– Lyakurwa ni ukoo mashuhuri wa kichagga unaopatikana zaidi mwanzoni mwa ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro. Huu ni ukoo wa watu mashuhuri na wenye historia kubwa inayokwenda mbali sana katika eneo la himaya ya umangi Mengwe ambayo baadaye ilikuja kuitwa himaya ya umangi Keni-Mriti-Mengwe.
– Ukoo wa Lyakurwa na koo nyingine kadhaa za eneo hili kama vile Salia, Salema, Moshi n.k. zimetoa watawala mbalimbali wa himaya ya umangi Mengwe tangu zamani. Ukoo huu pia ni ukoo ambao katika miaka ya mwanzoni mwa karne ya 20 ulitengeneza uhasama mkubwa na ukoo wa watawala katika himaya ya umangi Keni na mivutano hii ilipelekea mpaka mapigano yaliyozua uadui mkubwa. Kwa sehemu mivutano hiyo ilisababishwa na kugombea nafasi ya kutawala eneo lote la himaya ya umangi mpya ilikuja kuitwa Keni-Mriti-Mengwe.
– Moja kati ya watawala mashuhuri wa eneo hili waliowahi kutokea kwenye ukoo huu wa Lyakurwa ni pamoja na Salema na mtoto wake Salia. Ukoo wa Lyakurwa umeendelea kusambaa zaidi katika maeneo haya na maeneo ya ukanda wa mwanzoni mwa ukanda wa mashariki ya mbali ya Uchagga, Kilimanjaro na hivyo unapatikana kwa wingi sana kwa baadhi ya vijiji na kwa uchache kwa vijiji vingine.
– Hivyo ukoo wa Lyakurwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahango, Mahida, Rombo.
– Ukoo wa Lyakurwa unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Mamsera Juu, Mamsera, Rombo.
– Ukoo wa Lyakurwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mamsera Kati, Mamsera, Rombo.
– Ukoo wa Lyakurwa unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Mengwe Juu, Mengwe, Rombo. Kimsingi karibu nusu ya kijiji cha Mengwe juu, Rombo umetawala ukoo wa Lyakurwa.
– Ukoo wa Lyakurwa unapatikana wa wingi sana sana katika kijiji cha Ngareni, Kata ya Ngoyoni, Mengwe, Rombo.
– Ukoo wa Lyakurwa unapatikana kwa wingi sana sana sana katika kijiji cha Mengwe Chini, Mengwe, Rombo.
– Ukoo wa Lyakurwa unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Manda Chini, Mengwe, Rombo.
– Ukoo wa Lyakurwa unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Manda Juu, Mengwe, Rombo.
– Ukoo wa Lyakurwa unapatikana kwa uchache sana katika kijiji cha Mengeni Chini, Keni, Rombo.
Ukoo wa Lyakurwa ni ukoo wa watu mashuhuri na wenye wasomi wengi na watu makini. Hata hivyo bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu, hivyo kuna maswali mengi ambayo hayajajibiki kuhusu ukoo wa Lyakurwa. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Lyakurwa ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.
Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Lyakurwa.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Lyakurwa?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Lyakurwa?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Lyakurwa?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Lyakurwa una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?
5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?
6. Wewe ni Lyakurwa wa kutokea kijiji gani?
7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Lyakurwa kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Lyakurwa?
9. Wanawake wa ukoo wa Lyakurwa huitwaje, na kwa nini?
10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Lyakurwa?
11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Lyakurwa?
12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Lyakurwa?
13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Lyakurwa kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.
Urithi Wetu Wachagga (Facebook).
urithiwetuwachagga@gmail.com
Whatsapp/Call +255 754 584 270.