UKOO WA MSHANGA.

– Ukoo wa Mshanga ni ukoo mkongwe na uliotawanyika maeneo mbalimbali ya Uchagga, Kilimanjaro kuanzia magharibi mpaka mashariki kabisa. Huu ni ukoo wa wachagga wasiotajwa sana lakini wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro. Japo ukoo huu unapatikana maeneo mengi lakini karibu kwenye kila eneo wanalopatikana wanapatikana kwa uchache.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Mshanga unafahamika kwamba ndio ukoo uliokuwa unatawala katika eneo la kijiji cha Mori ambacho ni sehemu ya kijiji cha Tela, Old Moshi. Mzee wa zamani zaidi anayekumbukwa ambaye pia alikuwa ni ndio kiongozi wa ukoo huu na mtawala wa eneo la Mori lililokuja kuwa sehemu sehemu ya kijiji cha Tela, Old Moshi aliitwa Masika.

– Ukoo wa Mshanga umeendelea kusambaa magharibi na mashariki ya Kilimanjaro kupatikana maeneo mbalimbali japo sio kwa idadi kubwa. Wako wachagga mbalimbali wanaofanya vizuri kitaaluma na kibiashara kutoka kwenye ukoo wa Mshanga ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Ukoo wa Mshanga unapatikana kwa uchache maeneo ya vijiji vya kata ya Kindi, Kibosho.

– Ukoo wa Mshanga unapatikana kwa kiasi katika baadhi ya vijiji ya Uru hasa vya kata ya Shimbwe, Uru.

– Ukoo wa Mshanga unapatikana kidogo maeneo ya kijiji cha Korini Juu, Mbokomu.

– Ukoo wa Mshanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tela, Old Moshi.

– Ukoo wa Mshanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Mshanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Mshanga unapatikana kwa kiasi kwenye baadhi ya vijiji Mkuu, Rombo.

– Hata hivyo licha ya ukoo huu kusambaa na kutanuka bado kuna taarifa chache sana kuhusu ukoo wa Mshanga na namna ulivyoweza kuenea maeneo mbalimbali ya Uchagga, Kilimanjaro bila kuongezeka sana kwa idadi. Tunahitaji mchango zaidi wa mawazo ili kuweza kuongezea kwenye tafiti zaidi sambamba na kufahamu vijiji zaidi ambavyo ukoo huu unapatikana kwa ajili ya utafiti zaidi. Taarifa zaidi tunazokwenda kuzipata kutoka kwako zitasaidia kuongeza maudhui ambayo yatatumika kuhamasisha watu wa ukoo wa Mshanga kuimarisha mshikamano wao kuelekea kufanya makubwa kwa ngazi ya ukoo na hata kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja.

Karibu mchango wa mawazo zaidi.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mshanga?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mshanga?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mshanga?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mshanga una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Mshanga wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mshanga kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mshanga?

7. Wanawake wa ukoo wa Mshanga huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mshanga?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mshanga?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *