UKOO WA MALISA.

– Malisa ni ukoo mkongwe sana na wa wachagga mashuhuri na majasiri sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro. Malisa ni ukoo wa watu wapambanaji na wanaoamini katika kujituma sana na kuishi katika viwango vya juu zaidi vya mafanikio. Ukoo wa Malisa ni ukoo uliotoa watu wengi wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Malisa ambao ngome yao kuu kwa Uchaggani ni katika kijiji cha Kidia, Old Moshi walisifika kwa sifa kuu mbili ambazo hata hivyo hazikupaswa kwenda pamoja bali upekee wao ndio ulipelekea sifa hizi mbili kwenda pamoja. Sifa ya kwanza ya ukoo wa Malisa kama ilivyokuwa kwa ukoo wa Makundi walikuwa ni wachagga mahiri na hodari sana kwa shughuli za uhunzi au kufua vyuma. Hivyo ukoo wa Malisa walikuwa ni watengenezaji wa vifaa mbalimbali kwa kutumia zana za chuma na hususan silaha za kivita. Silaha nyingi zilizokuwa zinauzwa ndani na nje ya Uchaggani zilizotengenezwa na koo mbalimbali za kichagga zilitengenezwa kwa wingi sana pia na wachagga wa ukoo wa Malisa.

– Pili mbali na kutengeneza silaha za kivita kwa wingi ukoo wa Malisa pia walitoa askari hodari sana kwa mapigano vitani. Hii ilikuwa ni tofauti na desturi za Uchagga ambapo ziliruhusu zile koo zinazotengeza silaha kutokwenda kabisa vitani na kuwekeza nguvu na akili katika kutengeneza silaha pekee. Lakini wachagga wa ukoo wa Malisa waliokuwa na uthubutu na ujasiri sana waliona hawawezi kuwa mashujaa wala kupata heshima katika jamii ya wachagga bila kwenda vitani na kupigana kwani walipenda sana vita na mapambano pia. Hili lilichangiwa pia na himaya ya umangi Old Moshi wanakopatikana ukoo huu kwa wingi zaidi ambapo watu wake walikuwa wanapenda sana vita na hivyo watu hususan wanaume wasioenda vitani walionekana kama ni waoga na walidharauliwa sana Old Moshi.

– Hivyo wachagga wa ukoo wa Malisa tofauti na koo nyingine za wafua vyuma Uchaggani walitengeneza silaha kwa wingi sana ambazo ziliuzwa mpaka umasaini na kwingineko, lakini bado na vitani walienda pia. Ari hii ya upambanaji imeendelea kuonekana katika jamii ya wachagga wa ukoo wa Malisa mpaka leo ambapo wengi wamekuwa ni watu wa kujituma sana, waliopiga hatua kubwa maendeleo na wanaoheshimika sana katika maeneo yao.

– Ukoo wa Malisa umeendelea kukua na kuongezeka sana na kusambaa katika vijiji vingi mbalimbali vya Uchaggani magharibi na mashariki ya himaya ya umangi Old Moshi ambayo ndio chimbuko lao kwa Uchaggani, Kilimanjaro.

– Hivyo ukoo wa Malisa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Okaseni, Uru.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mnini, Uru.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shimbwe chini, Uru.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shimbwe Juu, Uru.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shimbwe kati, Uru.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shia, Old Moshi.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa wingi pia katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyou, Kilema.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyasomboro, Marangu.

– Ukoo wa Malisa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.

Licha ya mambo makubwa kihistoria ambayo ukoo wa Malisa wamefanya katika historia ya wachagga Kilimanjaro bado ni machache sana yanafahamika. Historia kubwa ya kishujaa ya ukoo huu inaendelea kupotea kwa vizazi vya zamani kuendelea kupotea hivyo tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu ukoo huu. Tunahitaji mchango wa mawazo zaidi ili kuhifadhi maudhui ya ukoo wa Malisa sambamba na nyingine za Uchagga kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Malisa.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Malisa?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Malisa?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Malisa?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Malisa una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Malisa wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Malisa kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Malisa?

9. Wanawake wa ukoo wa Malisa huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Malisa?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Malisa?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Malisa?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Malisa kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *