UKOO WA SHOO.

– Ukoo wa Shoo ni ukoo mkubwa na mashuhuri sana wa kichagga unaopatikana kwa wingi zaidi Machame na kwa kiasi maeneo mengine mbalimbali ya Uchaggani, Kilimanjaro. Ukoo wa Shoo umekuwa ukisifika kama ukoo wenye watu wengi makini wenye kujituma sana na wanaofanya vizuri sana katika maisha.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Shoo unatajwa kuwa moja kati ya koo kubwa zilizokuwa na wanaharakati wengi waliokuwa wanasimama imara kutetea haki za kiraia dhidi ya watawala iwe ni wakoloni au watawala wazawa. Ukoo wa Shoo umeendelea kukua na kuimarika na kutoa watu wengi zaidi wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania.

– Kutokana na kutanuka kwa ukoo wa Shoo ukoo huu unapatikana katika vijiji mbalimbali huko Masama.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Wari, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nronga, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Foo, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa wingi sana katika kitongoji cha Nkweshoo, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa wingi sana katika kitongoji cha Kimbushi, Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa wingi sana katika kata ya Lyamungo, Machame.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Umbwe, Kibosho.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Shoo unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

Ukoo wa Shoo ni ukoo mashuhuri lakini taarifa zake bado ni chache sana, tunahitaji mchango wa mawazo zaidi kuhusu ukoo huu mashuhuri wa Shoo katika kuchangia tafiti hizi za koo.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Shoo?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Shoo?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Shoo?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Shoo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Shoo wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Shoo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Shoo?

7. Wanawake wa ukoo wa Shoo huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Shoo?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Shoo?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *