UKOO WA NYANGE.

Nyange ni ukoo wa kichagga unaopatikana kwa wingi katika ukanda wa maeneo ya magharibi ya kati, mashariki ya karibu, mashariki ya kati na mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye historia kubwa sana na ya kipekee katika nchi ya Uchagga, Kilimanjaro. Ukoo wa Nyange ni ukoo wenye watu wengi mashuhuri na wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi katika ujasiriamali taaluma na biashara. Pia wapo wengi katika taasisi mbalimbali za umma na binafsi na hata katika mashirika ya kimataifa.

Kutoka kwenye historia tunafahamu kwamba mababu wa ukoo wa Nyange ndio hao waliokuwa mababu wa ukoo wa watawala katika eneo la himaya ya umangi Mamba ambao ni ukoo wa Moshi. Vizazi hivi vilikuwa na wapiganaji hodari sana ambao waliweza kuwa watawala wa kwanza Kilimanjaro kutawala maeneo makubwa na himaya nyingi za Kilimanjaro kwa pamoja kuanzia magharibi mpaka mashariki. Katika kipindi cha aidha mwishoni mwa miaka ya 1600 au mwanzoni mwa miaka ya 1700 majeshi hayo ya askari yaliweza kutawala karibu eneo lote la Vunjo na nusu ya Rombo huku wakidhibiti maeneo ya upande wa magharibi ya Uchagga, Kilimanjaro ya Uru na Kibosho.

Kutoka kwenye historia inasemekana kwamba Nyange mtoto wa Mangi Munyi aliyewahi kutawala eneo la Mamba alitokea kwenye ukoo wa Teri. Lakini pia katika himaya ya umangi Kilema aliwahi kuwepo Mangi aliyeitwa Nyange katika miaka hiyo ya karne ya 17. Historia inaonyesha kwamba katika karne ya 17 Mangi Nyange wa Kilema aliachiwa kiti cha umangi na baba yake aliyeitwa Mangi Mremi kwa sababu ndiye alikuwa mtoto mkubwa lakini alipinduliwa na kaka yake mdogo aliyeitwa Musuo ambaye alikuwa imara zaidi mjanja na mwenye uchu wa madaraka.

Hivyo Nyange alikimbilia Mamba ambayo ndio ilikuwa himaya yenye nguvu zaidi kwa wakati kwa ajili ya kupata hifadhi na msaada. Wakati huo Mamba ikitawaliwa na Mangi Mapfuluke walimpa msaada wa kijeshi Nyange ambapo Mamba waliivamia Kilema na kumwangusha Musuo kisha kumwondoa madarakani kwenye kiti cha umangi na kumtawalisha upya Nyange. Mangi Nyange ndiye baba yake Mangi Kombo wa Kilema ambaye ni baba yake Mangi Rongoma. Hivyo Mangi Nyange ndiye babu yake Mangi Rongoma ambaye ni mmoja kati ya watawala mashuhuri sana waliowahi kuwa na nguvu sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro.

Kutoka katika historia kwa utafiti uliofanywa na Mary Kathleen Stahl aliyeandika kitabu cha “History of the Chagga People of Kilimanjaro” katika miaka ya 1950’s na mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1960’s anasema kwamba ukoo wa Nyange ndio uliokuwa ukoo wa watawala katika kijiji cha Sango, Old Moshi. Ukoo wa Nyange ulikuwa unatoa watawala wa kijiji cha Sango, Old Moshi tangu zamani zaidi na baadaye kuwa ukoo wa mashuhuri uliokuwa unatoa wachili baada ya taasisi ya umangi kujiimarisha zaidi.

Hata hivyo ukoo wa Nyange umeendelea kusambaa zaidi katika maeneo ya vijiji vingi Kilimanjaro ukipatikana kwa uchache upande wa magharibi lakini kwa wingi kuanzia vijiji vya ukanda wa mashariki ya karibu, kwa wingi zaidi mashariki ya kati na kwa kiasi mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro.

-Hivyo ukoo wa Nyange unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Lyamungo Sinde, Machame.

– Ukoo wa Nyange unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Nyange unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mrumeni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Nyange unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Rauya, Marangu.

– Ukoo wa Nyange unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Samanga, Marangu.

– Ukoo wa Nyange unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

– Ukoo wa Nyange unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ashira, Marangu.

– Ukoo wa Nyange unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Masia, Marangu.

– Ukoo wa Nyange unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kokirie, Mamba.

Licha ya ukongwe wake lakini ukoo wa Nyange ni ukoo uliotawanyika na sana na unapatikana kwa uchache maeneo mengi ambayo bado ni vigumu hata kuyafahamu kwa undani. Tunahitaji taarifa zaidi juu ya ukoo huu unapopatikana na kwa kiwango kikubwa kiasi gani. Tunahitaji kuongeza sana kwenye maudhui ya maktaba ya ukoo wa Nyange kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho katika kujenga hamasa, umoja na mshikamano kuelekea kufanya makubwa.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Nyange.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Nyange?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Nyange?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Nyange?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Nyange una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Nyange wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Nyange kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Nyange?

9. Wanawake wa ukoo wa Nyange huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Nyange?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Nyange?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Nyange?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Nyange kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *