– Ukoo wa Macha ni ukoo mkubwa wenye idadi kubwa ya watu na uliosambaa maeneo mengi ya uchagga Kilimanjaro. Huu ni ukoo mkongwe na mashuhuri sana katika historia ya wachagga Kilimanjaro, wenye matawi mengi na unaoweza kuhesabu vizazi vingi vilivyopita.
– Kutoka kwenye historia tawi la ukoo wa Macha ambalo ni kongwe zaidi linapatikana katika kijiji cha Kidia, Old Moshi na linahusisha ukoo wa Macha uliokuja kugawanyika mara mbili na kupata ukoo wa Mshiu na Macha. Tawi hili la ukoo wa Macha wa kijiji cha Kidia, Old Moshi ambao kuna wakati ulikuwa unajulikana kama Mshiu-Macha ulisifika sana zamani kwa kutoa wasomi mahiri wa historia na tamaduni za wachagga kwa karne nyingi zilizopita.
– Inasemekana kwamba makazi ya mwanzoni ya ukoo wa Macha yalikuwa katika ukanda wa juu zaidi wa kijiji cha Kidia ambayo kwa sasa eneo la msitu wa mlima Kilimanjaro. Hata hivyo baadaye wakiongozwa na Mzee wa ukoo aliyeitwa Mrashi waliweka makazi ya kudumu katika kijiji cha Kidia kama eneo lao la asili kabla ya baadaye kusambaa katika maeneo mengine mbalimbali ya Uchaggani, Kilimanjaro.
– Inasemekana kwamba ukoo wa Macha hawakuwa wafugaji sana wa mifugo bali walikuwa zaidi ni wakulima hodari na warina asali pori. Wachagga wa ukoo wa Macha walikuwa ni watu mashuhuri na wenye kuheshimika sana na mara nyingi utawala wa Mangi uliteuwa wachili kutoka kwenye ukoo wa Macha kutokana na ukongwe wake na heshima kubwa waliyokuwa nayo.
– Wachagga wa ukoo wa Macha wameendelea kuwa ni watu mashuhuri sana na walioenea maeneo mbalimbali na wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Kilimanjaro na hata nje ya nchi. Ukoo huu umetoa wasomi, wafanyabiashara, wanasiasa na wengi mashuhuri katika taaluma mbalimbali.
– Wachagga wa ukoo wa Macha wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Okaseni, Uru.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Kariwa, Uru.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa kiasi katika vijiji vya kata ya Shimbwe, Uru.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa kiasi katika kijiji cha Mnini, Uru.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Korini chini, Mbokomu.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Korini Juu, Mbokomu.
– Ukoo wa Macha na Mshiu wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kidia, Old Moshi.
– Ukoo wa Macha na Mshiu wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Tela, Old Moshi.
– Ukoo Macha wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mahoma, Old Moshi.
– Ukoo wa Macha na Mshiu wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kikarara, Old Moshi.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Mdawi, Old Moshi.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Shia, Old Moshi.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika vijiji vya Sango na Mowo, Old Moshi.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Nduoni, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kwamare, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Yamu, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Iwa, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana katika kijiji cha Kanango, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi sana Marua, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana kwa wingi katika kijiji cha Kanji, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Nganjoni na Mrumeni, Kirua Vunjo.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Leghomulo, Kilema.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Sembeti, Marangu.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Samanga, Marangu.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Maring’a Juu, Mwika.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Mrimbo Uuwo, Mwika.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Kiruweni, Mwika.
– Ukoo wa Macha wanapatikana katika kijiji cha Kimangaro, Mwika.
– Hata hivyo licha ya kwamba ukoo wa Macha wamekuwa ni wasomi mahiri wa historia na tamaduni za jamii ya wachagga kwa karne nyingi zilizopita lakini bado kuna uhaba mkubwa wa taarifa juu ya ukoo huu mkongwe na mashuhuri. Tunajitaji kupata taarifa zaidi ili kuongeza kwenye utafiti unaoendelea sambamba na kufahamu maeneo zaidi unakopatikana ukoo wa Macha ili kurahisha kazi ya kufanya utafiti zaidi.
– Pia taarifa zaidi zinaongeza maudhui mengi zaidi juu ya ukoo husika na wachagga kwa ujumla hivyo kuongeza hamasa ya kujenga mshikamano kuelekea kufanya makubwa kuanzia katika ngazi ya ukoo mpaka ngazi ya mtu mmoja mmoja. Karibu kwa mchango zaidi wa mawazo juu ya ukoo wa mashuhuri wa Macha.
1. Je, unafahamu nini kuhusiana na ukoo wa Macha?
2. Unafikiri ni kijiji gani ambacho kimesahaulika kutajwa lakini kuna ukoo wa Macha?
3. Kijijini kwenu kuna ukoo wa Macha?
4. Kama wewe ni wa ukoo wa Macha una nini cha kutuambia kuhusu ukoo wenu? Huwa mna maadhimisho yoyote au sherehe za ukoo mwezi gani? Wewe ni Macha wa kutokea kijiji gani?
5. Bado kuna ushirikiano wowote katika matukio mbalimbali muhimu na ndugu zenu wengine wa matawi ya ukoo wa Macha kutoka maeneo mengine ya Uchaggani?
6. Ni tabia gani unazozifahamu za wachagga wa ukoo wa Macha?
7. Wanawake wa ukoo wa Macha huitwaje?
8. Una rafiki yako yeyote wa kutokea kwenye ukoo wa Macha?
9. Watu gani mashuhuri unaowafahamu kutoka kwenye ukoo wa Macha?
Karibu kwa Mchango zaidi au maswali.
Ahsanteni.
Kesho tutaendelea na ukoo mwingine.
Whatsapp +255 754 584 270