UKOO WA SOKA/KISOKA/MSOKA.

– Msoka/Soka/Kisoka ni ukoo maarufu wa wachagga unaopatikana katika maeneo ya ukanda wa magharibi ya kati, magharibi ya karibu na mashariki ya karibu ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Msoka na wengine Soka na Kisoka ni watu wanaofanya vizuri zaidi katika maeneo mbalimbali kwa mfano kitaaluma ukoo wa Msoka wanaonekana kufanya vizuri zaidi na katika biashara na ujasiriamali wachagga wa ukoo wa Soka na Kisoka wanafanya vizuri zaidi.

– Kutoka kwenye historia bado hatuna taarifa nyingi za uhakika zinazoeleza kwa undani chanzo na asili ya ukoo wa Msoka/Soka/Kisoka kwa Uchaggani na namna ukoo huu umesambaa katika maeneo na vijiji zaidi vya Uchagga, Kilimanjaro. Hata kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” haujazungumziwa chanzo chake lakini ni ukoo wenye watu wasomi mashuhuri wengi hivyo kuna fursa na nafasi kubwa ya kuufahamu zaidi kupitia watu wa ukoo huu.

– Ukoo wa Msoka umesambaa katika vijiji vingi japo sio kwa wingi sana lakini una matawi mengi ambayo mengi hayashirikiani sana kwa miaka ya sasa, hivyo.

– Ukoo wa Soka unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Manushi Ndoo, Kibosho.

– Ukoo wa Soka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Kombo, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kitandu, Kibosho.

– Ukoo wa Soka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mloe, Kibosho.

– Ukoo wa Soka unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kindi Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kindi Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Soka unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kindi Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sambarai, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Maua. Kibosho.

  • Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Otaruni, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kirima Juu, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kirima Kati, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Boro, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Singachini, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Singa, Kibosho.

– Ukoo wa Kisoka unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Mweka, Kibosho.

– Ukoo wa Msoka unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Longuo, Uru Kusini.

– Ukoo wa Msoka unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kariwa, Uru.

– Ukoo wa Msoka unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mrawi, Uru.

– Ukoo wa Msoka unapatikana kwa wingi katika kijiji cha Msuni, Uru.

– Ukoo wa Msoka unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Korini Juu, Mbokomu, Old Moshi.

– Ukoo wa Msoka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Msoka unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

Ukoo wa Soka/Kisoka/Msoka ni ukoo maarufu na wenye matawi mengi yaliyogawanyika sana katika vijiji vya Uchagga, Kilimanjaro, lakini bado kuna ombwe kubwa la taarifa juu ya namna ukoo huu umegawanyika na kutengeneza matawi yake. Hivyo tunahitaji kupata maudhui zaidi ya ukoo wa Soka/Kisoka/Msoka na namna ulivyotawanyika maeneo ya vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro ili kuyaweka katika maktaba ya ukoo wa Soka/Kisoka/Msoka sambamba na maktaba ya wachagga kwa ujumla kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vinavyokuja. Lengo la kukusanya maudhui haya ni kuweza kujenga hamasa, umoja na mshikamano kwa kizazi kinachokuwa na kilichopo sasa kuweza kupata pa kuanzia katika kuelekea kujitambua zaidi na kufanya makubwa kwenye maisha kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja, ukoo na jamii nzima ya wachagga.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Soka/Kisoka/Msoka.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Soka, Kisoka na Msoka?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Soka/Msoka/Kisoka?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Soka/Kisoka/Msoka?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Soka/Msoka/Kisoka una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Soka, Kisoka au Msoka wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Soka/Msoka/Kisoka kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Soka/Msoka/Kisoka?

9. Wanawake wa ukoo wa Soka/Msoka/Kisoka huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Soka/Msoka/Kisoka?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Soka/Msoka/Kisoka?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Soka/Kisoka/Msoka?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Soka/Msoka/Kisoka kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

3 Comments

  1. Nmepitia makalai nkaona katika vijiji vilivyo tajwa ukoo wa Kisoka yako mwendo yalio saulika kama vile sanya juu kuna ukoo wa Kisoka shiri matunda nako kuna ukoo wa Kisoka chekereni ya bonite nako kuna ukoo wa Kisoka japo maeneo haya3 nliotaja wapo wachache sio wengi sana lakini wapo wakisoka

    1. Okay, ahsante sana kwa nyongeza.

  2. 탑플레이어 포커 머니상 – 포커 머니 거래의 미래를 함께 만들어가요! 끊임없는 혁신과 발전을 통해 탑플레이어 머니상에서 포커 머니 거래의 미래를 디자인하고 있습니다.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *