UKOO WA MARANDU.

– Marandu ni ukoo maarufu wa kichagga unaopatikana kwa kiasi katika ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga na kwa wingi zaidi katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Marandu ukiwa ni ukoo mkongwe wenye watu katika tasnia mbalimbali hususan biashara na ujasiriamali ni ukoo pia uliotoa na unaoendelea kutoa watu mbalimbali mashuhuri walioacha alama kubwa katika historia ya wachagga, Kilimanjaro tangu zamani mpaka sasa.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Marandu ni ukoo unaopatikana zaidi maeneo ya katikati ya ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro katika eneo ambalo lilikuja kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi katikati ya karne ya 20. Ukoo wa Marandu ni ukoo pia unaohusishwa na kuwa na watu wengi wajasiri na wenye uthubutu wa kufanya mambo makubwa katika maisha. Hata hivyo mwishoni mwa karne ya 19 ukoo wa Marandu ni moja kati ya koo zilizowahi kupitia tukio kubwa la uonevu lililoacha kumbukumbu ya kusikitisha.

– Ukiwa umetoa watu mbalimbali mashuhuri mmoja kati wachaggga maarufu sana katika historia anayetokea kwenye ukoo wa Marandu ni aliyekuwa Mangi Mwitori wa jimbo la Rombo, Uchagga Mangi John Ndaskoi Maruma Marandu ambaye pia alijaribu kugombea kiti cha umangi mkuu wa wachagga mwaka 1951 bila mafanikio. Mangi John Ndaskoi Maruma Marandu aliyekuja kuweka makazi yake katika eneo la KirwaKeni ambalo leo hii karibu na KNCU Kirwakeni chimbuko lake ni kutoka katika iliyokuwa himaya ndogo ya umangi Kerio ambapo huenda ndio chimbuko la ukoo huu.

– Mangi John Ndaskoi Maruma Marandu ambaye anasemekana kwamba katika utoto wake alilelewa huko Vunjo, Marangu na kukuza katika dini ya kilutheri tofauti na wachagga wengi wa ukanda wa mashariki ya mbali ambao ni wakatoliki zaidi, baada ya kukua na kuwa amesoma alirudi kugombea kiti cha utawala katika eneo la Rombo. Hata hivyo pamoja na kwamba ni wa ukoo wa Marandu na asili yake ni Rombo kuna watu walijaribu kumpiga vita kutokana na kulelewa kilutheri huko Vunjo na kumhusisha kwamba sio mwenyeji wa Rombo, lakini kutokana na elimu kubwa aliyokuwa nayo iliyomwezesha kujenga ushawishi mkubwa kwa watu wengi hususan wenye mamlaka aliweza kukubalika sana.

– Mwaka 1955 Mangi John Ndaskoi Maruma Marandu alifanikiwa kukalia kiti cha umangi mwitori wa jimbo la Rombo, Uchagga kilichokuwa kinakaliwa na Mangi Edward Latemba wa himaya ya umangi Mashati. Mangi John Ndaskoi Maruma Marandu kwa kukalia kiti hicho cha umangi aliweza kuleta mapinduzi makubwa kiuchumi na hata kiutawala katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro hususan katika eneo la Mashati, Rombo ambalo mwanzoni lilichukulia kama eneo lilirudi nyuma zaidi kimaendeleo ukilinganisha na himaya nyingine za ukanda huo.

– Kupitia mapinduzi makubwa ya kilimo cha kahawa ambacho mwanzoni hakikuwa na mafanikio makubwa sana katika eneo la Rombo, chini ya utawala wa Mangi John Ndaskoi Marandu ambaye alipigania sana hata sheria za ardhi Rombo na hususan Mashati ilipiga hatua kubwa. Ukoo huu wa Marandu umeendelea kukua na kusambaa zaidi katika vijiji na maeneo mengine ya Uchagga, Kilimanjaro lakini zaidi katika ukanda wa mashariki ya mbali ambapo unapatikana kwa wingi zaidi.

– Kupitia kusambaa huko ukoo wa Marandu umeendelea kusambaa katika vijiji zaidi na upatikana kuanzia ukanda wa mashariki ya kati katika vijiji vya eneo la Vunjo kwa kiasi.

– Hivyo ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Lyamrakana, Marangu.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ubaa, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ushiri, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kerio, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Keni, KirwaKeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kirua, Kirwakeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiraeni, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mrere, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Katangara, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mahorosha, Mashati, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kirongo Chini, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kahe, Usseri, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Nayeme, Tarakea, Rombo.

– Ukoo wa Marandu unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kikelelwa, Tarakea, Rombo.

Pamoja na taarifa kiasi tulizofanikiwa kukusanya kuhusu ukoo wa Marandu bado kuna mengi sana yasiyojulikana kuhusu ukoo huu maarufu. Tunahitaji mchango zaidi wa mawazo kutoka kwenu kuhusiana na ukoo wa Marandu ili tuweze kuongeza katika maktaba ya ukoo huu sambamba na koo za kichagga kwa ujumla. Maudhui haya ya ukoo wa Marandu yanaenda kuingia kwenye maktaba za mtandaoni na baadaye yatapokuwa yameboreshwa kuwekwa kwenye nakala ngumu na kuingia kwenye maktaba za kawaida. Lengo ni kujenga hamasa na kuamsha ari ya kufahamu zaidi kuhusu koo na asili zetu katika kuimarisha umoja na mshikamano kuelekea kufanya mambo mengi zaidi muhimu na makubwa.

Karibu kwa mchango zaidi wa Mawazo kuhusu ukoo wa Marandu.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Marandu?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Marandu?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Marandu?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Marandu una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Marandu wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Marandu kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Marandu?

9. Wanawake wa ukoo wa Lyamuya huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Marandu?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Marandu?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Marandu?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Marandu kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *