UKOO WA MCHAKI/CHAKI.

– Mchaki/Chaki ni ukoo wa wachagga unaopatikana katika maeneo ya vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro kuanzia ukanda wa katikati kuelekea ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro. Wachagga wa ukoo wa Mchaki/Chaki kwa ujumla ni watu makini na kuna wengi ambao wanafanya vizuri sana katika nyanja mbalimbali kuanzia ufundi, kitaaluma, biashara na ujasiriamali na mpaka kwenye taasisi na mashirika makubwa ya ndani na nchi ya nchi.

– Ukoo huu wa Mchaki/Chaki japo haujamzungumziwa sana katika kitabu cha “Miaka 700 Ya Wachagga” lakini ni ukoo wenye umashuhuri sana katika maeneo unakopatikana na kuna vijiji ambapo unapatikana kwa wingi sana.

– Ukoo wa Mchaki/Chaki hasa wanaopatikana katika ukanda wa mashariki ya kati ya Uchagga, Kilimanjaro wengi pia ni wasomi wazuri na wenye mshikamano sana katika ngazi ya ukoo. Ukoo huu licha ya kwamba chimbuko lake bado hatujaweza kulifahamu kwa uhakika ndani ya Uchagga, Kilimanjaro lakini umesambaa katika eneo la katika zaidi ya Uchagga japo sio kwa wingi sana lakini katika vijiji mbalimbali.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Mowo, Old Moshi.

– Ukoo wa Chaki na Mchaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Sango, Old Moshi.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa wingi sana sana katika kijiji cha Manu, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Koresa, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Nganjoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Chaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.

– Ukoo wa Mchaki unapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mkyashi, Kilema.

– Ukoo wa Mchaki unapatikana kwa wingi kiasi katika kijiji cha Sembeti, Marangu.

Ukoo wa Mchaki/Chaki ni ukoo wenye watu wengi na wasomi wengi pia na watu wengi makini na wenye umoja na mshikamano sana wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali. Lakini huu ni ukoo ambao licha ya kuwa na wasomi wengi bado hakuna maudhui mengi yaliyoandikwa kuhusu ukoo huu. Tunahitaji kufahamu mengi zaidi kuhusu ukoo wa Mchaki/Chaki na namna ulivyotengeneza matawi yake katika maeneo ya vijiji mbalimbali vya Uchagga, Kilimanjaro ili kuhifadhi maudhui mengi zaidi katika maktaba ya ukoo huu na jamii ya wachagga kwa ujumla. Tunahitaji kuhifadhi taarifa na maudhui ya ukoo wa Mchaki/Chaki katika maktaba za mitandaoni na maktaba halisi pia kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja kujitambua na kujijengea kujiamini zaidi kuelekea kufanya makubwa kwenye maisha katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwenye ukoo, kwenye ngazi ya ukoo na jamii nzima ya wachagga kwa ujumla.

Karibu kwa Mchango zaidi wa mawazo na taarifa kuhusu ukoo wa Mchaki/Chaki.

1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Mchaki/Chaki?

2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Mchaki/Chaki?

3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Mchaki/Chaki?

4. Kama wewe ni wa ukoo wa Mchaki/Chaki una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu?

5. Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani?

6. Wewe ni Mchaki/Chaki wa kutokea kijiji gani?

7. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Mchaki/Chaki kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?

8. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Mchaki/Chaki?

9. Wanawake wa ukoo wa Mchaki/Chaki huitwaje, na kwa nini?

10. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Mchaki/Chaki?

11. Ni watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Mchaki/Chaki?

12. Kuna mnyama yeyote ambaye labda ni mwiko kuliwa na wachagga wa ukoo wa Mchaki/Chaki?

13. Kuna ukoo ambao hawaruhusiwi kuoana na Wako-Mchaki/Chaki kwa sababu zilizowahi kuwepo miaka ya zamani au nyingine zozote?

Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.

Ahsanteni.

Wiki ijayo tutaendelea na ukoo mwingine.

www.wachagga.com

Urithi Wetu Wachagga (Facebook)

Whatsapp +255 754 584 270.

urithiwetuwachagga@gmail.com

You may also like...

Popular Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *