UKOO WA KITALI.

– Kitali ni ukoo wa wachagga unaopatikana kwa kiasi katika maeneo ya mashariki ya karibu, mashariki ya kati na mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kitali wamesambaa kwa kiasi katika baadhi ya vijiji lakini vinavyopatikana mbalimbali sana kuelekea upande wa mashariki ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Kitali wanafanya shughuli mbalimbali za ujasirimali na katika taasisi za serikali, binafsi na hata mashirika ya kimataifa ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.

– Kutoka kwenye historia Kitali ni moja kati ya koo zilizokuwa na umashuhuri na ziliheshimiwa na watawala kwani zilitoa watu makini na viongozi wa ngazi mbalimbali katika maeneo yao. Moja kati ya watu mashuhuri aliyewahi kutoka kwenye ukoo huu wa Kitali ni Mr. Jackson Kitali aliyegombea kiti cha umangi Mkuu wa wachagga akitokea katika kijiji cha Tella, Old Moshi katika uchaguzi ambao Thomas Marealle kutokea Marangu alishinda na kukalia kiti hicho.

– Mr. Jackson Kitali akiwa bado ni kijana wa umri wa miaka 28 peke yake alikuwa ni mgombea ambaye hakuweza kujenga ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa Mangi Mkuu wa wachagga uliokuwa na ushindani mkali hivyo hakutoa upinzani mkali kama wagombea wengine. Baadaye baada ya TANU kupewa madaraka ya kuongoza nchi kutoka kwa Waingereza Bwana Jackson Kitali alijiunga na chama hicho na kujenga ushawishi kiasi cha kuweza kuwa Mwenyekiti wa chama wilaya. Alikuja kufariki mwaka 2002 na kuzikwa kijijini kwao Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Kitali ambao kimsingi ni ukoo mdogo umeendelea kukua na kuongezeka na kusambaa zaidi katika maeneo ya vijiji mbalimbali hususan kuelekea mashariki.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kitandu, Uru.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Tella, Old Moshi.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kitowo, Marangu.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kyala, Marangu.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Manda chini, Mengwe, Rombo.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mengeni Kitasha, Keni, Rombo.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shimbi Masho, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Kitali unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Maharo, Mkuu, Rombo.

Karibu kwa Mchango wa Mawazo zaidi kuhusiana na ukoo wa Kitali ambao hausikiki sana lakini una mambo makubwa. Karibu kwa pamoja tuweze kuongeza maudhui zaidi kwenye maktaba ya ukoo wa Kitali pamoja ulioenea zaidi katika ya Uchagga kuelekea mashariki ya mbali ili kusaidia katika kujenga hali ya kujitambua na kujenga kujiamini zaidi kuelekea kufanikisha makubwa. Maudhui haya yatachangia katika kuongeza zaidi kwenye taarifa za kitafiti na kujifahamu zaidi wachagga kwa ujumla kama jamii.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Kitali.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Kitali?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Kitali?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Kitali?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Kitali una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Kitali wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Kitali kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Kitali?

9. Wanawake wa ukoo wa Kitali huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Kitali?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Kitali?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Kitali?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Kitali kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *