– Uisso ni ukoo mkubwa wa kichagga unaopatikana kwa wingi katika maeneo ya ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro na kwa wingi zaidi katika eneo la ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wa watu wajasiri na wenye kujiamini sana katika mapambano ya aina yoyote ile. Ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso ni ukoo wenye watu wengi wajasiriamali na wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi.
– Kutoka kwenye historia ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso ni ukoo uliowahi kutoa watu wengi mashuhuri tangu zamani mpaka sasa. Katika eneo la himaya ndogo ya umangi Katangara katika eneo la Mashati, Rombo na katika baadaye kwa eneo lote la himaya ya umangi Mashati ambali awali lilijulikana zaidi kama “Mkulia” ukoo wa Uisso ndio ulitoa watawala wa eneo hili.
– Watawala wa mwisho waliojulikana zaidi katika eneo hili la Mkulia au Mashati, Rombo kutokea katika ukoo wa Uisso ni Mangi Latemba wa Katangara na mtoto wake Mangi Edward Katemba Uisso aliyekuja kuwa mtawala wa mwisho wa eneo lote la Mashati, Rombo. Mangi Edward Latemba ndiye mtawala wa mwisho aliyekuja kuwa na ushawishi zaidi katika himaya ya umangi Mashati katika jimbo la Rombo, Uchagga.
– Baada ya hapo ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso umeendelea kutoa kutoa watu mbalimbali mashuhuri na wanaofanya vizuri katika maeneo mengi ya maisha. Ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso umeendelea kusambaa na kuongezeka sana na unapatikana katika maeneo ya vijiji mbalimbali katika Uchagga, Kilimanjaro hususan katika ukanda wote wa mashariki ya katika na zaidi ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Samanga, Marangu.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mshiri, Marangu.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa kiasi katika kijiji chaMasia-Marangu.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kotela, Mamba.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Komakundi, Mamba.
– Ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kondeni, Mwika.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mrimbo Uuwo hususan katika kitongoji cha Kirimeni, Mwika.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mawanjeni, Mwika.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Matala, Mwika.
– Ukoo wa Woisso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mahango, Mahida, Rombo.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mamsera Kati, Mamsera, Rombo.
– Ukoo wa Woisso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Shimbi Masho, Shimbi, Mkuu, Rombo.
– Ukoo wa Woisso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Shimbi Mashami, Shimbi, Mkuu, Rombo.
– Ukoo wa Woisso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shimbi Kati, Shimbi, Mkuu, Rombo.
– Ukoo wa Woisso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Shimbi Mashariki, Shimbi, Mkuu, Rombo.
– Ukoo wa Woisso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.
– Ukoo wa Woisso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mrao, Mashati, Rombo.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kirua-Rombo, Mashati.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Katangara, Mashati, Rombo.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Msaranga, Mashati, Rombo.
– Ukoo wa Uisso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kitowo, Olele, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kingachi, Usseri, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kiwanda, Usseri, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kwalakamu, Usseri, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Ubetu, Usseri, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Ngasseni, Usseri, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kahe, Usseri, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msangai, Tarakea, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana katika kijiji cha Reha/Urauri, Tarakea, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nessae, Tarakea, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kibaoni, Tarakea, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nayeme, Tarakea, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mbomai, Tarakea, Rombo.
– Ukoo wa Oisso unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kikelelwa, Tarakea, Rombo.
Ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso ni ukoo wenye historia kubwa lakini kuna mengi sana hayajulikana kuhusu ukoo huu kuanzia namna ulivyogawanyika na kusambaa. Tunahitaji kupata taarifa zaidi za aina yoyote juu ya ukoo huu mkubwa, maarufu na mashuhuri pia. Tunahitaji kuongeza maudhui mengi kadiri inavyowezekana kwenye maktaba ya ukoo huu pamoja na koo za kichagga kwa ujumla. Kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye katika kuwajengea mshikamano na hamasa kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha na kujenga jamii bora tunahitaji sana kukusanya na kutunza kumbukumbu hizi ambazo zinakwenda kuongeza uelewa wa jamii ya wachagga na thamani yake miongoni mwa jamii zenye kujitambua duniani.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Uisso/Oisso/Woisso wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso?
9. Wanawake wa ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Uisso/Oisso/Woisso?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Uisso/Oisso/Woisso kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp +255 754 584 270.