HUU MTAZAMO HASI UNABOMOA ZAIDI KULIKO KUJENGA.

– Ni rahisi kusambaza picha kama hizi ambazo zinaonekana kama ni za kuchekesha japo humjui nani aliyezitengeneza na alikuwa na lengo gani. Kuna uwezekano picha hizi huwa zinatengenezwa na mtu/watu wenye malengo ya kuharibu taswira nzima ya hili suala la kurudi nyumbani ili kudhoofisha au kuionyesha jamii kwamba hayo ndio haswa yanayofanyika.

– Je, katika mambo mengi muhimu yanayofanyika hii ndio taswira tuliyochagua isambae kwa jamii ambayo ndio inajenga mtazamo wa kile kinachokwenda kufanyika?

– Je, ni nani anatengeneza picha hizo na ana lengo gani? Huenda kweli mtu huyo ana lengo la kuchekesha watu tu, lakini je, anajua madhara ya mitazamo inayojengeka hapo kwa watu wengi ambao huwa hawajishughulisha kutafakari kwa kina undani wa kile anachokiana?

– Je, huyo aliyetengeneza hiyo anayoita ripoti ya Christmas kutoka Uchaggani, ni nini kilipelekea yeye kuwaza kutengeneza hiyo ripoti hasi na sio chanya? Ni nini ulikuwa ni msukumo wake kufanya hivyo?

– Ikiwa kweli tunahitaji kufanya kwa ubora zaidi mambo haya yenye umuhimu mkubwa katika kuimarisha mshikamano wa kindugu katika jamii yetu ya wachagga, sio tunahitaji kusambaza maudhui na picha zinazojenga mitazamo chanya ili kuhamasisha na kuboresha zaidi?

Karibu kwa Maoni na Ushauri.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *