UKOO WA KWEKA.

– Kweka ni ukoo maarufu na mkubwa sana unaopatikana kwa wingi upande wa magharibi ya Uchaggani, Kilimanjaro. Wachagga wengi wa ukoo wa Kweka ni watu wenye nidhamu ya kazi na wenye kujituma wakiwa wamesambaa maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na katika maeneo yote ya nchi na hata nje ya Tanzania.

– Kutoka kwenye historia asili ya ukoo wa Kweka ndani ya Uchagga ni katika vijiji vya kata ya Narumu, Machame. Wachagga wa ukoo huu walikuwa ni watu mahodari sana kwa ufinyanzi zamani na vyombo vingi vya kupikia kwa Uchagga kote hususan vyungu vilikuwa vinatengenezwa na wachagga wa ukoo huu na nyingine za maeneo hayo pamoja na wachagga wa Usseri, Rombo.

– Hata hivyo japo wachagga walikuwa wanategemea pia kununua vyombo kutokea kwenye jamii nyingine nje ya Kilimanjaro lakini walipenda zaidi na kuvisifu zaidi vyombo kutokea Uchaggani Narumu na Usseri kuliko vilivyotoka nje ya Uchaggani. Waliviamini na kuvipenda vyungu vya Uchaggani na hivyo walinunua vyombo kutoka nje ya Uchagga pale tu uzalishaji uliposhindwa kukidhi mahitaji. Dr. Bruno Guttman kwenye, “Poetry and Thinking of the Chagga” amezungumzia hili namna wachagga hasa wanawake walivyokuwa wanaamini vyombo hivi dhidi ya vile vilitoka kwenye jamii za nje ya Uchagga. Hiyo ilikuwa ni dalili kwamba hata utengenezaji wake ulikuwa ni wa viwango bora na wenye kuaminika na hayo yalichangiwa na uhodari wa ukoo huu.

– Ukoo wa Kweka uliendelea kusambaa katika maeneo mengine ya Uchagga hususan upande wa magharibi ya Uchagga katika himaya za Machame ya mashariki na Machame ya magharibu au Masama.

– Hivyo ukoo wa Kweka unapatikana kuanzia upande wa magharibi kwa uchache katika kijiji cha Lukani, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nkwasira, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyuu, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Losaa, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mashua, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mudio, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mbosho, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mroma, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Lemira, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Saawe, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Isuki, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ng’uni, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mbweera, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboreny, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatika kwa kiasi katika kijiji cha Sonu, Masama.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Uswaa, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Wari Sinde, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nronga, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uduru, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Nshara, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tella, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Orori, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Usari, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mulama, Narumu, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kitongoji cha Kimbushi, Nkuu, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamungo Sinde, Machame.

– Ukoo wa Kweka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamungo Kati, Machame.

– Ukoo wa Kweka inawezekana wanapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Manushi, Kibosho.

Ukoo wa Kweka ni ukoo uliotoa wachagga mashuhuri mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro akiwema Askofu Mkuu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini Dr. Erasto N. Kweka anayetokea katika kijiji cha Uswaa, Machame. Lakini licha ya ukoo huu kuwa na watu wengi wasomi sana lakini bado ni machache yaliyoandikwa na kuwekwa kwenye kumbukumbu juu ya ukoo wa Kweka.

– Ukoo wa Kweka ukiwa pia ni ukoo wa kihistoria kwa moja ya koo mashuhuri katika shughuli za ufinyanzi tunahitaji kupata taarifa nyingi zaidi kuhusu ukoo huu. Taarifa ambazo zitahamasisha mshikamano zaidi miongoni mwa wanaukoo huu na pengine hata kufufua na kuendeleza ujuzi ule muhimu wa zamani. Pia tunahitaji taarifa zaidi kwa ajili ya kuongeza kwenye utafiti unaoendelea.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kweka.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kweka?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kweka?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kweka?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kweka una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kweka wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kweka kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kweka?

9. Wanawake wa ukoo wa Kweka huitwaje?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kweka?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kweka?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kweka?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kweka kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *