– Tenga na Mtenga ni ukoo wa mkongwe na wenye umashuhuri sana kwa baadhi ya maeneo ya Uchagga, Kilimanjaro ambao umeoyesha umahiri mkubwa katika nyanja mbalimbali katika nyakati tofauti tofauti za kihistoria. Hata hivyo japo hakuna taarifa za kutosha zinazoweza kuunganisha matawi ya ukoo huu kwa usahihi kwa maeneo yote zinakopatikana katika ardhi ya Uchagga, Kilimanjaro lakini ukoo huu wa Tenga/Mtenga unapatikana kwa wingi kuanzia maeneo ya ukanda wa mashariki ya karibu ya Uchagga, Kilimanjaro, maeneo ya ukanda wa mashariki ya kati na kwa wingi pia katika eneo la mwanzoni na katikati la ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro.
– Kutoka kwenye historia ukoo wa Tenga/Mtenga umekuwa ni ukoo wa watu mashuhuri waliofanya mambo makubwa katika historia ya Uchagga, Kilimanjaro na katika himaya ya umangi ya Kirua-Rombo katika eneo ambalo kwa sasa ni tarafa ya Mashati, Rombo ulikuwa ni ukoo wa watawala aliotokea Mangi maarufu kidogo wa mwisho mwisho katikati ya karne ya 20 aliyekuwa katika baraza la halmashauri kuu ya wachagga Mangi Baltazari Mashinga. Ndani ya kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” ukoo huu wa Mtenga wa tawi la Kirua Rombo umezungumziwa na vizazi vyake na namna ulivyotawala katika himaya ndogo ya umangi Kirua-Rombo, katika eneo ambalo kwa sasa ni tarafa ya Mashati, Rombo.
– Wachagga wa ukoo wa Tenga/Mtenga wameendelea kuwa ni watu makini sana wanaofanya vizuri katika taaluma na fani mbalimbali kuanzia biashara, ujasiriamali na katika mashirika na taasisi za ndani na nje ya nchi. Moja kati ya wachagga mashuhuri sana kuwa kutokea katika ukoo wa Tenga aliwahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha soka Tanzania TFF Leodgar Tenga ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji mzuri miaka ya zamani japo bado hatujaweza kupata taarifa sahihi za kijiji anachotokea.
– Kutoka kwenye historia pia ukoo wa Tenga ndio ukoo ulioweka historia kwa kutoa mchagga wa kwanza mkristo katika historia ya wachagga, Kilimanjaro katika karne ya 19 aliyejulikana kwa jina la Yohanna Nene Tenga sambamba na mchagga mwingine kutoka kwenye ukoo wa Ringo aliyejulikana kwa jina la Tomasi Kitimbo Ringo katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi waliobatizwa katika eneo lililopewa hadhi ya utakatifu na wakristo la Kitimbirihu katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi. Hadithi nzima ya tukio hilo na historia yote ya ukristo Uchaggani imeelezwa kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga”.
– Ukoo wa Tenga/Mtenga umeendelea kukua zaidi na kusambaa maeneo mbalimbali ya vijiji vingi zaidi Uchaggani kuanzia katikati kuelekea mashariki zaidi. Hivyo,
– Ukoo wa Tenga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mnini, Uru.
– Ukoo wa Tenga unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.
– Ukoo wa Tenga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.
– Ukoo wa Tenga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Shia, Old Moshi.
– Ukoo wa Tenga unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Sango, Old Moshi.
– Ukoo wa Tenga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Pofo, Kilema.
– Ukoo wa Tenga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Masaera, Kilema.
– Ukoo wa Tenga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ngangu, Kilema.
– Ukoo wa Tenga/Mtenga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mengeni Chini, Keni, Rombo.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mengeni-Kitasha, Keni, Rombo.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Aleni Chini, Keni, Rombo.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Makiidi, Mkuu, Rombo.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mokala, Mkuu, Rombo.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Ikuini, Ushiri/Ikuini, Mkuu, Rombo.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mrao, Mraokeryo, Mashati, Rombo.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Kirua-Rombo, Mashati, Rombo.
– Ukoo wa Mtenga unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kiraeni, Mashati, Rombo.
Ukoo wa Tenga/Mtenga ni ukoo wenye umashuhuri mkubwa na wenye historia ndefu sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro, ni ukoo wenye matawi mengi yaliyogawanyika sana lakini bado kuna ombwe kubwa la taarifa juu ya namna ukoo huu umegawanyika na kutengeneza matawi yake. Hivyo tunahitaji kupata maudhui zaidi ya ukoo wa Mtenga na namna ulivyotawanyika maeneo mbalimbali ya Uchagga, Kilimanjaro ili kuyaweka katika maktaba ya ukoo huu sambamba na maktaba ya wachagga kwa ujumla kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vinavyokuja. Lengo la kukusanya maudhui haya ni kuweza kujenga hamasa, umoja na mshikamano kwa kizazi kinachokuwa kuweza kupata pa kuanzia katika kuelekea kujitambua zaidi na kufanya makubwa kwenye maisha kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ukoo na jamii nzima ya wachagga.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Tenga/Mtenga.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Tenga/Mtenga?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Tenga/Mtenga?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Tenga/Mtenga?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Tenga/Mtenga una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Tenga/Mtenga wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Tenga/Mtenga kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Tenga/Mtenga?
9. Wanawake wa ukoo wa Tenga/Mtenga huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Tenga/Mtenga?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Tenga/Mtenga?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Tenga/Mtenga?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Tenga/Mtenga kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp/Call +255 754 584 270.