UKOO WA KANZA.

– Kanza ni ukoo usio maarufu sana unaopatikana kwa wingi katika vijiji vya maeneo ya katikati ya Kilimanjaro. Huu ni ukoo wa watu wenye umakini mkubwa na wengi wanafanya vizuri sana katika taaluma maeneo mbalimbali na diplomasia na hata katika biashara.

– Kutoka kwenye historia Kanza ni ukoo uliokuwa mashuhuri na uliokuwa unatawala katika kijiji cha Sango, Old Moshi. Ukoo huu wa Kanza kuna baadhi ya taarifa za kihistoria zinauhusisha kuwa na mahusiano ya karibu na ukoo wa Nyange unaopatikana maeneo ya Old Moshi na Mamba. Ukoo huu wa Kanza umekuwa ni ukoo wenye nguvu na uliotawala katika kijiji cha Sango, Old Moshi katika kipindi cha karne kadhaa zilizopita na baadaye kuwa moja kati ya koo zenye nguvu zilizokuwa zinatoa wachili wa kijiji na wasaidizi wa Mangi.

– Ukoo wa Kanza japo haukusambaa sana lakini uliweza kutanuka zaidi na kupatikana katika vijiji vingine kadhaa maeneo mengine ya Uchaggani, Kilimanjaro.

– Hivyo ukoo wa Kanza unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Kanza unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Kanza unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Yamu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Kanza unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

Bado kuna taarifa chache sana kuhusiana na ukoo wa Kanza na jinsi wanavyohusiana na koo nyingine. Pia kuna watu wengi wa ukoo wa Kanza wanaofanya vizuri sana maeneo mbalimbali. Tunahitaji taarifa zaidi kuhusiana na ukoo wa Kanza ili kuongeza kwenye utafiti unaoendelea na kukuza sana maudhui ya koo na tamaduni za wachagga kwa ujumla ili kujenga uelewa mkubwa kwa kizazi cha sasa na vingine vinavyofuatia. Hii itasaidi kujenga hamasa na mshikamano zaidi kwa jamii ya wachagga kuelekea kufanya makubwa katika maisha kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kanza.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kanza?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kanza?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kanza?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kanza una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kanza wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kanza kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kanza?

9. Wanawake wa ukoo wa Kanza huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kanza?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kanza?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kanza?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kanza kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *