UKOO WA FOYA.

– Foya ni ukoo wa wachagga wanaopatikana zaidi katika eneo la katikati au magharibi ya kati ya nchi ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wenye watu makini sana ambapo katika miaka ya zamani sana ulikuwa ni moja kati ya koo mashuhuri zilizotoa mainjinia wataalamu wa miundombinu za umwagiliaji na mifereji ya maji kwa ujumla. Hata sasa ukoo wa Foya ni ukoo wa watu wasomi na wanaofanya vizuri sana katika maeneo mbalimbali hususan kitaaluma.

– Kutoka kwenye historia ukoo wa Foya umezungumziwa kwa undani kama ukoo wenye asili na chimbuko lake katika maeneo ya nyanda za juu za Mbokomu katika kijiji cha Tema kwenye kitongoji chao cha asili kiitwacho Foyeni. Hivyo ukoo wa Foya ni kati ya zile koo chache ambazo zina maeneo yao rasmi yaliyoitwa kwa jina la ukoo huo katika eneo la Foyeni, kijiji cha Tema, kata ya Mbokomu, Old Moshi. Taasisi nyingine katika kijiji cha Foyeni kilichobeba jina la ukoo huu ni shule ya msingi Foyeni na kanisa la KKKT Usharika wa Foyeni, Mbokomu.

– Ukoo wa Foya pia umezungumziwa zaidi kwa kina katika kitabu chetu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” asili yake na chimbuko lake. Eneo la Foyeni pia limezungumziwa kama eneo lenye hali nzuri sana ya hewa na chemchemi nyingi za maji ambapo ndio maeneo haya ya Foyeni kwenye chimbuko la ukoo wa Foya unakopatikana mti mrefu kuliko yote Afrika aina ya Mkukusu katika kijiji cha Tema, kata ya Mbokomu, Old Moshi. Hadithi yote kuhusu mti huu mrefu zaidi kuliko miti mingine yote Afrika na mazingira yake imejadiliwa kwa kina kwenye kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga”.

– Ukoo wa Foya ambao unatambulika na historia kama ukoo mkongwe sana katika eneo la ukanda wa juu wa eneo la Mbokomu umeendelea kukua na kusambaa katika maeneo ya vijiji mbalimbali ndani ya Mbokomu na hata nje. Hivyo ukoo wa Foya unapatikana sehemu mbalimbali zifuata.

– Ukoo wa Foya unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Tema, Mbokomu, Old Moshi.

– Ukoo wa Foya unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Korini Juu, Mbokomu hasa katika kitongoji cha Fukeni.

– Ukoo wa Foya unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Korini Kati, Mbokomu.

– Ukoo wa Foya unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Korini Kusini, Mbokomu.

– Ukoo wa Foya unapatikana kwa uchache katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.

– Ukoo wa Foya unapatikana kwa uchache Kirua Vunjo Magharibi.

Tunahitaji kufahamu zaidi kuhusu ukoo wa Foya ili kuongeza maudhui zaidi kwenye maktaba ya ukoo huu na maktaba ya wachagga kwa ujumla kwenye maktaba ya mitandaoni na hata baadaye katika nakala ngumu. Kuna mengi yanapaswa kuibuliwa ili kuhakikisha kizazi cha sasa na kinachokuja kinapata kujitambua zaidi na kujiamini katika kuelekea kufanya mambo makubwa kwenye maisha.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Foya.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Foya?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Foya?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Foya?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Foya una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Foya wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Foya kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Foya?

9. Wanawake wa ukoo wa Foya huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Foya?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Foya?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Foya?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Foya kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook).

urithiwetuwachagga@gmail.com

Whatsapp/Call +255 754 584 270.

You may also like...

Popular Posts

2 Comments

  1. Emma RAJAB Foya says:

    Historically
    Uko wa wafoya ulianzia old moshi kirua chini ya uongozi wa Mangi
    Na baadaye wakaahamia Foyeni kijiji cha Tema
    Na kwa ukoo wa wafoya wanawake wanaitwa
    Mafude
    Mahoo
    Na Makyura
    Kwa nini
    Babu wa kwanza ambaye ni Foya alikuwa na wake wa 3 wenye Majina hayo na ndio
    Maana leo hii unasikia
    Foya ya mafude
    Foya ya mahoo
    Foya ya makyura
    .ukoo wa foya ni watu wanaopenda kufanya kazi
    Lakini wanaongea sana
    Ila wanatofautia na hasili ya bibo wa kwanza
    Foya ya mafude wao wanaongea sana
    Foya ya mahoo ni wapole kwa hasili yao
    Na foya ya makyura
    Ni wapole kupitiliza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *