubwa. Hivyo Kuna Faida Kubwa Kwetu Binafsi na Kwa Vizazi Vinavyofuata Kwa Sisi Kurudisha Utukufu Uliopotea.

Lakini Kuna Watu Wanaamini Kwamba Kuhimiza Utukufu wa Kijamii na Utukufu Binafsi ni Majivuno(Egoism) na Majivuno Yanaoekana ni Sifa Isiyofaa au Uovu. Je Hali Ya Kutaka Kujiimarisha na Kurudisha Utukufu Uliopotea na Kuonekana ni Majivuno(Egoism) ni Uovu?

Mwanafalsafa Maarufu wa Karne Ya 20 Aliyejulikana Kwa Jina La Ayn Rand(1905 – 1982) Alipata Umaarufu Mkubwa Katika Kuandika Riwaya za Kifalsafa na Riwaya Zake Mbili Kupata Umaarufu Mkubwa (Fountainhead 1943) na (Atlas Shrugged 1957). Ayn Rand Katika Kusimamia Falsafa Yake Inayoamini Katika Ushujaa wa Mtu Binfasi Kwa Manufaa Ya Furaha Yake Binafsi Ambayo Jumla Yake Ndio Mafanikio Ya Kijamii, Anaamini Kwamba Majivuno(Egoism) Yasiyodhuru Wengine Ni Sifa Muhimu Kwa Mafanikio Ya Mtu au Watu. Hii ni Kwa Sababu Hiyo (Ego) Ndio Inayomsukuma Mtu Kupambana Sana na Kufanya Makubwa na Ina Mahusiano Ya Karibu Sana na Kile Anachokifanikisha.

Hata Hivyo Tunaishi Kwenye Jamii Ambayo Maadili Yaliyotengenezwa Yalihimiza Zaidi Ufanano wa Makundi Ya Watu(Uniformity) na Kuonekana ni Kama Yanakosoa Utofauti(Diversity). Hali Hiyo Iliyotengeneza Maadili Yaliyolenga Kuua Huo Utofauti(Diversity) Imewaingia Sana Watu Kiasi Kwamba Kuna Watu Wanahisi Ukakasi Pale Unapohimiza Utofauti(Diversity). Hivyo Unavyohimiza Utofauti (Diversity) Unaweza Kuonekana Sio Mtu Mzuri na Kuhisiwa Kwamba Unachofanya Sio Kitu Sahihi Kwa Sababu Ya Nguvu Ya Zile Propaganda Zilizotumika Kujengea Watu Mitazamo Ya Kuamini Katika Maadili Ya Ufanano wa Makundi Ya Kijamii na Kuua Kabisa Ule Utofauti Bila Kujali Madhara Yake. Na Hiyo ni Kwa Sababu Pia Kuna Watu Waliopewa Nafasi Ya Juu Zaidi Ya Kimaadili Katika Propaganda Hizo (Highest Moral Position) Ambapo Wamepewa Kama Utakatifu Fulani Wanaotumika Kuhimiza Maadili Hayo Kwa Jamii. Utasikia “Fulani Alikataa Hili”. Utajiuliza Huyo Fulani ni Nani Kwani? Utakuta Huyo Fulani ni Mtu Ambaye Propaganda Ilitumika Kumpa Nafasi Ya Juu Zaidi Ya Kumaadili na Hata Utakatifu Fulani Kwamba Ndiye Awe Hakimu wa Maadili Ya Jamii Husika.

Sasa Hapo Ndipo Tunaporudi Kwa Mwanafalsafa Friedrich Nietzsche Kwamba Sehemu Ya Maadili Inayoaminiwa na Jamii Ililetwa Kwa Manufaa Ya Watu Fulani Lakini Hayana Maana Yoyote Zaidi Ya Kuwa Kikwazo Kwa Maendeleo Licha Ya Kuambatanishwa Pia Na Hofu za Aina Mbalimbali. Kumbe Sehemu Ya Maadili Hayo Yalibebwa na Agenda Binafsi za Mhusika na Wakati Yalisukumwa na Chuki Pia Dhidi Ya Makundi Mbalimbali.

Na Ndio Maana Kuna Itikadi za Kisiasa Zilizopewa Uzito Mkubwa Tukaziamini na Kuziishi Lakini Zikaishia Kutuingiza Kwenye Umaskini Mkubwa na Hata Mpaka Leo Sehemu Ya Mizizi Yake Bado ni Kikwazo Kwa Maendeleo Yetu Kwani Jamii Bado Haijaondokana na Fikra Hizo Potofu Moja Kwa Moja. Hivyo Sasa Hakuna Kikubwa Unachoweza Kufanya Kwa Maadili Potofu Yaliyoko Kwenye Jamii Zaidi Ya Kuyapuuza.

Kwa Maana Hiyo Sasa Tuna Kila Sababu Ya kurudisha Utukufu Uliopotea Bila Kujiwekea Hatia Ya Aina Yoyote Moyoni Ya Kwamba Tunakwenda Kinyume na Maadili Ya Aina Yoyote. Kwa Sababu Tutakuwa Tunajihujumu Wenyewe Kwa Kujiwekea Hatia Kwa Kutumia Maadili Yaliyotengenezwa Kwa Lengo La Kutudhoofisha. Tuna Kila Sababu Ya Kupuuza Maadili Hayo.

Hivyo Basi Tuendelee Kununua Kitabu Ili Kujenga Mtazamo Chanya na Sahihi Katika Kurudisha Utukufu Uliodidimizwa Kwetu na Zaidi Kwa Watoto Wetu Katika Kuwajengea Kujiamini Kuelekea Kufanya Mambo Makubwa Kwenye Maisha Yao na Vizazi Vinavyofuata. Ndio Maana Hata Mangi Petro Itosi Marealle Anatuambia Mambo Makubwa na Makuu Yanatarajiwa Kutoka Kwetu, Hatupaswi Kumwangusha.

Karibu Kwa Maoni.

Karibu Kwa Kitabu.

Whatsapp No. +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *