UKOO WA MEELA.

– Meela ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana kwa wingi maeneo ya Uchaggani kati kuelekea mashariki. Huu ni ukoo uliosambaa katika vijiji mbalimbali vya maeneo haya. Hata hivyo japo sio ukoo uliosambaa maeneo mengi sana lakini ukoo wa Meela ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri wanaofanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kihistoria ukoo wa Meela ni ukoo uliojikita zaidi katika himaya ya umangi Marangu upande wa kaskazini katika eneo ambalo leo hii ni kata ya Marangu magharibi. Ukoo huu uliokuwa mashuhuri sana eneo hili kiasi kwamba umeweza kuchukua mpaka jina la kijiji ambacho kuna koo nyingine ziko kwa wingi zaidi kinachoitwa kijiji cha Komela, Marangu. Kijiji hiki cha Komela na vijiji vingine vya jirani ukoo huu unapatikana kwa wingi sana.

– Ukoo huu wa Meela umeendelea kusambaa zaidi maeneo hayo kuelekea mashariki na magharibi na hivyo unapatikana katika vijiji vinavyozunguka maeneo hayo.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nduweni, Marangu.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Komela, Marangu.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mmbahe, Marangu.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Lyasomboro, Marangu.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Arisi, Marangu.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Rauya, Marangu.

– Ukoo wa Meela unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.

Kuna uhitaji mkubwa taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Meela wenye wasomi wengi mbalimbali ndani na nje ya nchi. Maudhui ya ukoo wa Meela yataongeza kwenye stoo ya maudhui ya wachagga kwa ujumla na kusaidia kujenga mashikamano zaidi baina ya wanaukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla kuelekea kuwa jamii bora na inayojitambua kwa viwango vya juu. Kujitambua huko ni sehemu muhimu ya maendeleo tunayoyapigania usiku na mchana.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Meela.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Meela?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Meela?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Meela?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Meela una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Meela wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Meela kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Meela?

9. Wanawake wa ukoo wa Meela huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Meela?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Meela?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Meela?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Meela kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *