UKOO WA SHAO.

– Shao ni mkubwa wa wachagga wanaopatikana katika ukanda wa mwishoni mwa mashariki ya kati na mashariki zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro. Baadhi ya watu huwa hawawezi kuutofautisha ukoo wa “Shao” na ukoo mwingine maarufu wa “Shayo”. Hata hivyo baadhi ya watu wa ukoo wa Shao wanaamini kwamba wao ni ukoo mmoja na Shayo na wengine hata kujiita kwa ukoo huo.

– Lakini kwa ukanda huo mwishoni mwa mashariki ya kati na mashariki zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro kuna vijiji vingi ambavyo koo zote mbili za “Shao” na “Shayo” zinapatikana na zinaishi sambamba. Hata hivyo licha ya ukoo wa “Shayo” kuwa mkubwa sana lakini hata ukoo wa “Shao” nao ni mkubwa kwa upande wa mashariki na wenye watu wengi.

– Ukoo wa Shao ni ukoo uliotoa watu wengi mashuhuri na watu wengine wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali kuanzia biashara na ujasiriamali mpaka kwenye taasisi mbalimbali za umma na mashirika binafsi. Kati ya watu maarufu waliowahi kutokea kwenye ukoo wa Shao ni pamoja na aliyewahi kuwa Askofu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Martin F. Shao kutoka katika kijiji cha Lole, Mwika na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Rombo Mh. Joseph Selasini Shao.

– Ukoo wa Shao umesambaa katika vijiji vingi vya mashariki ya kati kuelekea mashariki zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro wakipatikana kwa wingi kwa baadhi ya vijiji na kwa uchache kwa vijiji vingine.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Msae Nganyeni, Mwika.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msae Kinyamvuo, Mwika.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Lole Marera, Mwika.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Lole, Mwika.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Maring’a, Mwika.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Uuwo, Mwika. Sehemu kubwa sana ya kijiji cha Uuwo, Mwika imetawaliwa na ukoo wa Shao.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirimeni, Mwika.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mawanjeni, Mwika.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mahango, Mahida, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Nguduni, Mahida, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mamsera Juu, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mamsera Kati, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mamsera Chini, Mamsera, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Ngoyoni, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Ngareni, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Manda Juu, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Mengeni Chini, Keni, Rombo. Ukoo wa Shao uko kwa wingi sana katika kijiji cha Mengeni Chini.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Mengeni Kitasha, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Machame Aleni, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Aleni Chini, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Shimbi Mashami, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Shao unapatikana kwa kiasi katika vitongoji vya kata ya Kelamfua, Mkuu, Rombo.

Tunahitaji kupata taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Shao unaopatikana kwa wingi sana maeneo ya mashariki ya Kilimanjaro. Tunaomba mchango zaidi wa mawazo kuhusiana ukoo huu tuweze pia kuongeza kwenye maktaba ya maudhui ya koo za Wachagga, Kilimanjaro.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Shao.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Shao?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Shao?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Shao?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Shao una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Shao wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Shao kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Shao?

9. Wanawake wa ukoo wa Shao huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Shao?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Shao?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Shao?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Shao kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *