UKOO WA CHAMI

– Chami ni ukoo mkubwa wa wachagga wanaopatikana upande wa magharibi ya kati kuelekea magharibi zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Chami ni kati ya koo ambazo kihistoria ziliweza kutoa watu hodari na mashuhuri katika utaalamu wa ufinyanzi na wafanyabiashara wa bidhaa za ufinyanzi hususan vyombo vya nyumbani. – Vyombo vingi vya nyumbani vilivyotengenezwa na …

UKOO WA SHAO.

– Shao ni mkubwa wa wachagga wanaopatikana katika ukanda wa mwishoni mwa mashariki ya kati na mashariki zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro. Baadhi ya watu huwa hawawezi kuutofautisha ukoo wa “Shao” na ukoo mwingine maarufu wa “Shayo”. Hata hivyo baadhi ya watu wa ukoo wa Shao wanaamini kwamba wao ni ukoo mmoja na Shayo na wengine …

UKOO WA MUNISHI.

– Munishi ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Munishi ni ukoo mkubwa wenye watu wengi lakini pia wenye utata fulani nyuma yake kutokana na kuhusianishwa na koo nyingine za kichagga zinazoshabihiana nao kwa majina. – Kuna dhana inayoaminika kwamba kuna uhusiana wa …

UKOO WA MURO.

– Muro ni ukoo wa wachagga wanaopatikana upande wa magharibi zaidi ya Uchagga, Kilimanjaro. Japo majina ya Muro yamepata kuonekana Uchaggani katika nyakati tofauti tofauti kwenye koo mbalimbali lakini ukoo wa Muro unasemekana kuwa ni tawi la ukoo mkubwa wa Mboro uliosambaa uchaggani kote. – Watu mbalimbali mashuhuri waliowahi kufahamika sana katika historia ya wachagga …

UKOO WA MATERU.

– Materu ni ukoo maarufu wa wachagga unapatikana kwa wingi zaidi eneo la katikati ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Materu kwa sehemu wamekuwa ni watu wenye haiba ya kupenda dini na maridhiano. Chimbuko la ukoo wa Materu kwa maeneo ya Uchaggani, Kilimanjaro linaweza kuwa ni eneo la Uru mashariki ambapo ukoo wa Materu …

UKOO WA MWACHA.

– Mwacha ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi maeneo ya magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Mwacha umekuwa ni ukoo wa watu wajasiri sana kama ilivyo kwa koo nyingi za eneo hilo na pia una watu wengi wanaofanya vizuri sana katika shughuli za biashara na ujasiriamali ndani na nje ya …

UKOO WA MMBANDO.

– Mmbando ni ukoo mkubwa wa wachagga unaopatikana kwa wingi zaidi upande wa mashariki ya kati kuelekea mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Mmbando ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri na wanaofanya vizuri katika biashara, taaluma na hata uongozi. – Ukoo wa Mmbando umeendelea kusambaa na kuongezekana sana idadi kwenye maeneo mapya walikohamia kutoka kwenye …

UKOO WA MACHANGE.

– Machange ni ukoo wa wachagga ulioeneo maeneo ya katikati ya Uchagga, Kilimanjaro kwa kiasi na maeneo ya mashariki ya kati ya Uchagga kwa wingi kiasi. Ukoo wa Machange ni ukoo wenye watu wengi wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali kimaisha kuanzia kuanzia biashara, ujasiriamali, taaluma na hata kwenye taasisi mbalimbali binafsi na za umma ndani …

UKOO WA MMASI.

– Mmasi ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi upande wa magharibi ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Mmasi wamesambaa maeneo ya vijiji vingi vya eneo la magharibi ya kati ya Uchagga Kilimanjaro hususan upande wa magharibi katika maeneo zilipokuwepo himaya za umangi Kibosho na Kindi. – Kutoka kwenye historia …