UKOO WA LYIMO.

– Ukoo wa Lyimo ni moja ya koo kubwa, kongwe, mashuhuri na maarufu sana unaosambaa maeneo mengi ya Uchaggani, Kilimanjaro na unaopatikana kwa wingi sana kila eneo ulipo. Bila mashaka yoyote huu ni ukoo uliotoa wa wenye wachagga mashuhuri na uliotoa watu wengi sana maarufu katika historia ya wachagga Kilimanjaro kwa karne nyingi zilizopita na hata mpaka sasa.

– Kutoka kwenye historia makazi ya asili ya mwanzoni ya ukoo wa Lyimo ni katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu ambapo ndio kama kiini cha utawala wa himaya ya umangi Marangu. Hata hivyo inasemekana kwamba wazee waanzilishi wa ukoo wa Lyimo kupitia Mzee maarufu aliyejulikana kwa jina la Mlambaki walitokea upande wa mashariki zaidi huko Usseri, Rombo walikoacha ndugu wengine na kusogea kuweka makazi ya kudumu katika ukanda wa juu wa Marangu katika vilima vya Kifinika katika eneo linalojulikana kama Fuphu Lya Komkuu ambalo kwa sasa ni ndani ya msitu wa mlima Kilimanjaro juu ya Mandara hut.

– Wachagga wa ukoo wa Lyimo walishuka kuelekea ukanda wa chini wa Marangu na kupambana na koo nyingi ili kuweza kuweka makazi katika eneo bora zaidi. Mwishoni walifanikiwa kupambana na ukoo wa Mboro na kuwaondoa katika eneo la kijiji cha Lyamrakana ambapo waliweka makazi ya kudumu na kutawala. Hata hivyo licha ya baadaye kuzidiwa nguvu na ukoo wa Mtui na kuhamishwa kwa nguvu katika kijiji cha Lyamrakana kwa muda walifanikiwa kurudi kupambana tena mpaka kuwashinda vita wachagga wa ukoo wa Mtui wa Mshiri na kurudisha makazi yao ya kudumu katika kijiji cha Lyamrakana.

– Ukoo wa Lyimo kutokea Lyamrakana walisambaa maeneo mengi ya Uchaggani, Kilimanjaro mashariki na magharibi. Tawi la mwanzoni zaidi la ukoo wa Lyimo kuondoka Lyamrakana, Marangu ni Lyimo ya Kilema ambayo iliondoka Lyamrakana kwenye karne ya 17 hivi baada ya ndugu kutoelewena. Baadaye ukoo wa Lyimo kwa sababu mbalimbali hususan za kisiasa waliendelea kusambaa maeneo mengine ya kuweka makazi kutoka kwenye matawi ya awali.

– Tawi lingine maarufu la ukoo wa Lyimo walioondoka Lyamrakana ni tawi la ukoo wa Lyimo ya Kondeni, Mwika. Tawi la ukoo wa Lyimo ya Mwika, Kondeni ambao ni ukoo mkubwa sana unasemekana kutoka kwenye historia kwamba walitokea Lyamrakana, Marangu mwishoni mwa karne ya 19 kwa lengo la kuitawala Kondeni na kuimarisha ushawishi wao wa kisiasa Kondeni, Mwika dhidi ya koo zilizokuwa nguvu Kondeni kama vile Mangesho, Ngomuo, Teemba n.k. Lyimo hii ya Kondeni ikaja kuwa moja kati ya matawi maarufu ya ukoo wa Lyimo na wanaopatikana kwa idadi kubwa sana.

– Ukoo wa Lyimo wamekuwa wakisifika kwenye historia kama wachagga wenye kupenda kutumia mbinu, fitna na ujanja kufanikiwa kisiasa wakati wa siasa za zamani za uchaggani kuliko kutumia nguvu, majeshi na vita kama ilivyokuwa kwa watawala wengi. Hii ilichangia kusaidia ukoo wa Lyimo kusambaa maeneo mengi na kwa idadi kubwa na hivyo kuwa maarufu na mashuhuri sana mpaka leo. Ukoo huu umeendelea kusambaa maeneo mengi kuelekea mashariki na magharibi ya Uchagga, Kilimanjaro na kuanzisha matawi mengi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Okaseni, Uru.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mwasi Kusini, Uru.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Mnini, Uru.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiwalaa, Mbokomu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kiboriloni, Moshi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Tela, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Tsudunyi, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kwamare, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi pia katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Pofo, Kilema.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Masaera, Kilema.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kilema chini, Kilema.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ngangu, Kilema.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kyura, Kilema.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Rosho, Kilema.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Rauya, Marangu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Arisi, Marangu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Lyasongoro, Marangu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Mshiri, Marangu.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kotela, Mamba.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Kimbogho, Mamba.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kiria, Mamba.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Mkolowony, Mamba.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Kimangara, Mamba.

– Ukoo wa Lyimo unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Lekura, Mamba.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Matala, Mwika Kusini.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Shokony, Mwika.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana katika kijiji cha Kirimeni na Uuwo, Mwika.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa kiasi katika kata ya Mahida, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Lyimo wanapatikana kwa uchache sana Kerio, Mashati, Rombo.

Ukoo wa Lyimo ambao ni ukoo wa wachagga mashuhuri wengi ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi na ukoo mkubwa na wenye matawi mengi sana lakini bado taarifa za namna ukoo huu umegawanyika na kusambaa ni chache. Hivyo tunahitaji taarifa zaidi kwa ajli ya utafiti zaidi lakini ikiwa ni sambamba na kuandika na kuhifadhi maudhui mengi ya ukoo huu yanayoweza kuwa chache na hamasa ya kuwaleta wanaukoo huu pamoja kuelekea kufanikisha mambo makubwa katika maisha kwa ngazi ya ukoo na kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Lyimo?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Lyimo?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Lyimo?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Lyimo una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Lyimo wa kutokea kijiji gani?

5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Lyimo kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Lyimo?

7. Wanawake wa ukoo wa Lyimo huitwaje?

8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Lyimo?

9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Lyimo?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *