– Lyamuya ni ukoo maarufu wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Lyamuya una watu wengi waliosambaa maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro wakifanya vizuri katika shughuli za biashara na ujasiriamali. Ukoo wa Lyamuya pia una watu wengi wanaofanya kazi katika taasisi na mashirika ya umma na binafsi na hata katika taasisi na mashirika ya kimataifa.
– Kutoka kwenye historia ukoo wa Lyamuya unasemekana ni moja kati ya matawi mengi sana yaliyotokea kwenye ukoo mkubwa wa Mboro uliovunjika na kutengeneza matawi madogo madogo mengi sana ya koo zilizosambaa Uchaggani kote, Kilimanjaro kutokea magharibi kabisa mpaka mashariki ya mbali. Hata hivyo nadharia hii iko katika hali ya utata zaidi ambapo unahitajika utafiti kina zaidi kuweza kufahamu kwa undani wale halisia na wale ambao tayari walikuwa na ukoo husika kwa baadhi ya koo zinazoaminiwa hivyo.
– Hata hivyo nadharia hii ya chimbuko la ukoo wa Lyamuya inaongezewa nguvu zaidi na uwepo wa ukoo huu kwa wingi katika eneo lililokuwa eneo la asili la ukoo wa Mboro katika vijiji vya Lyamrakana na Sembeti, Marangu.
– Ukoo wa Lyamuya umesambaa zaidi katika ukanda huo huo wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro na unapatikana kwa wingi sana kwa baadhi ya vijiji na kwa uchache kwenye vijiji vingine.
– Ukoo wa Lyamuya unapatika kwa kiasi katika kijiji cha Mrawi, Uru.
– Ukoo wa Lyamuya unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kitandu, Uru.
– Ukoo wa Lyamuya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kyou, Kilema.
– Ukoo wa Lyamuya unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Ruwa, Kilema.
– Ukoo wa Lyamuya unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.
– Ukoo wa Lyamuya unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.
– Ukoo wa Lyamuya unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Sembeti, Marangu.
– Ukoo wa Lyamuya unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Masia, Marangu.
Tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu ukoo wa Lyamuya, kwa sababu licha ya taarifa hizo kiasi tulizoweza kupata kuhusu ukoo wa Lyamuya bado kuna mengi sana bado hatujaweza kufahamu kuhusu ukoo huu. Maudhui haya tunayojaribu kukusanya yanalenga kuelimisha sambamba na kujenga hamasa ya watu wa ukoo husika na jamii nzima ya wachagga kuamka na kujaribu kujitafuta ili iwe chachu ya kujenga mshikamano katika kuhamasisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Tunategemea hili liweze kwenda sambamba na kuendeleza na kutunza tamaduni bora za kichagga zilizoweza kutuletea ufahari na zinazoweza kuendelea kuifanya jamii hii kuwa bora zaidi na zaidi.
Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Lyamuya.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Lyamuya?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Lyamuya?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Lyamuya?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Lyamuya una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Lyamuya wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Lyamuya kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Lyamuya?
9. Wanawake wa ukoo wa Lyamuya huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Lyamuya?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Lyamuya?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Lyamuya?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Lyamuya kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp +255 754 584 270