– Mangesho ni ukoo wa wachagga unaopatikana katika eneo la mwishoni mwa ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga na kwa kiasi katika eneo la katikati la ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Hata hivyo bado hakuna taarifa za uhakika kama ukoo wa Mangesho wa eneo hili la katikati ya ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga na ukoo wa Mangesho wa eneo la mwishoni mwa ukanda wa mashariki ya kati una mahusiano ya moja kwa moja.
– Kutoka kwenye historia katika simulizi na maandiko ya karne ya 19 na 20 na ukiwa umetajwa pia kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” inaaminika kwamba katika eneo hili la mwishoni mwa ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro ukoo wa Mangesho ndio ukoo mkongwe zaidi kuweka makazi yake katika kijiji cha Kondeni, Mwika Kusini. Baadaye ndio zilifuatia koo za Ngomuo, Teemba na Lyimo waliokuja baadaye kabisa wakitokea Lyamrakana, Marangu. Ukoo wa Mangesho walikuwa ni wafugaji hodari wa mifugo na walishuka kutokea kwenye ukanda juu kabisa wa eneo la Msae maeneo ya msituni na kuweka makazi ya kudumu katika kijiji cha Kondeni, Mwika kusini pengine mwishoni mwa karne ya 16 au karne ya 17.
– Kwa upande wa ukoo wa Mangesho wanaopatikana katika ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga katika eneo Keni, Mashati, Rombo historia yao inakwenda mpaka aidha mwanzoni mwa karne ya 19 au mwishoni mwa karne ya 18 ambapo wana mahusiano ya karibu au ni tawi la ukoo wa Urassa wa Keni ya Mkulya katika eneo la Mashati, Rombo. Ukoo huu wa Mangesho ya Keni ya Mkulya, Mashati, Rombo kama unavyozungumziwa kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” sio mkubwa sana wala hauko kwa wingi kama Mangesho wa eneo la Vunjo na bado hakuna uhakika kama kuna mahusiano ya moja kwa moja baina ya matawi hayo mawili ya ukoo wa Mangesho.
– Ukoo wa Mangesho kama jinsi ulivyokuwa ni ukoo hodari kwa mifugo kabla na baada ya karne ya 19 lakini hata sasa ni ukoo wenye watu wengi makini wanaofanya vizuri sana kitaaluma na katika shughuli za biashara na ujasiriamali. Pia wanapatikana katika taasisi mbalimbali za serikali na binafsi ndani na nje ya nchi.
– Ukoo wa Mangesho haujasambaa katika vijiji vingi vya Uchagga, Kilimanjaro hivyo.
– Ukoo wa Mangesho unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kondeni, Mwika.
– Ukoo wa Mangesho unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Keni, Mashati, Rombo.
– Ukoo wa Mangesho unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kiraeni, Mashati, Rombo.
Ukoo wa Mangesho ni ukoo wenye historia ndefu zaidi ya namna vizazi vyake vilivyokwenda na kuishia kuwa. Hivyo tunahitaji kupata maudhui zaidi ya ukoo wa Mangesho ili kuweka katika maktaba ya ukoo huu sambamba na maktaba ya wachagga kwa ujumla kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vinavyokuja. Lengo la kukusanya maudhui haya ni kuweza kujenga hamasa, umoja na mshikamano kwa kizazi kinachokuwa katika kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ukoo na jamii nzima ya wachagga.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Mangesho.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mangesho?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mangesho?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mangesho?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mangesho una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Mangesho wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mangesho kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mangesho?
9. Wanawake wa ukoo wa Mangesho huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mangesho?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mangesho?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mangesho?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mangesho kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp +255 754 584 270.