UKOO WA SHIRIMA

– Shirima ni ukoo maarufu na mashuhuri sana wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi upande wa mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Shirima ni kati ya koo za wachagga ambazo kongwe, kubwa, mashuhuri na maarufu sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Ukoo wa Shirima pia ni ukoo wenye watu maarufu na wenye mafanikio makubwa ukiwa ni moja kati ya koo kubwa zaidi katika eneo la Rombo na uchaggani kwa ujumla.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Shirima ni ukoo wenye chimbuko lake katika eneo la himaya za umangi za Rombo ukionekana kuwa mashuhuri na unaoheshimika zaidi katika eneo la Mkulya yaani katika eneo la kati ya mto Ungwasi na mto Mlembea. Ukoo wa Shirima pia ni ulikuwa ni ukoo wa watawala katika himaya za umangi kadhaa katika eneo la Mkulya au Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shirima ndio ukoo uliokuwa unatawala katika himaya ya umangi Mrere wakati wa Mangi Kalula na baadaye katika utawala wa mtoto wake Mangi Pauli Kalula, katika eneo hili la Mkulya ambalo mpaka kufikia mwaka 1899 kulikuwa na jumla ya himaya kumi za umangi. Ukoo wa Shirima pia ndio ukoo uliokuwa unatawala katika himaya ya umangi Old Mashati ambayo ilipata umaarufu zaidi wakati wa utawala wa Mangi Senguo aliyekuja kuitawala Mashati yote hapo baadaye, kutoka kwenye ngome yake ya utawala huko Mtimhoo katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shirima pia ndio walikuwa watawala wa himaya ya umangi Olele iliyopo katika eneo la Mkulya ambayo hata hivyo baadaye katikati ya karne ya 20 baada ya utawala wa Mangi Paul Mtauli ilikuja kuunganishwa kwenye himaya ya umangi Usseri iliyopo upande wa mashariki wa mto Mlembea katika eneo la Usseri. Hivyo kwa himaya za umangi za Rombo na hususan katika eneo la Mkulya lililopo katikati ya mto Ungwasi na mto Mlembea ukoo wa Shirima ulikuwa ni ukoo mashuhuri uliotawala himaya kadhaa kati ya himaya takriban kumi za eneo hili mpaka kufikia karne ya 19.

– Hata hivyo ukoo wa Shirima umeendelea kuwa ni ukoo wa watu wengi makini na hasa wafanyabiashara wakubwa wanaofanya vizuri sana maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Moja kati ya wawekezaji na matajiri wakubwa ambaye pia ndiye mwanzilishi na mmiliki mkuu wa kampuni binafsi ya safari za anga hapa Afrika mashariki ya Precision Air inamilikiwa na Michael Ngaleku Shirima kutokea katika ukoo huu wa Shirima ya Ngasseni, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shirima umeendelea kuongezeka sana na kusambaa maeneo mbalimbali na hivyo unapatikana kwa wingi sana sehemu nyingi zaidi.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika kijiji cha Lyasomboro, Marangu.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika kijiji cha Arisi, Marangu.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa uchache katika vijiji vya Mamba.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondiki, Mwika.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mrimbo Uuwo, Mwika.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kirimeni, Mwika.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi katika vijiji vya kata ya Mahida, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mamsera Juu, Mamsera, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mamsera Kati, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika kijiji cha Kidondoni, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika kijiji cha Manda juu, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika kijiji cha Manda chini, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika vijiji vingine vya tarafa ya Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika kijiji cha Mengeni chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika kijiji cha Mengeni Kitasha, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika kijiji cha Aleni, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi pia katika vijiji vya tarafa ya Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana katika vijiji vya kata ya MraoKeryo na KirwaKeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mrere, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi sana pia katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kisale, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi katika vijiji vya kata ya Olele, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ngasseni, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi sana katika vijiji vingine vya tarafa ya Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Shirima unapatikana kwa wingi sana pia katika vijiji vya tarafa ya Tarakeo, Rombo.

– Hata hivyo ukoo wa Shirima umeendelea kukua na kusambaa zaidi katika eneo lote la Rombo pamoja na maeneo ya Vunjo lakini licha ya kuwa na wasomi wengi bado taarifa za namna ukoo huu umeendelea na kusambaa ni chache sana. Hivyo tunahitaji taarifa zaidi kuhusu ukoo huu wa Shirima ili kuweza kuwa na maudhui zaidi yatakayoweza kuhamasisha mashikamano zaidi na ari ya kujituma zaidi miongoni mwa wanaukoo.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Shirima.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Shirima?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Shirima?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Shirima?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Shirima una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Shirima wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Shirima kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Shirima?

9. Wanawake wa ukoo wa Shirima huitwaje?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Shirima?

11. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Shirima?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Shirima?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Shirima kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *