Kwenye Kitabu cha “A History of Western Philosophy” Kilichoandikwa na Mwanafalsafa Mashuhuri Muingereza wa Karne Ya 20 Bertrand Rusell, Anaeleza Kwamba Maendeleo Ya Zamani Ya Ugiriki/Uyunani Ya Kale(Ancient Greece) Yalitokana na Ushawishi wa Himaya ya Misri Ya Kale (Ancient Egypt).
Lakini Pia Inafahamika Kwamba Maendeleo Ya Uyunani/Ugiriki Ya Kale(Ancient Greece Civilisation) Ndio Chanzo na Msingi wa Maendeleo Ya Ulaya Ya Leo Hii. Ujanja Wote Ambao Wanao Wazungu wa Ulaya Ambao Waliueneza Maeneo Mbalimbali Duniani Chanzo Chake ni Fikra na Mifumo Ambayo Ilianzia Uyunani/Ugiriki Ya Kale.
Mwanafalsafa Bertrand Russell Anaeleza Kwamba Ugiriki Ya Kale Iliendeleza Mawazo Mengi Yaliyoifanya Kupiga Hatua Kubwa Kutoka Kwenye Himaya Ya Misri Ya Kale, Kisha Baadaye Rumi Ya Kale Ikaendeleza Mawazo Mengi Kutoka Ugiriki Yale Kale na Hata Kuiangusha na Kuitawala.
Hii Ndio Sababu Inaaminika Kwamba Ustaarabu Ulianzia Afrika. Kuna Mpaka Minara Mikubwa Ya Kumbukumbu Maarufu Kama “Obelisk” Ambayo Iling’olewa Huko Misri na Kusafirishwa Kwenda Kuchimba Roma Wakati Huo Dola Ya Rumi Ikiwa Ndio Yenye Nguvu Duniani. Hapo ni Ukiachana na Zile Piramidi Kubwa Sana za Maajabu Misri Ambazo Isingewezekana Kuzing’oa na Kuzipeleka Rumi.
Hata Wanahistoria Mashuhuri wa Ugiriki Ya Kale Kama Vile Herodotus na Thucydides Wameandika Mambo Makubwa Sana Yaliyofanywa na Misri Ya Kale Ambayo Mengi Hata Ugiriki Ya Kale Hawakuwahi Kuyafikia. Pia Wameeleza Utukufu Mkubwa Sana na Umashuhuri wa Misri Ya Kale Ambao Kwa Mujibu wa Mwanafalsafa Bertrand Russell Ndio Uliyowahamasisha Ugiriki/Uyunani Ya Kale Kufanya Makubwa Katika Nyanja Zote za Kimaisha na Hata Baadaye Kuistaarabisha Ulaya.
Rumi Ya Kale Ndio Baadaye Ikaja Kusambaza Mawazo Mengi na Falsafa Nyingi Ilizorithi Kutoka Ugiriki Ya Kale Katika Bara Zima La Ulaya. Kisha Baadaye Sana Ndipo Wazungu Walizunguka Kuitawala Dunia na Kusambaza Ushawishi Wao na Falsafa Nyingi Dunia Nzima na Mpaka Leo Hii Bado Wanaonekana Ndio Watu Wajanja Zaidi Duniani Au Waliopiga Hatua Zaidi Katika Kuwa “Civilised.”
Sasa Nchi Ya Ugiriki Ya Kale Ilikuwa Inafanana Vitu Vingi Sana na Nchi Ya Wachagga Namna Ilivyokuwa, Kuanzia Mifumo Ya Utawala Mpaka Mahusiano Ya Kihistoria Baina Ya Himaya Zake. Hivyo Ugiriki/Uyunani Ya Kale ni Mfano Mzuri Sana wa Kufananishia na Nchi Ya Wachagga Ikiwa Mtu Anajiuliza Suala Lolote La Kimfumo au Siasa za Wachagga.
Katika Kufanana Huko Tunaweza Kufananishia Himaya za Ugiriki Ya Kale na Uchagga Kama Ifuatavyo. Machame Tunaweza Kuifananishia na Athens, Himaya Ya Ugiriki Ya Kale Iliyosifika Kwa Viwango vya Juu vya Kitaaluma na Kutoa Wanafalsafa Wengi Bora Sana. Kibosho Tunaweza Kuifananisha na Sparta Ambayo Ilikuja Kuwa Imara Sana Kijeshi Mpaka Kufanikiwa Kuiangusha Athens Iliyokuwa na Imara Kitaaluma na Kiuchumi. Na Kweli Kibosho Licha Ya Kuonewa Sana na Machame Kwa Miaka Mingi Baadaye Wakati wa Mangi Sina Mushi Ilikuja Kufanikiwa Kuiangusha na Kuitawala Machame.
Old Moshi Tunaweza Kuifananisha na Macedonia, Himaya Ya Ugiriki Ya Kale Iliyokuja Kuimarishwa na Philip II, Baba Yake Alexander The Great na Kufanikiwa Kuiangusha Uyunani/Ugiriki Yote na Kuitawala. Kama Jinsi Old Moshi Ilivyoimarishwa Zaidi Wakati wa Utawala wa Mangi Rindi Mandara na Kuwa na Nguvu Kilimanjaro Kisha Akafuata Mtoto Wake Mangi Meli Mandara Kama Jinsi Philip II Alipofuatiwa na Mtoto Wake Alexander The Great.
Marangu Tunaweza Kuifananisha na Korintho Sehemu Ambayo Himaya Zenye Nguvu Zilikuwa Zikifanyia Maridhiano Au Vita. Kilema Tunaweza Kuifananisha na Thebes Ambayo Iliwahi Kuwa na Nguvu Sana Kijeshi na Hata Mpaka Mwisho Haijawahi Kuwa Dhaifu Sana. Mamba Tunaweza Kuifananisha na Argos Ambayo Nay Mara Nyingi Ilikuwa na Nguvu Sana. Mwika Tunaifananisha na Rhodes, Uru Tukaifananisha na Syracuse.
Kirua Vunjo Tukaifananisha na Eretria, Siha Tukaifananisha na Elis. Kisha Eneo La Rombo Tunaweza Kulifananisha na Eneo La Ionia Maeneo Ya Bahari Ya Agean. Ni Eneo Ambalo Lilikuwa Linazungumza Kigiriki Cha Mashariki Likiwa Upande wa Kaskazini Zaidi Kama Jinsi Ambavyo Eneo La Rombo na Himaya Zake Nyingi Lilivyo Upande wa Mashariki Zaidi Ya Kilimanjaro.
Ufananisho Huu Nilioutoa Nimetunga Mwenyewe na Sio Kwamba Unaendana Kwa Kiasi Kikubwa Sana Ila Kwa Ajili Ya Huu Mjadala ni Mifano Ambayo Nimeona Kea Mbali Inakaribiana Namna Ilivyokuwa Katika Ugiriki Ya Kale. Mtu Mwingine Anaweza Kupangilia Vinginevyo na Bado Akawa Sahihi Pia.
Alexander The Great au Maarufu Pia Kama Alexander III of Macedonia Anahisiwa Kuwa ni Moja Kati Ya Watawala Waliowahi Kuwa na Nguvu Sana Duniani Katika Historia na Kutawala Eneo Kubwa Sana Duniani Pengine Akiongoza au Kuwa Sambamba na Watawala Wengine Kama Wakina Genghis Khan wa Himaya Ya Mongolia Ya Zamani na Watawala wa Uajemi Ya Kale. Alexander The Great Alikuwa ni Mtoto wa Philip II Ambaye Aliingusha na Kuitawala Ugiriki Yote Akisaidiana na Mtoto Wake Alexander.
Sasa Katika Historia Ya Wachagga Kilimanjaro Mfanano wa Alexander The Great Unaweza Kukaribiana Zaidi na Mangi Meli Mandara Japo Kuna Tofauti Kubwa Sana Pia. Mfanano Uliopo ni Kwamba Alexander The Great Alikuwa Ameachiwa Himaya Yenye Nguvu Sana na Baba Yake Philip II Kama Jinsi Mangi Meli Mandara Alivyokuwa Ameachiwa Himaya Yenye Nguvu na Baba Yake Mangi Rindi Mandara.
Lakini Pia Alexander The Great Alikuwa ni Mwenye Ari Kubwa Ya Kuingia Madarakani na Kufanya Mambo Makubwa Sana Katika Utawala Wake, Kama Jinsi Mangi Meli Mandara Alivyokuwa na Ari Ya Kuingia Madarakani na Kufanya Mambo Makubwa Sana Katika Utawala Wake.
Kwenye Kitabu cha “Mission to Kilimanjaro” Kilichoandikwa na Alexander Le Roy Anasema Mangi Meli Alikuwa Amejiandaa Kufanya Mambo Makubwa Sana Kwenye Utawala Wake na Mara Baada Ya Kuwashinda Vita Wajerumani na Kuwaondoa Kilimanjaro Mwaka 1892 Aliajitangaza Kwamba Yeye Ndiye Mtawala Mkuu wa Kilimanjaro Licha Ya Kwamba Mangi Sina Mushi Upande Wake wa Mashariki Alikuwepo na Alikuwa na Nguvu Kubwa sana Pia Kijeshi.
Mangi Sina Mushi Tunaweza Kumfananisha na Leonidas I wa Sparta Ambaye Alikuwa na Nguvu Kubwa Sana Kijeshi na Hata Himaya Yake Ilikuwa ni Ngumu Sana Kuangushwa na Majeshi Ya Philip II wa Macedonia. Lakini Hata Hivyo Hawakuwahi Kupigana Vita na Mangi Meli Kutokana na Mabadiliko Ya Kisiasa Yaliyokuwepo.
Hivyo Mangi Meli Mandara Alikuwa na Ujasiri, Ari na Hamasa Kubwa Ya Kufanya Makubwa Kama Alexander The Great Lakini Licha Ya Kufanikiwa Kuwaondoa Wajerumani Kilimanjaro na Kuanza Mikakati Zaidi Ya Kujiimarisha Kufanya Makubwa Baada Ya Kama Mwaka Mmoja na Nusu Wajerumani Walirudi Tena na Kufanikiwa Kumdhibiti. Tofauti na Alexander The Great Yeye Alifanikiwa Kukusanya Majeshi Yote Ya Ugiriki na Kwenda Kupambana na Himaya Nyingine Zenye Nguvu na Kuziangusha na Kuongeza Nguvu Yake Zaidi.
Lakini Kama Mangi Meli Mandara Angefanikiwa Kutanuka Bila Wajerumani Kurudi Pengine Angefika Mbali Zaidi na Kuziangusha Himaya Imara Afrika Mashariki Kama Vile Himaya Buganda Iliyokuwa na Nguvu Sana Pia Kwa Kutumia Jeshi La Kilimanjaro. Hii ni Kama Jinsi Ambavyo Alexander The Great Alifanikiwa Kuiangusha Himaya Kubwa Yenye Nguvu Zaidi na Yenye Wanajeshi Wengi Zaidi Ya Uajemi Iliyokuwa Chini Ya Mtawala Mashuhuri na Mwenye Nguvu Darius III. Hakuna Mtu Alitegemea Kwamba Alexander The Great Angeweza Kumwangusha Mtu Imara na Mwenye Nguvu na Mwenye Himaya Kubwa Kama Darius III wa Himaya ya Uajemi. Na Baada Ya Kufanikisha Kumwangusha Darius III wa Uajemi, Alexander The Great Alikuwa Hazuiliki Tena.
Sasa Ikiwa Kwamba Mangi Rindi Mandara Baba Yake Mangi Meli Alikuwa Akipeleka Majeshi Yote Ya Kilimanjaro Kwenda Kupambana Nje Ya Kilimanjaro Mpaka Huko Loita na Masai Mara Upande wa Kenya na Kurudi na Ushindi Mkubwa ni Wazi Kwamba Mangi Meli Ili Kufanya Makubwa Zaidi Kumzidi Baba Yake Kama Jinsi Alexander The Great Alivyomzidi Baba Yake Philip II Angeweza Kwenda Mbali Zaidi Mpaka Kaskazini Ya Ziwa Victoria. Philip II Alikuwa na Mafanikio Makubwa Sana Pengine Kuliko Mtawala Mwingine Yeyote wa Ugiriki Ya Kale Hapo Kabla Hapo Kabla Lakini Alexander The Great Aliazimia Kufanya Makubwa Kumzidi Baba Yake na Akafanikisha.
Mangi Rindi Mandara, Baba Yake Mangi Meli Pia Alikuwa na Mafanikio Makubwa Kwani Aliweza Kukusanya Majeshi Karibu Yote Ya Kilimanjaro na Kwenda Kuitiisha Mpaka Huko Usambara na Tanga Kwa Ujumla, Loita Kenya, Ukamba na Maeneo Mengine. Mangi Meli Naye Aliazimia Kufanya Makubwa Kuliko Baba Yake Hivyo Endapo Kama Angedhibiti Eneo Hilo Angeweza Kujiamini na Kuangusha Himaya Kubwa Zaidi na Kuzitawala na Kuimarisha Sana Utawala wa Kilimanjaro Kama Alexander The Great Alivyofanya Kwa Ugiriki Ya Kale na Hata Kueneza Tamaduni za Wagiriki Maeneo Mbalimbali.
Kutokana na Wachagga Kuwa na Historia Inayofanana na Wagiriki Imeweza Kuwa ni Yenye Kuvutia Sana Ukilinganisha na Historia za Jamii Nyingi Mbalimbali. Tuendelea Kuhifadhi Historia Yetu Yenye Mambo Mengi Makubwa na Muhimu Ya Kujivunia na Kuweza Kuirithisha Kwa Vizazi Vinavyofuata Kwani ni Ya Kipekee Sana na Inasaidia Sana Kuwajengea Watu Kujiamini Binafsi(Self Esteem) Kuelekea Kufanya Makubwa Kwenye Maisha Yao.
Tunafanya Hivyo Kwa Kununua Kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” Kwani Maandishi Hudumu Kwa Maelfu Ya Miaka na Kuendelea Kuhamasisha Watu Kwa Maelfu na Maelfu Ya Miaka. Kununua, Kusoma na Kuhifadhi Vitabu/Maandishi Ndio Njia Sahihi Zaidi Ya Kuhakikisha Kwamba Jamii Inaendelea Kuwa Hai Kwa Mamia Mpaka Maelfu Ya Vizazi Vinavyokuja. Hivyo Tuendelee Kuipa Uhai Jamii Yetu Kwa Miaka Mingi Mbele Kwa Kununua Kitabu cha Historia Kwa Wingi Zaidi Badala Ya Kuendelea Kulalamika Kwamba Jamii Yetu Inapotea.
Karibu Sana.