UCHAMBUZI WA KITABU. – SEHEMU YA 1

*Maisha Ya Mchagga Hapa Duniani Na Ahera” By Mangi Petro Itosi Marealle* (Usisahau Ku-share).

Uchambuzi by Mary Assenga.

Mangi Petro Itosi Marealle Alikuwa Mangi Mwitori Wa Vunjo, Uchagga. Baba Yake Alikuwa Ni Mangi Ndegoruo Kilamia “Marealle”, Aliyekuwa Mangi Wa Marangu Ambaye Alikuwa Mtoto Wa Mangi Ndaalio Mjukuu wa Mangi Itosi.

Mangi Petro Itosi Marealle Aliyekuwa Kijana Msomi Na Mwenye Kujitambua Sana Alifanya Utafiti Mkubwa Na Kufikia Mwaka 1946 Aliandika Kitabu Hiki Ili Kuhifadhi Tamaduni Nzuri Na Mambo Mengine Mazuri Ya Nchi Ya Uchagga Yaliyoonekana Kuelekea Kuathiriwa Na Mwingiliano Na Jamii Nyingine Za Kigeni Kutoka Maeneo Tofauti Ya Dunia.

Lengo Hasa La Mwandishi Mangi Petro Itosi Marealle Ilikuwa Ni Kuhifadhi Mambo Haya Mazuri Katika Kitabu Hiki Ambacho Ni Zawadi Kwa Vijana Na Wasichana Wa Uchagga Ambao Anategemea Watatunza Kuenzi Na Kurithisha Tamaduni Hizi Nzuri Kwa Vizazi Vinavyofuata, Alikuwa Anategemea Jamii Hii Ya Wachagga Itaendelea Kustaarabika Na Kukua Bila Kuiacha Misingi Yake Na Tamaduni Zake Ambazo Ndio Zitasababisha Jamii Hii Kuendelea Kuwepo Na Kuendelea Kufanya Vizuri Zaidi Na Zaidi Bila Kupoteza Asili Hii Iliyodumu Kwa Karne Nyingi.

Mwandishi Wa Kitabu Hiki Mangi Petro Itosi Marealle Pia Amegusia Kwa Kiasi Maendeleo Yaliyoletwa Na Wachagga Mpaka Kufikia Mwaka 1946 Kupitia Kile Alichokiita “Ujamaa Wa Wachagga” Chini Ya Chama Cha Ushirika Cha Wachagga Cha KNCU(Kilimanjaro Native Cooperation Union) Ambacho Ndio Chama Kikongwe Kabisa Cha Ushirika Katika Barani Afrika Kilichoanzishwa Mwaka 1933.

Sasa Twende Pamoja Katika Uchambuzi Wa Kitabu Hiki Ambacho Alikiandika Kama “Dedication” Kwa Vijana Na Wasichana Wa Uchagga Akitarajia Kutokea Hapa Wafanye Mambo Makubwa Na Pia Kuandika Vitabu Vingine Vingi Na Bora Zaidi.

Maisha Ya Mchagga Hapo Zamani Yalikuwa Katika Mpangilio Kuanzia Kabla Mimba Haijatungwa Mpaka Mwisho Wa Maisha Yake Hapa Duniani.

Itaendelea.

Urithi Wetu Wachagga.

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *