– Mwanga ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa magharibi ya kati kuelekea magharibi ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro kwa wingi katika baadhi ya vijiji na kwa uchache katika vijiji vingine. Baadhi ya wachagga wa ukoo wa Mwanga ni watu wenye uwezo mkubwa sana kiakili na waliojaliwa vipaji vikubwa katika taaluma na ujasiriamali. Inafahamika kwamba hata ukoo mdogo wa Mengi unaopatikana kwa uchache katika kijiji cha Nkuu Sinde, Machame ni tawi la ukoo wa Mwanga.
– Wachagga wa ukoo wa Mwanga wanafanya vizuri sana katika taasisi mbalimbali kitaaluma ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Mchagga mashuhuri zaidi kutokea kwenye ukoo huu wa Mwanga ni aliyekuwa mfanyabiashara mashuhuri na bilionea Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi. Dr. Reginald Abrahamu Mengi kutoka katika ukoo huu Mwanga ameweka historia ya kuwa kati ya watu wachache sana hapa Afrika mashariki walioweza kujenga utajiri mkubwa sana.
– Licha ya kwamba takwimu za forbes zinaonyesha kuwa utajiri wa Dr. Reginald Mengi ulifikia juu kidogo ya nusu bilioni moja za kimarekani lakini Reginald Mengi mwenyewe aliwahi kukiri kwamba sehemu kubwa ya utajiri wake haijarekodiwa au kusema haipo kwenye taasisi ya mashirika haya. Hiyo ni kusema kwamba utajiri wa Reginald Mengi uliweza kufikia zaidi ya dola bilioni za kimarekani na kumfanya kuwa mchagga pekee aliyefikia kiwango cha ubilionea. Lakini hii pia inamfanya Dr. Reginald Mengi kutoka kwenye ukoo huu wa Mwanga kuwa ndiye mwafrika mzawa mweusi pekee hapa Afrika mashariki aliyefanikiwa kufikiwa kiwango cha ubilionea wa dola kupitia biashara na ujasiriamali.
– Dr. Reginald Mengi kutoka kwenye ukoo wa Mwanga pia ndiye mtanzania aliyejaribu kuthubutu kupingana na hata kukosoa itikadi na sera za mrengo wa kushoto za awamu ya kwanza katika nyakati ambapo bado haikuwa salama sana kufanya hivyo na hilo lilikaribia kumgharibu utajiri wake katika miaka ya mwanzoni. Hata hivyo kupitia imani na msimamo wake katika sekta binafsi na uchumi huria Dr. Reginald Mengi kwa ushirikiano wa karibu na serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa Tanzania alikuwa ndiye mtu aliyepambania sekta binafsi kwa nguvu zaidi na kufanikiwa kutengeneza mahusiano bora sana kati ya sekta binafsi na serikali na hata kuunda mamlaka mbalimbali zilizosaidia katika eneo hilo kama vile PPP n.k.,
– Harakati zake hizi pamoja na nyingine nyingi sana katika maeneo aliyowekeza na aliyokuwa anatoa misaada yamesaidia katika kukuza sana na kuimarisha sana uchumi wa nchi. Juhudi zake hizi zilitambuliwa pia na Rais Mkapa katika nyakati tofauti tofauti. Maeneo mengine aliyoyapigania sana ni pamoja na mazingira, demokrasia, uhuru wa habari n.k., Mchagga mwingine mashuhuri kutoka kwenye ukoo huu Mwanga ni Mr. Elitira Mengi kaka yake na Dr. Reginald Mengi aliyejenga utajiri mkubwa pia miaka ya zamani zaidi kabla ya mali zake kutaifishwa na serikali ya awamu ya kwanza.
– Ukoo wa Mwanga umesambaa Uchaggani kwa uchache katika ukanda wa magharibi ya karibu na kwa wingi katika ukanda wa magharibi ya kati kuelekea magharibi ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro.
– Hivyo ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mbosho, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lemira, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Ng’uni, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Roo, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mudio, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mbweera, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mboreny, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Ngira, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Sonu, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kware, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mungushi, Masama.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Uswaa, Machame.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shari/Uraa, Machame.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Foo, Machame hususan katika kitongoji cha Nkweseko.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nshara, Machame.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Nkuu Sinde, Machame.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Lyamungo Kilanya, Machame.
– Ukoo wa Mwanga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Singa, Kibosho.
Pamoja na ukoo huu kujulikana sana upande wa magharibi ya Uchagga, Kilimanjaro bado kuna taarifa chache sana juu ya ukoo huu, chimbuko lake na namna ulivyosambaa. Tunahitaji kupata taarifa zaidi juu ya ukoo huu ili tuweze kuongeza maudhui mengi zaidi katika maktaba zote kwa manufaa ya sasa na uzao wa baadaye. Hii ni moja kati ya njia sahihi za kujenga hamasa, mshikamano na ari ya kuelekea kufanya makubwa katika ngazi ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Mwanga.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mwanga?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mwanga?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mwanga?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mwanga una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Mwanga wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mwanga kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mwanga?
9. Wanawake wa ukoo wa Mwanga huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mwanga?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mwanga?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mwanga?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mwanga kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
Email: urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp +255 754 584 270.