UKOO WA OTTARU.

– Ottaru ni ukoo wa wachagga wenye chimbuko lao kwa Uchaggani katika kijiji kinachojulikana kama Otaruni, Kibosho. Hata hivyo ukoo huu wa Ottaru unaonekana ukipatikana kwa wingi zaidi katika kijiji cha Kirima kuliko kwenye chimbuko lao huko Otaruni ambako kuna mchanganyiko wa koo hususan ukoo wa Massawe.

– Kutoka kwenye simulizi za wazee wenyewe wa ukoo wa Ottaru Kibosho kupitia brother Florence James Ottaru ni kwamba ukoo wa Ottaru ulikuwa ni mkubwa na unaopatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Otaruni, Kibosho. Lakini ukoo huu ulikuwa ni ukoo wa wanamapinduzi na watu wenye msimamo mkali ambao walionekana kushindana na utawala wa Mangi Kibosho na kusemekana kwamba walikuwa sehemu ya kupanga njama za kufanya mapinduzi.

– Hivyo kama ilivyokuwa kwa ukoo wa Olotu Mallya taarifa za chini chini za uhaini wa ukoo wa Ottaru dhidi ya utawala wa Mangi zilifika kwa Mangi kupitia mtandao wa mashushushu na hivyo majeshi yakatumwa kwenda kushambulia ngome yao katika kijiji cha Otaruni. Hivyo wachagga wa ukoo wa Ottaru wakashambuliwa vibaya na kupigwa sana baadhi ya waliuawa lakini wengi walifanikiwa kukimbilia katika maeneo ya vijiji mbalimbali Kibosho na hata nje ya Kibosho.

– Baadhi ya waliobaki Kibosho na hasa katika kijiji cha Otaruni walibadilisha majina ya ukoo wengi wakijiita Massawe na wengine hata kuhamia kwenye koo nyingine. Hata hivyo kuna ndugu wengine walikimbilia uhamishoni Arusha na kwenda kuishi huko moja kwa moja lakini walikuja kurudi Kibosho miaka ya baadaye na kuweka makazi ya kudumu katika kijiji cha Kirima, Kibosho. Kwa namna hivyo ukoo wa Ottaru ukawa umetawanyika sana na kupatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Otaruni ambacho kimsingi ndio makazi ya ukoo wa Ottaru.

– Wachagga wa ukoo wa Ottaru kama jinsi walivyokuwa wanaharakati tangu zamani ni watu wanaojituma na wenye bidii kubwa sana katika maisha. Licha ya kwamba sio wengi sana kwa idadi lakini wanafanya vizuri ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya Tanzania katika biashara, ujasiriamali na maeneo mengine katika maisha.

– Ukoo wa Ottaru wameendelea kuongezeka kwa idadi na wanaendelea kuongeza zaidi na hivyo wanapatikana katika vijiji kadhaa Kibosho kuanzia kijiji cha Otaruni kwenye ambapo wanapatikana kwa kiasi.

– Ukoo wa Ottaru wanapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Ottaru wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kirima Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Ottaru wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Singa chini, Kibosho.

– Ukoo wa Ottaru wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uchau, Kibosho.

Kutokana na misukosuko waliopitia ukoo wa Ottaru umegawanyika na kusambaratika sana hivyo kuna changamoto juu ya upatikanaji wa taarifa zake zinazoendana na kuendana na simulizi zake. Kwea maana hiyo tungeomba mchango wa mawazo kuhusu taarifa za ukoo wa Ottaru wenye asili yake katika kijiji cha Otaruni, Kibosho ambacho ndio kilikuwa ngome ya ukoo huu kabla ya kusambaratishwa. Hii itasaidia kuongeza maudhui kuhusu koo za wachagga na zaidi kwa ukoo wenyewe husika wa Ottaru.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Ottaru.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Ottaru?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Ottaru?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Ottaru?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Ottaru una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Ottaru wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Ottaru kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Ottaru?

9. Wanawake wa ukoo wa Ottaru huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Ottaru?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Ottaru?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Ottaru?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Ottaru kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *