– Ukoo wa Masaki ni ukoo maarufu katika eneo la himaya ya umangi Siha/Sanya Juu katika vijiji vya Samaki Maini na Mae. Wachagga wa ukoo wa Masaki wakiwa wameshuka kutoka kwenye plango ya Shira waliweka makazi yao ya mwanzoni ya kudumu katika kijiji cha Samaki Maini sambamba na ukoo wa Orio/Urio na Kileo.
– Kutoka kwenye historia inaelezwa kwamba ukoo wa Masaki ndio wachagga wa kwanza katika eneo la himaya ya umangi Siha/Sanya Juu kupanda mazao kipindi cha mvua za masika. Hivyo ukoo wa Masaki ndio wakulima wa mwanzoni zaidi katika eneo hili la himaya ya umangi Siha na walikuwa ni wakulima hodari sana na wafugaji pia.
Tunahitaji mchango wa mawazo zaidi juu ya ukoo huu Masaki ambao ni mkongwe sana magharibi ya Kilimanjaro.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Masaki?
2. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Masaki?
3. Kama wewe ni wa ukoo wa Natai una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
4. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo huo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
5. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Masaki?
6. Wanawake wa ukoo wa Masaki huitwaje?
7. Una rafiki yako yeyote wa ukoo wa Masaki?
8. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Masaki?
Karibu kwa Maoni na Maswali.