– Leo Tarehe 10/Novemba Ndio Siku Ya Wachagga, “Chagga’s Day”.
– Ni Siku Maalum Kwa Wachagga Wote Waliopo Mijini na Vijijini, Ndani na Nje Ya Kilimanjaro na Ndani na Nje Ya Nchi Pia Kukumbuka Siku Ambayo Watangulizi Wetu Waliiazimia Siku Hii Kama Siku Maalum Ya Kupumzika na Kusherehekea Maendeleo Ya Wachagga.
– Ni Siku Kubwa Iliyosherehekewa Kwa Shamra Shamra za Hali Ya Juu na Wachagga wa Rika Zote Ambayo Iliambatana Hotuba Nyingi Mbalimbali za Kuhamasisha Maendeleo Ya Uchagga Katika Nyanja Zote Kuanzia Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa, Kiutamaduni na Hata Maendeleo Makubwa Ya Ustaarabu Uliokuwa Unakuwa Kwa Kasi Ndani Ya Jamii Ya Wachagga. Ni Siku Iliyopendwa na Kujivuniwa na Wachagga Wote Ambao Walifurahia Sana Hatua Kubwa za Kimaendeleo Walizokuwa Wanaendelea Kupiga Kwa Kasi Kubwa Katika Kila Eneo.
– Sasa Kwa Wachagga wa Leo Siku Hii Ambayo Tumeamua Kuirudisha Kuendelea Kuisherehekea, Inakwenda Kuwa Ni Siku Ya Kuenzi na Kujivunia Mambo Makubwa Waliyofanikisha Watangulizi Wetu Mpaka Kufikia Miaka Ya 1960’s Wakati Huo Huo na Sisi Tukiendelea Kujitafuta Ili Kujipata Katika Njia Ambayo Inakwenda Kurudisha Ule Utukufu Uliofifia. Siku Hii Ambayo Inaendelea Kutujengea Ari, Umoja na Mshikamano Kupitia Sherehe Tulizoziandaa Tunaitumia Kutafakari Zaidi Katika Kuendelea Kuboresha Yale Tunayoazimia Kuyafanikisha Kama Wachagga wa Leo Kwa Kizazi Cha Sasa na Kile Kinachokuja. Hivyo Tuna Jukumu na Wajibu wa Kujifunza Mambo Makubwa Yaliyofanywa na Wazee Wetu na Kuyahadithia Kwa Watoto ili Kuotesha Mbegu Ambayo Inaendelea Kukomaa Katika Akili Zao.
– Jambo Muhimu Kufanya Kwa Siku Hii Maalum Ya Leo Ni Kujifunza Jambo Lolote Muhimu Kubwa na La Kujivunia Walilofanya Watangulizi Wetu Zamani na Kisha Kulifundisha Kwa Watoto au Vijana Wadogo Unaoishi Nao Nyumbani au Mtaani. Sambamba na Hilo Unaweza Kusherehekea Pia Kwa Hadithi na Nyimbo, Vyakula na Vinywaji Vya Kichagga Huku Ukijikumbusha Umuhimu wa Siku Hii.
– Muhimu Zaidi Kwa Walioko Dar es Salaam na Hata Maeneo Ya Karibu, Kuanzia Leo Jioni Kutakuwa na Mkesha wa Siku Ya Wachagga Pale Katika Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam na Kesho Ndio Itakuwa Kilele cha Maadhimisho Ya Siku Ya Wachagga Ambapo Kutakuwa na Kila Aina Ya Burudani na Shamra Shamra za Sherehe Hiyo. Watu Wengi Watahudhuria na Kutakuwa na Mafundisho na Hotuba Mbalimbali. Wote Tutakuwepo Kesho Katika Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama, Dar Es Salaam na Nakala za Kitabu cha, “Miaka 700 Ya Wachagga” Zitapatikana Kwa Bei Ya Punguzo.
UJUMBE WA KUTUMA KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI SIKU HII MAALUM YA WACHAGGA NI…,
“Siku Hii Ya Wachagga Ikawe Yenye Baraka Kwako na Ikaendelee Kuongeza Hamasa na Kuimarisha Umoja na Mshikamano Miongoni Mwetu Wachagga Katika Kuendelea Kupiga Hatua Kubwa Zaidi Kuyafikia Maendeleo Makubwa Katika Nyanja Zote”.
HERI YA SIKU KUU YA WACHAGGA KWENU WOTE.
HAPPY CHAGGA’S DAY TO Y’ALL.
Urithi Wetu Wachagga
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp +255 754 584 270.