MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHAGGA (CHAGGA DAY) YA MWAKA 2022.

KIJIJI CHA MAKUMBUSHO YA TAIFA KIJITONYAMA, DAR ES SALAAM NOV. 12, 2022.

– Kama ambavyo tumeendelea kufahamu kwamba kila tarehe 10/Novemba ya kila mwaka ilikuwa ni siku kuu kubwa ya maadhimisho ya siku ya wachagga iliyokuwa ikifanyika zamani Moshi.

– Siku hii ilikuwa siku muhimu sana kwa wachagga kwani ndio siku iliyokuwa ikitumika kama kilele cha kusherehekea na kuendelea kuhimiza maendeleo ya wachagga kiuchumi, kisiasa na kitamaduni katika mifumo ya dunia ya kisasa. Wachagga waliadhimisha siku hii ambayo walianza kutumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua uongozi ambao uliingia kwenye mfumo mzima wa kuendesha serikali yao wenyewe iliyowaletea maendeleo makubwa miaka ya 1950’s/1960’s.

– Lakini baadaye, utawala wa Waingereza ulipoondoka na nchi kuingia kwenye awamu ya kwanza ya Jamhuri aliyechukua madaraka ya serikali ya Jamhuri hakuifurahia na hivyo baada ya miaka michache ilifutwa. Lakini kwa kuwa hakukuwa na hoja ya msingi ya kuifuta kwa sababu ilikuwa ni sherehe ya kijamii kama sherehe za vikundi vingine vya kijamii watu walianza kuhamasisha irudishwe na kuendelea kusherehekewa kama zamani.

– Baada ya wachagga wengi kuihitaji sana siku kuu hii kubwa kwa wachagga irudishwe, Urassa entertainment wakishirikiana na Kijiji cha Makumbusho ya Taifa wamejitahidi kuhakikisha wanaandaa siku kuu hii ya wachagga itakayofanyika ndani ya Kijiji cha Makumbusho ya Taifa Kijitonyama, Dar es Salaam.

– Wachagga wote wanakaribishwa siku hiyo, waje wakiwa na ubunifu mbalimbali na michango zaidi ya mawazo juu ya namna ya kuendelea kuboresha na kuhamasisha zaidi watu kuitambua na kufanyika kwa siku kuu hii kila mwaka, kila mahali na kwenye kila familia ya wachagga popote walipo duniani.

– Lengo hasa la maadhimisho haya ya sherehe za siku kuu hii ya wachagga kwa sasa kama ilivyokuwa zamani zile ni ili kuendelea kuhamasisha maendeleo makubwa zaidi na zaidi ya kiuchumi ya wachagga na kule wanakotokea pamoja na kuhamasisha umoja na mshikamano miongoni mwetu. Ni jambo kubwa sana kukutana wachagga wote na hata wengine watakaopenda kujumuika nasi tukiwa wenye hamasa kubwa ya kuzungumzia na kuhamasishana mambo yenye maslahi ya pamoja kwetu sote.

– Hata hivyo kwa sababu tarehe ya siku yenyewe ya wachagga ya Novemba 10 inaangukia siku ya Alhamisi ambayo ni siku ya kazi tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni siku kuu ya kitaifa Kilimanjaro, basi maadhimisho haya ya sasa yamesogezwa siku ya Jumamosi ya Novemba 12. Siku hiyo kutakuwa na burudani za kila aina na shamra shamra kubwa za furaha na hamasa ya siku hii kubwa sana kwa wachagga. Kwa wale watakaobaki nyumbani kwa sababu mbalimbali basi nao wasiache kusherehekea kwa namna yao ya kipekee kuhusu maisha na utamaduni wa wachagga kwa ujumla.

– Kwa yeyote anayeweza kuhudhuria usipange kukosa.

– Kwa Mawasiliano Piga namba +255 745 260 606.

Karibu kwa Maoni au Maswali.

Urithi Wetu Wachagga.

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *