BONIFACE PAULO MASSAWE.

– Boniface Paulo Massawe ni mchagga kutokea Kibosho ambaye haijulikana exactly anatokea kijiji gani. Lakini Bwana huyu alizaa mtoto na mwanamke mmoja kutokea huko Marangu miaka kama 35 au 36 iliyopita alipokuwa akiishi Moshi mjini. Mtoto huyo ni wa kike na ameshakuwa binti mkubwa ambaye ameolewa na mwanaume wa huko huko Marangu na ana familia yake.

– Kwa bahati mbaya mama yake na huyu binti alifariki binti akiwa na umri kama wa miaka 4 hivi akiwa hajaweka wazi taarifa za kutosha kuhusu namna ya kumpata mwanaume aliyezaa naye baada ya kuondoka Moshi mjini na kurudi huko kwao Marangu. Binti amelelewa upande wa wajomba zake akiwa hajui kabisa ndugu zake upande wa baba mzazi wala hajui kama baba huyo bado yupo hai au la. Binti amekuwa na shauku yake ya kufahamu upande wa baba yake mzazi imekuwa kubwa.

– Tuliongea nikajaribu kumwambia japo ukoo wa Massawe huko Kibosho ni mkubwa sana na upo karibu kila kijiji Kibosho tena kwa wingi sana na yeye ana taarifa chache sana za huo upande wa baba mzazi lakini tujaribu kufuatilia huenda tukafanikiwa kumpata. Hivyo tunahitaji taarifa za kutoka sehemu yoyote Kibosho yenye ukoo wa Massawe ambapo kuna Mzee Paulo Massawe ambaye ana mtoto anayeitwa Boniface Massawe aliyewahi kuzaa na mwanamke kutoka Marangu lakini wakaachana na mwanamke huyo kurudi kwao.

– Mwanamke yule hakukaa muda mrefu kabla ya kufariki lakini hakuna uhakika kama huyo Boniface mwenyewe hata anajua kwamba mwanamke yule alifariki miaka michache baadaye. Huyo Boniface ni mtu mzima aliyezaliwa kwenye miaka ya mwanzoni mwa 1950’s au kabla ya hapo hivyo huyo baba yake Mzee Paulo Massawe huenda alizaliwa kwenye miaka ya 1930’s au 1920’s au kabla ya hapo.

– Muhimu ni kupata taarifa za mtu anayeitwa Paulo Massawe au Boniface Paulo Massawe wa Kibosho kisha akijulikana au ndugu zake kujulikana waweze kuwasiliana na binti huyu ndugu yao. Taarifa zaidi ni kwamba mama wa huyo Boniface Paulo Massawe yaani mke wa Mzee Paulo Massawe alikuwa anajulikana kwa jina moja la Mage. Karibu kwa maoni na kama kuna yeyote mwenye mawasiliano au mwenye taarifa zaidi tuwasiliane.

Ahsanteni.

Karibu kwa michango zaidi ya mawazo.

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *