UKOO WA LEMA.

– Ukoo wa Lema ni ukoo mkubwa sana wa wachagga mashuhuri na wenye heshima kubwa sana ndani na nje ya Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Lema wamekuwa ni watu wapambanaji na wenye msimamo thabiti katika mambo ya msingi tangu karne nyingi zilizopita mpaka sasa. Ukoo wa Lema una watu wengi mashuhuri wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania. Huu ni ukoo unaojulikana kwa kuwa na madaktari wengi sana pia.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Lema asili yake ni Machame kutokea kwenye kizazi cha Mangi Mashami ambaye ni mtawala wa zamani sana aliyeanzia maisha katika kijiji cha Uswaa Sienyi. Baadaye utawala wa vizazi vilivyofuata wakapandisha mpaka juu zaidi na kuweka makazi katika eneo la Shari/Uraa, Machame katikati ya mto Marire na mto Kikafu. Kisha walipandisha tena mpaka Kalali na kuendelea juu zaidi na kuweka makazi ya kudumu katika kijiji cha Foo, Machame.

– Baada ya kuishi katika kijiji cha Foo kwa muda wachagga wa ukoo wa Lema walilazimika kuondoka Foo iliyokuwa ngome ya ukoo wa Mushi na kuvuka mto Semira uliopo upande wa magharibi wa kijiji cha Foo na kwenda kuweka makazi ya kudumu katika kijiji cha Nronga, Machame. Tangu wakati huo kijiji cha Nronga, Machame kimekuwa ndio ngome ya ukoo wa Lema mpaka leo hii. Hata hivyo wachagga wengine wa ukoo wa Lema walielekea upande wa magharibi zaidi kuvuka mto Marire na hata mto Namwi na kuweka makazi ya kudumu katika vijiji mbalimbali vya Masama pia. Baadhi ya wachagga wa ukoo wa Lema walioondoka Foo walielekea upande wa mashariki na kuweka makazi katika vijiji vya Nkuu na hata Lyamungo.

– Ukoo wa Lema umekuwa ni ukoo wenye nguvu kubwa ya ushawishi katika siasa za uchaggani na hususan Machame kiasi kwamba ulikuwa ukitikisa baadhi ya tawala zilizokuwa za kikatili kama vile utawala wa Mangi Ndesserua wa Machame. Wakati wa utawala wa Mangi Ndesserua wa Machame katikati ya karne ya 19 wakati Machame kukiwa na taharuki kubwa ya kisiasa kutokana na ukorofi wa Mangi Ndesserua wachagga wa ukoo wa Lema kama ilivyokuwa wa wachagga wengine walikuwa ni moja ya wahanga wa siasa za utawala wake. Hivyo wengi wa wachagga wa ukoo wa Lema waliokuwa wanapingana na siasa Mangi Ndesserua walijikuta wanakimbilia magharibi ya Machame huko Masama na hata mpaka Meru.

– Inasemekana kwamba wachagga wa ukoo wa Lema waliokimbilia Meru peke yake katikati ya karne ya 19 kukwepa mkono wa chuma wa Mangi Ndesserua walikuwa ni wengi kiasi kwamba waliweza kutengeneza tawi jipya kabisa la ukoo huko Meru. Lakini hata hivyo katika kurudisha hali ya utulivu Machame na kujiimarisha kisiasa kutoka kwenye taharuki kubwa Mangi Ndesserua alijaribu kufanya maridhiano na wachagga wa ukoo wa Lema wa kijiji cha Nronga kwa kuoa mwanamke kutoka kwenye ukoo huo aliyeitwa Nuya.

– Nuya, mke wa Mangi Ndesserua kutoka kwenye ukoo wa Lema wa kijiji cha Nronga, Machame ndiye alikuja kumzaa Shangali aliyekuja kuwa Mangi wa Machame baadaye na vizazi vyake kuja kuwa na ushawishi mkubwa kisiasa Machame mpaka katikati ya karne ya 20. Hii ni licha ya utawala wa Mangi Shangali kuyumba sana mwanzoni. Nuya mwenyewe mama yake Shangali kutoka kwenye ukoo wa Lema alikuja kuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye siasa za Machame na uchaggani kwa ujumla na anahesabika kuwa ni mmoja kati ya wanawake shupavu na mashuhuri sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro.

– Ukoo wa Lema wameendelea kufanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali na baadhi ni watu wenye majina makubwa sana katika nyanja mbalimbali za kimaisha huku kijiji cha Nronga ambacho ndio ngome ya ukoo wa Lema kikiwa ni moja kati ya vijiji vya Uchaggani Kilimanjaro vyenye heshima ya kipekee. Hata hivyo bado tunahitaji kufahamu zaidi juu ya ukoo huu mashuhuri wa wakoLema na maeneo zaidi wanakopatikana na maeneo zaidi walikosambaa.

– Wachagga wa ukoo Lema wanapatikana maeneo mengi hususan upande wa magharibi ya Kilimanjaro kuanzia sehemu za Meru.

– Ukoo wa Lema wanapatikana maeneo ya Sanya Juu hususan katika kijiji cha Lawate.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lukani, Masama.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Lemira, Masama.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mbwoeera na Mudio, Masama.

– Ukoo wa Lema wanapatikana katika kijiji cha Mroma, Masama.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Saawe, Masama.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sonu na Ngira, Masama.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kyeeri, Machame.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Lema unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Wari, Machame.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nronga, Machame.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Foo, Machame.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa wingi pia katika kijiji cha Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa wingi sana katika kitongoji cha Kimbushi, Machame.

– Ukoo wa Lema wanapatikana kwa wingi sana katika vijiji vya kata ya Lyamungo Machame.

Tunahitaji kupata mchango zaidi wa mawazo kuhusu ukoo huu mashuhuri wa wachagga Kilimanjaro ili kuongezea kwenye tafiti za koo na hata maudhui zaidi kuhusu ukoo huu.

Karibu kwa mchango zaidi wa mawazo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Lema?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Lema?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Lema?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Lema una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Lema wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Lema kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Lema?

7. Wanawake wa ukoo wa Lema huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Lema?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Lema?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *