UKOO WA NDOSI.

– Ukoo wa Ndosi ni ukoo mkongwe sana na unaopatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mbweera, Masama kati. Ukoo wa Ndosi ni tawi la ukoo wa Mboro ambao tulishaujadili hapa kwa kina na matawi yake lakini tawi lilikuwa na nguvu sana katika eneo hili la Masama kati na ndio ulikuwa ukoo wa watawala eneo hili.

– Kutoka kwenye historia tawi la ukoo huu wa Mboro lililokuja kuchukua jina la ukoo wa Ndosi ambao waliweka makazi ya kudumu katika eneo la Mbweera, Masama katika Machame ya magharibi walitokea katika kijiji cha Sonu Masama.

– Kwa tafiti zilizofanyika katikati ya karne ya 20 zinaonyesha kwamba tawi hili la ukoo wa Mboro linalojulikana kama ukoo wa Ndosi walihama Sonu chini ya kiongozi wao wa ukoo aliyeitwa Ikere mwishoni mwa karne ya 18. Mzee wa mwisho wa ukoo wa Ndosi wa Mbweera, Masama ambaye ametajwa zaidi kwenye historia aliyekuwepo hai mpaka katikati ya karne ya 20 alijulikana kwa jina la Lula.

– Ukoo wa Ndosi ukiwa ni tawi la ukoo wa Mboro kama kawaida yake tunajua walikuwa ni watu shupavu na wapambanaji sana wanaotambuliwa vyema na historia. Huu ndio ukoo ambao uliweza kuzidiwa nguvu ya ushawishi na ukoo wa Mushi katika eneo la Masama waliochukua utawala wa himaya mpya ya umangi Masama mwaka 1950.

– Ukoo wa Ndosi uko kwa wingi sana katika kijiji cha Mbweera, Masama na maeneo ya jirani.

– Ukoo wa Ndosi unapatikana pia katika vijiji vya Sonu na Ngira, Masama.

– Ukoo wa Ndosi unapatikana pia kwa uchache katika kijiji cha Mudio, Masama.

– Ukoo wa Ndosi unapatikana pia kwa wingi huko Meru.

– Ukoo wa Ndosi unapatikana kwa kiasi pia katika vijiji vya Shari na Kyeeri, Machame.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Ndosi?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Ndosi?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Ndosi?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Ndosi una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Ndosi wa kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mboro kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Ndosi?

7. Wanawake wa ukoo wa Ndosi huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa ukoo wa Ndosi?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Ndosi?

Karibu kwa Maoni na Maswali.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *