– Rimoy ni ukoo wa wachagga wanaopatikana kwa wingi zaidi katika eneo la himaya ya umangi Kilema. Huu ni ukoo ambao sio mkubwa sana wala maarufu sana lakini ni ukoo wa watu mashuhuri wanaofanya vizuri sana kwenye masuala ya biashara na ujasiriamali. Ukoo wa Rimoy ni ukoo wa watu wenye kujiamini na wengi wenye hadhi fulani katika jamii.
– Bado hatuna taarifa za kutosha sana juu ya kama ukoo huu umechepuka kutoka kwenye tawi lingine kubwa la ukoo au wapi haswa ni asili yake lakini ukoo huu umesamba zaidi katika eneo la ukanda wa mwanzoni wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukiwa unapatikana zaidi maeneo ya ukanda wa juu ukoo huu umesambaa kwa kiasi pia katika vijiji vingine unakopatikana kwa uchache huku ukipatikana kwa wingi zaidi katika ukanda wa juu.
– Ukoo wa Rimoy unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kyou, Kilema.
– Ukoo wa Rimoy unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Ruwa, Kilema.
– Ukoo wa Rimoy unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Makami Juu, Kilema.
Ukoo wa Rimoy sio ukoo mkubwa sana wala maarufu lakini ni ukoo wa watu wanaofanya mambo makubwa, hivyo kunapaswa kuwepo kwa maudhui mengi ya kuhusu ukoo huu. Tunahitaji taarifa zaidi kuhusu ukoo wa Rimoy ili kuongeza kwenye maktaba zote za kuhusu mambo ya wachagga kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye. Taarifa ambazo zitaongeza mshikamano na hamasa zaidi kwa ukoo wa Rimoy kuelekea kujenga umoja imara wa ukoo na kuimarisha zaidi jamii ya wachagga kwa ujumla.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Rimoy.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Rimoy?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Rimoy?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Rimoy?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Rimoy una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Rimoy wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Rimoy kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Rimoy?
9. Wanawake wa ukoo wa Rimoy huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Rimoy?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Rimoy?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Rimoy?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Rimoy kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
Whatsapp/Call +255 754 584 270.