TUANDIKE KUHUSU KOO ZETU.

Wachagga ni jamii yenye watu wengi sana na ni moja kati ya makabila/jamii kubwa na maarufu sana Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla. Kupitia Fasihi/Literature wachagga ni kati ya makabila maarufu sana Afrika. Na kabla ya uhuru wa Tanganyika wachagga walikuwa ni kati ya jamii chache zilizokuwa zinaongoza kwa maendeleo makubwa sana sio tu kwa …

TUNAELEKEA WAPI KAMA JAMII?

Wakati wowote katika historia, swali moja ambalo watu au jamii hupaswa kujiuliza ni tunaelekea wapi? Hili ni swali muhimu sana kwa sababu linasaidia kuwapa watu/jamii fursa na nafasi ya kuamua kwa usahihi kule wanakotaka kuelekea badala ya kusubiri hatma iamue yenyewe. Kwa sababu watu wakishindwa kuamua wanaelekea wapi watajikuta sehemu ambayo hawakutamani kufika na kujilaumu …

MANGI LEMNGE KUIMBERE MOSHI WA MAMBA

Pichani kushoto ni Mangi Lemnge Kwimbere (baba yangu)aliyekuwa Mangi wa Mamba kuanzia miaka ya katikati ya 1930 hadi miaka ya 1950 alipochaguliwa kuwahead chief wa Vunjo kabla ya kuanza cheo cha Mwitori.Kulia ni baba yake Mangi Kwimbere Mlawi..aliyepokea umangi kwa Ukyekekyi Mlawi. Kwimbere ndiye aliyewapa Wamisionari eneo la Ashira mahali palipokuwa wakitupwa watu waliokufa (maiti). …